Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Khilafah Pekee Ndiyo Itakayoiokoa Karachi kutokana na Kupuuzwa Vibaya na Mfumo wa Kifederali wa Kidemokrasia

Kutokana na hasara kubwa ya mali na kulemazwa kwa usambazaji wa umeme, sehemu kubwa ya Karachi ilisalia imezama ndani ya mchanganyiko wa maji ya mvua na maji taka, siku kadhaa baada ya mvua kubwa katika msimu wa kila mwaka wa mvua ya masika. Hilo, kwa siku kadhaa, miongo mingi ya kupuuzwa kwa kitovu cha kiuchumi cha Pakistan na jiji lake kubwa zaidi, nyumbani kwa zaidi ya watu milioni ishirini, ililipuka na kuwa janga la kitaifa.

Kukabiliana na hasira kubwa za umma kwa kushindwa kushughulikia mateso ya Karachi licha ya kuwemo ndani ya serikali kwa miaka miwili, uongozi uliofedheheka wa Pakistan wa kisiasa na kijeshi kwa haraka ulitangaza Mpango wa Mageuzi wa Karachi. Lakini, siku moja tu baada ya tangazo hilo kubwa la mpango huo, mzozo mkali baina ya ngazi ya mkoa na jimbo ya serikali ulizuka juu ya ufadhili wa mpango huo, mnamo 6 Septemba 2020. Mpango huu tayari unafeli kwa sababu umeshindwa kukabiliana na sababu msingi ya migawanyiko mikubwa ya muda mrefu ya Karachi, Demokrasia.

Kupitia majimbo, Demokrasia inaugawa utawala wa Karachi kutoka juu kwenda chini katika ngazi tatu, katika ngazi ya mji, mkoa na jimbo, huku kukiwa na uchaguzi tofauti kwa kila ngazi. Ugavi wa mamlaka katika ngazi za serikali hupelekea kupuuzwa kwa mambo ya watu, kwani maafisa wa jimbo, mkoa na mji hukataa majukumu, wakitaja sababu za maswala ya kimamlaka. Hata sasa wakati Karachi ikiendelea kurudia hali yake ya kawaida, maafisa wa MQM katika mji, PPP katika mkoa na PTI katika serikali ya jimbo wameshughulika na kulaumiana wao kwa wao.

Kupitia utenganishaji wa mamlaka, Demokrasia hugawanya utawala kutoka kulia kwenda kushoto miongoni mwa wizara, kama vile wizara tofauti za maji, umeme na usalama wa chakula, na miongoni mwa asasi za dola, kwa matawi tofauti ya utekelezaji, bunge na mahakama. Badala ya kuunda serikali yenye kuhesabiwa, ugavi huu wa mamlaka hupelekea kupuuzwa kwa mambo ya watu, kwani wizara na asasi kwa mara nyengine tena hutupiana lawama na kukataa majukumu.

Kupitia upanuzi wake wa uwakilishi wa kisiasa katika utunzi wa sheria, Demokrasia imewagawanya raia wa jiji kuu, lenye makabila mengi la Karachi miongoni mwa makundi kadhaa ya kisiasa, kila moja likidai kuwakilisha ima Sindhi, Mohajir, Pathan, Punjabi au Baluch. Kutokana na Demokrasia, siasa za Karachi na utunzi wa sheria ni ushindani mkali baina ya makundi hasimu ya kisiasa, huku wakati wa uchaguzi ukiwa ni kama tangazo la vita, pamoja na ghasia na mauaji.

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Kwa miongo saba, Demokrasia imefeli jijini Karachi kwa kuwa ni nidhamu mbovu, iliyoundwa na wanadamu ambayo kamwe haiwezi kuleta umoja katika jamii na dola. Demokrasia imefeli kwa miuondo yake yote, ima iwe ni muundo wa kiraia wa bunge, muundo wa kijeshi wa kiraisi au muundo wake mseto wa sasa. Hata mbebaji wa kiulimwengu wa bendera ya Demokrasia, Amerika, imegawanyika pakubwa kutokana na Demokrasia, huku kukishuhudiwa mizozo kati ya makundi ya watu wenye rangi tofauti tofauti, ngazi za serikali na asasi, katika mwaka wa uchaguzi wa uraisi.

Ni Khilafah pekee ndiyo itakayomaliza mgawanyiko mbaya kupitia kutabikisha Uislamu. Katika Uislamu, watawala kuvua hukmu kutokana na nususi zilizoteremshwa, kinyume na Demokrasia ambapo makundi ya kisiasa hutunga sheria kwa mujibu wa maslahi yao. Katika Uislamu, watawala wanawajibika kujifunga na Uislamu kama sheria. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ)

“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” [Surah an-Nisa'a 4:59]. Mahakama ya Madhalim inaweza kumuondoa mtawala yeyote, akiwemo Khalifah, kwa kudumu na ukiukaji waziwazi wa Uislamu. Endapo mtawala atakataa kuondolewa, ni juu ya watu wenye nguvu kumuondoa kwa nguvu. Zaidi ya hayo, vyama vya kisiasa katika Baraza la Ummah lililo katikati na Baraza la Wilayah katika mikoa huwashauri watawala kwa mujibu wa Uislamu. Hivyo, majeshi, mahakama, makongamano na watawala yote huunganishwa kwa lengo moja, kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) pekee.

Katika Uislamu, Khalifah mwenyewe ndiye mwenye mamlaka ya utawala ambaye anawajibika moja kwa moja kwa vitendo vya watawala wote ndani ya dola, ima gavana (Wali) katika mkoa au Aamil katika mji. Khalifah pekee ndiye mwenye uwezo wa kimamlaka wa kumbadilisha moja kwa moja Wali au Aamil kwa wengine walio na uwezo, endapo kutakuwa na malalamiko ya watu wa mkoa au mji huo. Hii ni kwa sababu ingawa Mwenyezi Mungu (swt) ameuweka ubwana wa utunzi wa sheria kwa Sheria Yake (swt) pekee, Yeye (swt) ameupatia Ummah mamlaka ya kuhukumu kwa Uislamu. Kupitia ahadi ya utiifu (Bay'ah), mamlaka haya huhamishwa kutoka kwa Ummah hadi kwa Khalifah, kupitia ridhaa na chaguo lao, huku Khalifah akiwajibika kikamilifu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Akhera na juu ya Ummah hapa Duniani. 

Kuhusiana na uraia, Ummah wa Kiislamu hujiangalia kama ndugu moja, wasiotengana, waliofungamanishwa na Itikadi ya Uislamu pekee. Haugawanyiki kwa misingi ya kikabila, lugha au maeneo na kamwe hakuna chama cha kisiasa kinachoweza kuasisiwa juu ya migawanyiko kama hii ya kijinga. Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

«مَنْ قُتِلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ يَدْعُو عَصَبِيَّةً أَوْ يَنْصُرُ عَصَبِيَّةً فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ»

“Mwenye kuuwawa chini ya bendera ya mtu mwenye upofu (wa njia yake ya haki), anayelingania asabiyya au kunusuru asabiyya, kifo chake ni kifo cha kijahiliya (ujinga).” [Muslim].

Ama idara, Khalifah huhakikisha kuwa inagatuliwa ili kuhakikisha kasi ya utekelezaji, huku akitenga fedha na rasilimali kwa mujibu wa mahitaji ya kila mkoa na mji, badala ya ukubwa wa idadi ya watu wake au uakilishi katika mabaraza. Hivyo, majibu kwa hali yoyote ya dharura ni ya haraka na ya ufanisi, kama ilivyoonekana wakati wa baa la njaa mjini Madina, chini ya Khalifa Muongofu, Umar al-Faruq (ra).

Enyi Waislamu wa Pakistan!

Je, mji uliogawanyika, wenye matatizo wa Karachi hautukumbushi mji wa Yathrib, kabla ya kugeuzwa na Uislamu kuwa Al-Madina Al-Munawwara? Hali ya Ummah wa Kiislamu haitasahihishwa katika ngazi yoyote, mji au Ummah kwa jumla, hadi turudi kwa kile kilichosahihisha mwanzoni, kuhukumu kwa Uislamu. Khilafah iliimarisha miji mitukufu ambayo ilikuwa nyota za ulimwengu kwa karne kumi na tatu za uwepo wake, ikiwemo Madina, Damascus, Baghdad, Cairo na Istanbul na itafanya hivyo tena wakati itakaporudi inshaAllah. Hivyo basi natuimarisheni kujitolea kwetu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na tufanye bidii kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, bila ya kumcha yeyote isipokuwa Yeye (swt) na kumtegemea Yeye (swt) pekee kwa ajili ya mafanikio. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ الأَشْهَادُ)

“Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa duniani na siku watapo simama Mashahidi.” [Ghafir: 51].

H. 21 Muharram 1442
M. : Jumatano, 09 Septemba 2020

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu