Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 21 Safar 1447 | Na: Afg. 1447 H / 02 |
M. Ijumaa, 15 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Iwapo Kuanguka kwa ‘Jamhuri’ Hakukupelekea Kusimamishwa kwa Khilafah, Ni lazima Kutumike kama Hatua ya Mpito kuelekea Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)
Kuporomoka kwa serikali ya Jamhuri nchini Afghanistan ni moja ya matukio muhimu zaidi kwa watu wa Afghanistan na Umma mpana wa Kiislamu katika karne ya 21. Serikali hii sio tu kwamba haikuwa na mizizi yoyote katika itikadi ya Kiislamu, bali ilikuwa ni zao la muundo wa ukoloni mamboleo - mfumo ulioagizwa kutoka nje uliojengwa ili kurasimisha ufisadi, utegemezi, na dhulma. Kuanguka kwake lilikuwa ni mwisho wa kimaumbile na usioepukika wa mfumo ambao, tangu kuanzishwa kwake, ulikuwa ngeni kwa kitambulisho cha Kiislamu na kupingana na maadili ya Uislamu.
Jamhuri, kama ilivyo lazimishwa nchini Afghanistan, ilikuwa ni muundno uliofeli na usio halali - utawala wa kitaghut kimaumbile - usio na uhalali wa Kiislamu, na hatimaye ilianguka chini ya shinikizo la upinzani wa Waislamu, ikhlasi ya Mujahidina, na tahadhari ya wabebaji Dawah. Tunawapongeza Waislamu wa Afghanistan, Mujahidina wakweli, wahubiri wa ukweli, na Umma wa Kiislamu kwa jumla kwa mabadiliko haya muhimu na yenye baraka. Tunaiona kuwa ni nukta muhimu ya mabadiliko, mwamko, na kuregea kwa ubwana wa Kiislamu.
Hata hivyo, Jamhuri na Demokrasia hazikufungika tu kwa jina au seti ya nembo au viambishi awali ambavyo hutoweka na kuanguka kwa utawala, zinawakilisha mfumo mpana wa kifikra na kisiasa, unaotawaliwa na kanuni mahususi za utawala wa ndani na sera ya kigeni. Kwa hivyo, licha ya mazungumzo ya “kuporomoka kwa jamhuri,” msingi wake wa kifikra, yaani taasisi zake za kisiasa, kanuni za kisheria, sera, na mtazamo wa ulimwengu, bado havijabadilika.
La kusikitisha, watawala wa leo, huku mara kwa mara wakichota kutoka kwa mila za Afghanistan, wanaendelea kutabanni vipengee muhimu vya uhalisia wa kisiasa, vitendo vya kibepari, na utaifa wa kikabila, alama mahususi za kielelezo cha Jamhuri wanayodai kuibadilisha. Mfano wa wazi ni msisitizo unaoendelea wa ‘maslahi ya taifa’ na jitihada za kuwiana na mfumo wa kisekula wa kilimwengu. Kwa hivyo, mabadiliko tu ya uongozi au kuvunjwa kwa chombo cha utawala kisichofanya kazi haipelekei kutokomeza kabisa mfumo wa Jamhuri.
Moja ya matatizo ya kudumu ya Afghanistan imekuwa kuyumba kwa muda mrefu kwa serikali zake. Ingawa uingiliaji wa kigeni umecheza dori, suala la kina zaidi liko katika ukosefu wa uhusiano halisi, wa kimaisha kati ya watawala na watu. Serikali mtawalia zimeshindwa kuanzisha kitambulisho cha pamoja kwa watu au kupata uhalali mkubwa wa umma. Haishangazi, mifumo hiyo kuporomoka, iwe kwa njia ya kutengana kwa ndani au kulazimisha kutoka nje.
Ikiwa serikali ya sasa inatafuta utulivu wa kweli na uhalali wa kudumu, lazima itambue kwamba mamlaka ya kisiasa yanatokana na Umma wa Kiislamu. Ni lazima iainishe masuluhisho ya Kiislamu ndani ya jamii na kujitolea, katika sera ya ndani na nje ya nchi, kwa Uislamu pekee. Katika mtazamo wa ulimwengu wa Kiislamu, nguvu zinatokana na jamii ya Kiislamu, sio kutoka kwa maombi kwa mfumo wa kimataifa au taasisi zake. Uhalali katika Uislamu hautolewi kwa njia ya kutambuliwa kimataifa, bali kupitia Bay’ah, kiapo halali cha utiifu kutoka kwa waumini.
Kwa hiyo, msingi hasa wa utawala katika Uislamu lazima ujengwe juu ya itikadi ya Kiislamu (‘aqeedah), siasa za Kiislamu, na misheni ya Kiislamu. Misheni hii inamkomboa mtawala kutoka katika mipaka ya utaifa, manufaa kiuchumi, na kutoegemea upande wowote, na badala yake inamfunga kwenye wajibu wa kutangaza na kusimamisha ukuu wa Uislamu kupitia Dawah na Jihad.
Hatimaye, ni lazima isisitizwe kwamba watawala wa sasa wa Afghanistan wanapitia Ibtila (mtihani) na majaribu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Baada ya mabadiliko ya kisiasa na kuchukua madaraka, ilikuwa ni wajibu juu yao kuonyesha shukrani kwa Mwenyezi Mungu (swt) si kwa maneno tu, bali kwa utabikishaji kamili, unaojumuisha Uislamu wote. Hii ni pamoja na: Kuendeleza Jihad nje ya mipaka ya nchi bandia; kung'oa maadili, fikra na mifumo yote isiyo ya Kiislamu; na kuweka msingi wa kusimamisha tena Khilafah na kuisimamisha kwa hakika haraka iwezekanavyo.
Iwapo watachagua badala yake kujiweka upya kama washiriki ndani ya mfumo wa kisekula wa kilimwengu; ikiwa wanataka kutambuliwa na dola za kikoloni na taasisi zao; ikiwa roho ya Jihad itafifia miongoni mwao; na ikiwa Uislamu utatekelezwa kwa kuchagua na kivipande, basi onyo la Mwenyezi Mungu (swt) litaanza kutekelezeka hivi karibuni:
[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]
“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Surah Muhammad 47:38].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |