Jumamosi, 15 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Ufuatiliaji Mkubwa wa Mkoloni Amerika juu ya kile kinachoitwa “Mageuzi” sio Chengine ila ni Jaribio la kupanua Udhibiti wake nchini Bangladesh

Balozi Mdogo wa Marekani jijini Dhaka, Tracy Ann Jacobson, alifanya mkutano na Profesa Ali Riaz, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Maridhiano wiki iliyopita ili kuuliza kuhusu mipango ya mageuzi inayoendelea na maendeleo yake. Jacobson na manaibu wake wamekuwa wakifanya mfululizo wa mikutano na wawakilishi wa vyama vikuu vya kisiasa. Kama sehemu ya ushirikiano wa Marekani ‘kukuza demokrasia’ nchini Bangladesh, tunaona mikutano na taarifa za mara kwa mara kutoka kwa Ubalozi wa Marekani nchini Bangladesh na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani zinazohimiza marekebisho katika utawala. Kusiwe na shaka kwamba msukumo wa Marekani wa kuleta mageuzi na kile kinachoitwa ‘uwajibikaji wa kidemokrasia’ haukusudiwi kheri ya watu wetu. Katika historia, mbeberu mamboleo Marekani imekuwa ikiunga mkono madikteta kwa maslahi yake huku ikitetea ‘demokrasia’ na ‘haki za binadamu’.

Mbele ya Serikali za Khiyana, Msikiti wa Al-Aqsa Unabadilishwa Kuwa Mahali Patakatifu kwa Mayahudi!!

Mbele ya macho ya watawala wa Waislamu, Mayahudi wamekuwa wakivamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa, uvamizi baada ya uvamizi, ambao wa hivi karibuni ulikuwa wa jana, Jumapili, ukiongozwa na adui wa Mwenyezi Mungu, Ben-Gvir na idadi kadhaa ya Mayahudi wenye itikadi kali, katika uvamizi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika msikiti huo.

Ni Wakati sasa wa Kugeuza Ukurasa wa Giza wa Oslo

Smotrich alitangaza kuangamia kwa mradi wa Dola ya Palestina kwa kuzinduliwa kwa mradi wa E1 au East One, ambao unachukuliwa kuwa utekelezaji wa kinachojulikana kama Mpango wa Jerusalem Kuu. Mpango huu unatenganisha Ukingo wa Magharibi wa Kaskazini kutoka Ukingo wa Magharibi wa Kusini, na, sambamba na hatua zilizochukuliwa na umbile la Kiyahudi uwanjani, unaunda viunga vilivyotengwa ndani yake ambavyo vinawazingira watu wa Ukingo wa Magharibi. Hili lilitanguliwa na kubomolewa kwa kambi kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi na kuorodheshwa kwa UNRWA kama shirika lisilo halali, ili suala la wakimbizi libaki kuwa lisilo na umuhimu wowote.

Amerika inaharakisha Mpango wake wa Kulitenganisha Eneo la Darfur Hakuna Suluhisho Isipokuwa kwa Kuufanya Umoja wa Dola kuwa Suala Nyeti

Tangu utawala wa Trump kuchukua faili ya Sudan baada ya kuchukua uongozi mnamo Januari 2025, imekuwa ikiongoza harakati za kijeshi na kisiasa nchini Sudan, ikishinikiza kujitenga kwa eneo la Darfur. Mnamo Jumatano, 26/3/2025, jeshi liliteka tena Khartoum. Al-Burhan alitangaza kutoka Kasri la Republican, “Khartoum iko huru na suala limekwisha.” Hatua za kijeshi ziliharakisha, na kuondoa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kutoka Sudan ya kati, ikijumuisha majimbo ya Al-Jazirah, Sennar, White Nile na Blue Nile.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu