Jumamosi, 14 Muharram 1446 | 2024/07/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Dhu al-Hijjah 1445 Na: H 1445 / 045
M.  Ijumaa, 05 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

 Utawala wa Mirziyoyev nchini Uzbekistan Unafuata Nyayo za Karimov Aliyekufa, katika Kuwatesa Mashababu wa Hizb ut Tahrir na Kukabiliana na Uislamu

(Imetafsiriwa)

Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 2024 kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov. Mashababu hao tayari walikuwa washatumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M. Licha ya madai yote yaliyotolewa na Mirziyev miaka iliyopita, ambapo alidai kuwa anapinga mateso na unyanyasaji dhidi ya wafungwa, na kwamba yuko kwenye njia ya kuimarisha uhuru wa fikra na itikadi na kupambana na ukamataji kiholela. Walakini, tabia ya hivi karibuni ya serikali ya Uzbekistan chini ya uongozi wake inaonyesha kwamba inafuata nyayo za Karimov aliyekufa katika kuwa na uadui na Uislamu na wale wote wanaoulingania. Serikali inawatesa mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa kutumia mbinu za kidhalimu na za kikatili ambazo mtangulizi wake wa uhalifu Karimov ilizitumika hapo awali.

Mashababu walikamatwa kiholela na kwa njia za kinyama na za kikatili. Waliteswa vikali. Walilazimishwa kuungama tuhuma walizobambikiziwa, ambapo waliwaweka mifuko kwenye vichwa vyao na kuweka shinikizo kali juu yao. Na walilazimishwa kutia saini maungamo hayo yaliyotayarishwa mapema chini ya tishio la kuletwa mke wa mmoja wao afisini na kumbaka. Na tishio jengine lilikuwa kumleta mtoto wa shababu mwengine anayesoma nje ya nchi, hadi Uzbekistan kupitia ubalozi, na kumleta mtoto wa shababu mwengine katika Afisi ya Mambo ya Ndani ili kumlazimisha kusaini hati ya kukiri. kulikuwa na tishio jengine la kumtesa shababu mwengine kwa shoti ya umeme.  Pia mashababu wengine 16  walikamatwa katika majimbo ya Tashkent, Andijan, Hawqan, Karshi na Samarkand. Waliletwa Tashkent na kuchunguzwa, kwa tuhuma zinazohusiana na kufanya vurugu na ugaidi!

Tuhuma za ugaidi na kutekeleza unyanyasaji dhidi ya mashahabu wa Hizb ut Tahrir ni wazi kuwa ni uzushi na uongo. Hizb ut Tahrir na mashababu wake hawafanyi fujo wala ugaidi, na wala hizb haijawahi kufanya hivyo tangu kuasisiwa kwake mwaka 1953 M. Haifanyi hivi sio kwa sababu ya kuogopa kwake tawala hizi au kujaribu kuridhiana na tawala dhalimu, bali kwa sababu inamwabudu Mwenyezi Mungu kwa njia yake ili kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, ambayo ni njia ya kifikra na kisiasa ambayo iliifuatwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kwa hiyo, tawala zote za ukandamizaji na za kipolisi katika nchi za Kiislamu na hata katika nchi za Magharibi hazikuweza kuthibitisha shtaka la ugaidi au vurugu dhidi ya Hizb ut Tahrir na mashababu wake, licha ya majaribio yao ya mara kwa mara. Lakini ni chuki inayofurika kutoka katika nyoyo za watawala wahalifu, ambayo inawasukuma kudanganya macho na masikio yao kutokana na kutaka kulipiza kisasi dhidi wabebaji wa mradi unaokuja wa Kiislamu, mradi wa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Watawala wa Waislamu, chini ya uongozi wa mabwana zao, viongozi wa uhalifu na ukoloni nchini Marekani, Uingereza, Urusi, Ufaransa na Ujerumani, wanaupiga vita mradi wa Uislamu na kuzikanyaga sheria na kanuni zao wanazozipigia debe na kuzinadi kwa ulimwengu (uhuru, demokrasia, haki za binadamu) linapokuja suala la ubebaji dawah miongoni mwa mashababu wa Hizb ut Tahrir.

Kuregea kwa Mirziyev katika mkabala wa ukandamizaji, ukamataji, na utesaji katika nyayo za Karimov aliyekufa kunaonyesha kwamba jambo hilo ni utekelezaji wa matamanio na sera za viongozi wa kikoloni nchini Urusi na Marekani, na kwamba watawala wetu, kama kawaida yao, hawamiliki maamuzi yao na si chochote ila wafuasi wa vibaraka wa ukoloni.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunauonya utawala wa Mirziyev dhidi ya kuregea kwenye sera ya ukandamizaji na ukatili ambayo utawala wa Karimov uliitumia dhidi ya Uislamu na wabebaji dawah yake. Hii ndiyo njia ya wahalifu na haitawanufaisha, bali itazidisha hasira za Umma juu yake na kujaalia kuangamia kwake, Umma wa Kiislamu sasa unatazamia siku hiyo utakapokombolewa kutokana na ukoloni na kuregea katika sheria ya Mola wake Mlezi, kama katiba, sheria na maisha, na Umma leo uko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kufikia lengo na matumaini yake. Hivyo basi, Mirziyev lazima awaachilie huru mashababu wetu mara moja na bila kuchelewa, aache kuwatesa wale wanaobeba ujumbe na kuwa na uadui kwa mradi wa Uislamu, na ajifunze kutoka kwa wale waliokuja kabla yake, hakika mwisho mwema ni kwa wachaMungu hata kama mila yote ya ukafiri itakusanyika pamoja, na Mwenyezi Mungu atainusuru dini yake, hata kama ni baada ya muda kidogo, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

﴿كَتَبَ اللهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ﴾

Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.[Mujadala: 21]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД

#PleaFromUzbekistan

#صرخة_من_أوزبيكستان

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hi.zat.one
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hi.zat.one

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu