Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 560
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 560
Vichwa Vikuu vya Toleo 560
Kauli za Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu, ambazo alizungumza moja kwa moja kuhusu kile kiitwacho “Israel Kubwa zaidi” na kuhusu mipango ya uhamishaji na upanuzi, zinafichua kwa mara nyengine tena itikadi iliyokita mizizi ndani ya nyoyo za viongozi wa umbile hili; itikadi ya khiyana, usaliti, na ulafi wa ardhi ya Waislamu. Matamshi haya si kuteleza kwa ulimi, bali ni tafsiri ya kivitendo ya mipango iliyoandikwa katika fikra ya kisiasa ya Kizayuni, na mipango inayotekelezwa uwanjani hatua kwa hatua.
Palestina ni ardhi ya Kiislamu; Umar al-Faruq (ra) aliifungua, Salahudin Al-Ayubi akaikomboa, na Khalifa Abdul Hamiid II akailinda. Haiuzwi, na haikubali kugawanyika baina ya watu wake, na aliyeikalia kimabavu, akiwatoa watu wake humo. Suluhisho lake sio dola mbili. Badala yake, utatuzi wake ni kama alivyosema Mwenyezi Mungu Al-Aziz, Al-Jabbar, na kauli yake (swt) ndiyo suluhisho la kweli, “Na wauweni katika vita popote mtakapowakuta, na watoeni popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah: 191].
Jioni ya Jumapili, 10 Agosti 2025, hema dogo la vyombo vya habari mbele ya Hospitali ya Al-Shifa Medical Complex katika Mji wa Gaza liliharibiwa kabisa na shambulizi la moja kwa moja kutoka kwa umbile la Kizayuni, na kuua waandishi wa habari watano waliokuwa wakinakili mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza. Miongoni mwa waliouawa shahidi walikuwa wanahabari Anas Al-Sharif, Mohammad Qreiqeh, na wapiga picha Ibrahim Zaher, Moamen Aliwa, na Mohammad Noufal. Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie miongoni mwa Mitume, wakweli, mashahidi na watu wema – ni maswahaba wema walioje.