Jumanne, 04 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

“Khiyana ya ‘Ruwaibidha’ (watawala wasiostahiki) na kuidhinishwa kwa mpango wa Trump kwa gharama ya damu ya mashahidi wa Palestina”

Baada ya hotuba ya rais wa Marekani kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa – ambayo asili ilikusudiwa kuhakiki kadhia ya Palestina – na katika wakati ambapo, kwa msimamo mmoja kutoka zaidi ya dola 150 kati ya dola 193 za Umoja wa Mataifa, “dola ya Palestina” tayari imetambuliwa, Rais Trump aliikejeli jumuiya ya kimataifa kwa kuyaita maneno ya “viongozi” kama “domo tupu.” Pia alikejeli makubaliano ya kimazingira, akaiichukulia mikataba ya uhamiaji kuwa ya kudharauliwa, na akakashifu mchakato wa Ulaya wa kuitambua Palestina kwa kuiita udhaifu. Hotuba yake ilionekana kama dua ya mwisho ya mazishi (fatiha) iliyosomwa juu ya makubaliano ya kimataifa, madai ya mtazamo wa upande mmoja wa Amerika katika masuala ya kimataifa, na tangazo la kulazimisha rai yake juu ya Mashariki ya Kati – haswa suala la Palestina.

Kutambuliwa kwa Dola ya Palestina Kutambuliwa kwa Mayahudi Kunyakua 78% ya Palestina!

Uingereza, Canada, Australia na Ureno zililitambua ile inayoitwa “Dola ya Palestina,” na kufuatiwa na nchi kadhaa katika mkutano wa ngazi ya juu wa kimataifa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa uliofanyika kuanzia Septemba 22-30, 2025, na ulioongozwa na Ufaransa na Saudi Arabia. Utambuzi huu ulikaribishwa na watawala Ruwaibidha (wajinga wasio na maana) wa Waislamu, pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Waarabu. Jambo la kushangaza ni kwamba, ilikaribishwa pia na mashirika ya Kipalestina, ambayo yanaona kuwa ni matunda ya uthabiti wao, kana kwamba Palestina imekombolewa na na umbile la Kiyahudi kung'olewa!

Ametokea kwa Mlango, Anaingia kwa Dirisha

Kwa mara nyengine tena, Amerika inafichua kiburi chake mbele ya ulimwengu. Onyo la Donald Trump kwamba “mambo mabaya yatatokea” isipokuwa Afghanistan ikabidhi Kambi ya Anga ya Bagram inaakisi sauti ile ile ya kibeberu ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifafanua sera ya Marekani kwa ardhi za Waislamu. Maneno kama haya sio lugha ya dola huru zinazoamiliana kwa usawa, bali ni maagizo ya mkoloni ambaye anaziona ardhi za Waislamu kama kituo cha kijeshi kwa ajili ya matamanio yake. Hii ndiyo hali halisi ya siasa za Magharibi: ushurutishaji, vitisho, na kudharau ubwana wa nchi zetu.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu