Jumanne, 01 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Watawala wa Pakistan Wametoa Kiapo cha Utiifu kwa Mfumo wa Kimataifa unaoongozwa na Marekani, Kuyafanya Watumwa Majeshi Yetu, Kuuweka Uchumi Wetu Rehani kwa Taasisi za Kimataifa na Kuufanya Mfumo Wetu wa Utawala na wa Kisiasa Mtiifu kwa Magharibi

(Imetafsiriwa)

Huku sokomoko ya uchaguzi ikiendelea nchini Pakistan, Waislamu wa Pakistan wanaungua kwa hasira na mfadhaiko kutokana na mauaji ya ndugu na dada zao wa Kipalestina huko Gaza, mikononi mwa umbile halifu la Kiyahudi. Wamewakasirikia watawala wa Pakistan kwa kutelekeza masuala muhimu ya Ummah. Waislamu wa Pakistan ni kama Hadith ya Mtume Muhammad (saw) ilivyowaeleza kuwa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

“Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwa na kuoneana upole kwao ni kama mwili mmoja. Pindi kiungo kimoja kinapoumia, mwili wote huitikia kwa kukosa usingizi na homa.” [Al-Bukhari na Muslim]. Waislamu wa Pakistan wamewataka watawala wao na majeshi kutaharaki kwa ajili ya Jihad kuwanusuru Waislamu wa Gaza, kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, na Ardhi yote iliyobarikiwa ya Palestina kutokana na uvamizi wa Kiyahudi. Lakini, watawala wa Pakistan wamekataa kwa ukaidi kuhamasisha jeshi shujaa la Pakistan kwa ajili ya Jihad, dhidi ya umbile la Kiyahudi. Badala yake wanaitaka jumuiya ya kimataifa inayoongozwa na Marekani na Umoja wa Mataifa kutatua suala la Palestina.

Watawala wa Pakistan wameunga mkono waziwazi "suluhisho la dola mbili" la Marekani kwa Palestina, ambalo linasalimisha sehemu kubwa ya Palestina kwa umbile la Mayahudi, na kuiacha dola ndogo dhaifu, isiyo na nguvu za kijeshi na tegemezi ya Waislamu. Watawala wa Pakistan wanategemea mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kutatua matatizo ya Ummah, ingawa ni mfumo huu wa kimataifa, ndio ambao umeunga mkono kikamilifu vita vya umbile la Kiyahudi dhidi ya Gaza. Marekani imepiga kura ya turufu maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani umbile la Kiyahudi, na kutaka kusitishwa kwa vita. Bunge la Wawakilishi la Marekani limepitisha mpango wa chama cha Republican kutoa msaada wa kijeshi wa $14.5 bilioni kwa ajili ya umbile la Kiyahudi. Marekani imelipa umbile la Kiyahudi msaada zaidi wa kijeshi kuliko nchi nyingine yoyote tangu Vita vya Pili vya Dunia, ikitoa msaada wenye thamani ya zaidi ya $124 bilioni. Zaidi ya hayo, Marekani inatoa silaha kwa umbile la Kiyahudi ili kuangusha mabomu juu ya vichwa vya Waislamu wa Palestina. Imepata daraja la anga kwa ajili ya vifaa vya vita kutoka Jordan, pamoja na daraja la ardhini kutoka Imarati. Meli za kivita za Jeshi la Wanamaji la Marekani na ndege za kivita zinashika doria kwenye Bahari Nyekundu ili kulinda maslahi ya Marekani.

Hivyo basi, vipi mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kutarajia kutoka kwa mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani kwamba utalinda maslahi ya Ummah, wakati ni mfumo huu huu ndio ambao unafanya kazi kikamilifu dhidi ya maslahi yetu? Utiifu wa watawala wa Pakistan kwa mfumo wa kimataifa umelifunga minyororo jeshi letu, kuvifungia vikosi vyetu vya jeshi kwenye kambi zao, huku ndege za kivita, manuari na vifaru vya maadui wetu vikizunguka-zunguka katika ardhi na bahari zetu, kwa uungwaji mkono kamili na wa kivitendo wa mfumo wa kimataifa. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu,

[أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ ءَامَنُوا۟ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓا۟ إِلَى ٱلطَّـٰغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوٓا۟ أَن يَكْفُرُوا۟ بِهِۦ وَيُرِيدُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَـٰلًۢا بَعِيدًۭا]

“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [Surah An-Nisa 4:60].

Ni Khilafah pekee kwa Njia ya Utume, ndiyo ambayo itaunganisha Ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola moja, na kuanzisha mfumo mpya wa kilimwengu kwa msingi wa Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume. Khilafah itayafungua minyororo majeshi yetu na kuyahamasisha katika Jihad dhidi ya maadui zetu ili kuwalinda watu wetu wanaodhulumiwa, na kuzikomboa ardhi zetu tukufu zinazokaliwa kimabavu.

Mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani umeuweka uchumi wa Pakistan katika utumwa, kupitia Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia. Umeipa Marekani udhibiti kamili juu ya maamuzi ya kiuchumi ya Pakistan, ambayo Marekani imetumia kama njia ya kudhibiti sera ya kigeni ya Pakistan. Tishio la kushindwa kwa uchumi na shinikizo la Jopo Kazi la Kifedha (FATF) zilitumiwa na Marekani ili kulazimisha uongozi wa kijeshi wa Pakistan kusambaratisha mashirika ya Jihad yanayopigana na Dola ya Kibaniani huko Kashmir inayokaliwa kimabavu. Hili liliiwezesha Dola ya Kibaniani kukandamiza upinzani wa Kashmir na kuiunganisha Kashmir kwa nguvu mnamo tarehe 5 Agosti 2019. Kupitia mipango ishirini na tatu ya IMF, na mipango kadhaa ya Benki ya Dunia, Marekani imeamuru ajenda huria ya kiuchumi mamboleo. Ilitekelezwa kwa uaminifu na kipote cha tawala wa Pakistan waliogeuza fikra za Kimagharibi. Imeunganisha uchumi wa Pakistan katika miundombinu ya kimataifa ya kifedha na kiuchumi inayotawaliwa na Magharibi, kuhakikisha utiifu wake.

Katika miongo miwili iliyopita, IMF na Benki ya Dunia ziliamuru sera za marekebisho ya uchumi wa Pakistan kutegemea pakubwa maduhuli na mtaji wa kigeni, na kuongeza maduhuli kutoka dolari bilioni 10 mwaka 2000 hadi dolari bilioni 82 mwaka 2022. Uagizaji huu ulifadhiliwa na mikopo ya kimataifa kutoka taasisi za kimataifa za Kimagharibi, masoko ya fedha yanayotawaliwa na nchi za Magharibi, nchi wanachama wa Klabu ya Paris na China. Kufikia 30 Juni 2023, deni la nje la Pakistan lilipanda hadi zaidi ya dolari bilioni 124. Kupitia mfumo wa kimataifa, Marekani inadhibiti ufikiaji wa Pakistan wa masoko ya nje, masoko ya fedha ya kimataifa, mikopo ya nje na mtiririko wa utumaji. Inatafuta kutumia uwezo huu kudhibiti sera ya Pakistan kwa Afghanistan, ikichochea uhasama kati ya Pakistan na Afghanistan, huku ikihimiza usawazishaji mahusiano kati ya Pakistan na Dola ya Kibaniani. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu,

[وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَـٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا]

“Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisaa 4:141].

Ni Khilafah pekee kwa Njia ya Utume, ndiyo ambayo itaunganisha Ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola moja, na kuanzisha mfumo mpya wa kilimwengu kwa msingi wa Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume. Khilafah itaunganisha mali nyingi zinazomilikiwa na ardhi za Waislamu na kuziweka katika matumizi ya Khalifa, ambaye atazitumia kumaliza umasikini, na kuleta ustawi kwa Umma wa Kiislamu.

Mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani umeuweka mfumo wa kisiasa wa Pakistan kuwa mtumwa wa Magharibi. Marekani na mfumo wake wa kimataifa umeunga mkono mara kwa mara utekelezaji wa Demokrasia kama mfumo wa utawala nchini Pakistan. Demokrasia inaweka ubwana kwa sheria iliyotungwa na mwanadamu na inakataa ubwana kwa sheria ya Shariah. Ni kupitia Demokrasia ambapo Marekani na Magharibi ziliweza kufanya sheria kupitishwa kupitia bunge la Pakistan, ambazo zimelazimisha maisha ya kiliberali ya Kimagharibi kwa Waislamu wa Pakistan. Ni bunge hilo ndilo lililopitisha Sheria ya Wanaobadili jinsia, Mswada wa Uhuru wa Maamuzi wa Benki Kuu, kuidhinisha mfumo wa kifedha wa Riba, utabikishaji wa sheria za kisekula za Kiingereza katika mahakama za Pakistan na sheria ya kupambana na ugaidi.

Inaasisi mamlaka ya hadhara ya Kimagharibi juu ya jamii yetu. Demokrasia pia inaruhusu viongozi wa kisiasa na kijeshi wanaotawala kutunga sheria ili kupata maslahi yao, iwe ni sheria zinazohusiana na kuongeza muda wa utumishi wa Mkuu wa Majeshi, Marekebisho ya Kumi na Nane ya kusambaza rasilimali kati ya mikoa inayodhibitiwa na vyama tofauti, kigezo cha sifa ya kuwa Waziri Mkuu au nguvu na mamlaka ya Mahakama ya Upeo ya kuwahisabu watawala. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu:

[وَأَنِ ٱحْكُم بَيْنَهُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَهُمْ وَٱحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَنۢ بَعْضِ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ إِلَيْكَ]

“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyo kuteremshia Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Maida 5:49].

Ni Khilafah pekee kwa Njia ya Utume, ndiyo ambayo itaunganisha Ulimwengu wa Kiislamu kuwa dola moja, na kuanzisha mfumo mpya wa kilimwengu kwa msingi ya Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume. Khilafah itatabikisha hukmu za Shariah zinazohusiana na utawala, jamii, mahakama na mfumo wa kiuchumi pamoja na elimu na sera za kigeni zinazoanzisha jamii ya Kiislamu, kuhuisha Umma wa Kiislamu na kuregesha utawala wa kimataifa wa hadhara ya Kiislamu.

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Uongozi wenu wa kisiasa na kijeshi umeahidi utiifu kwa mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Marekani. Watawala wa Pakistan hawawezi kufikiria kutawala Pakistan isipokuwa jinsi Marekani na mfumo wa kimataifa unavyowaruhusu. Majenerali na wanasiasa wa Pakistan wanaiogopa Marekani. Wanawasilisha uwezo na nguvu za Marekani kama kisingizio cha kutoipinga Marekani na mfumo wake wa kimataifa unaokandamiza. Isipokuwa njia hii ya uchukuaji hatua ibadilike, na uongozi mpya uingie madarakani ambao moja kwa moja na kwa uwazi unapinga mfumo wa kilimwengu unaoongozwa na Marekani, hali yetu haitabadilika. Majeshi yetu yataendelea kufungwa pingu, huku wanawake, watoto na wazee wetu wakiuawa kwa kuchinjwa na Makafiri.

Utajiri wa ardhi zetu utaendelea kumiminika katika nchi za Magharibi. Ardhi zetu zitaendelea kuhukumiwa na kutawaliwa na sheria za ukafiri na hadhara ya Kikafiri ya Kimagharibi. Hakuna njia nyingine ya kuleta mabadiliko, ila kupitia nyinyi. Ni lazima mutumie uwezo wenu na nguvu yenu kuwaondoa watawala hawa na kuipa Nusrah yenu Hizb ut Tahrir, chini ya Amiri wake, faqih mkubwa na mtawala, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah. Ni Khalifa ndiye ambaye atatayarisha njia huru kwa akili ya Ulimwengu wa Kiislamu, isiyo na uingiliwaji na ushawishi wa Kimagharibi. Hivyo basi, Hizb ut Tahrir itaweka msingi wa mfumo mpya wa dunia unaoegemezwa kwenye utabikishaji wa Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume, ili kupata umoja wa ardhi za Waislamu kama dola moja.

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Msiogope utawala wa Marekani. Inatenganishwa na bahari, ni dhaifu na inategemea ushirikiano wa uongozi wenu, kwa ajili ya kuendelea kwa himaya yake ya kilimwengu. Uongozi wenu haukufyatua risasi hata moja na umetazama kimya kimya Waislamu wakichinjwa na Makafiri, na sasa unakimbilia kuiunga mkono Marekani kwa ajili ya "suluhisho la dola mbili" huko Mashariki ya Kati. Toeni Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Viondoeni viti vya utawala vya uongozi huu wa kisiasa na kijeshi, mukifuata nyayo za Saad bin Muadh (ra) na Maanswari wa Madinah, na muweke msingi wa kuregesha hadhara ya Kiislamu. Pateni heshima kubwa zaidi ya kuifanya Pakistan kuwa nukta ya usaidizi wa kuregea kwa utawala wa Kiislamu, kurudi kwa hukmu kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu na kurudi kwa Umma wa Kiislamu kama kiongozi kwa wanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) yuko pamoja nanyi na atakufanyeni washindi. Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran Tukufu,

[هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surah At-Tawbah 9:33].

#Khilafah_New_World_Order

#خلافت_نیا_عالمی_آرڈر

H. 13 Rajab 1445
M. : Alhamisi, 25 Januari 2024

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu