Hatimaye, Viziba Uso Vimeanguka kutoka Nyusoni mwa Vibaraka wa Marekani, Erdogan, Rouhani na Putin. Wameshughulishwa na uwakala wa kuhakikisha wanamhifadhi kibaraka wa Marekani ndani ya Syria, ili Marekani imakinike kutatua Janga la Korea na China
- Imepeperushwa katika Hizb ut-Tahrir
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku ya Jumatano 04/04/2018, maraisi wa Urusi, Iran na Uturuki walikutana mjini Ankara, na kutoa kauli yao ya mwisho. Ilikuwa wazi kutokana na kauli hiyo, ima kupitia kauli ya maandishi au kwa yaliyofichika…kwamba wao watatu wameamua kuhakikisha wanaudhibitisha utawala wa kibaraka wa Marekani ndani ya Syria, na kusitisha muamko wa watu wa Syria wa kutaka kusimamisha utawala wa Kiislamu.