Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 28 Rajab 1446 | Na: H 1446 / 076 |
M. Jumanne, 28 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Kumbukumbu ya Kila Mwaka ya Kuvunjwa Khilafah na ukingoni mwa kuregea kwake, Tunaulingania Umma wa Kiislamu Uharakishe Kuisimamisha
(Imetafsiriwa)
Tangu Khilafah ilipovunjwa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, Ummah umekuwa ukipitia majanga na kushindwa mfululizo; kuanzia mgawanyiko wa ardhi yake, mpaka kunyang'anywa mali yake, na kuwaua wanawe, na kudhihakiwa matukufu yake na mashambulizi dhidi ya Sharia yake. Hata hivyo, leo Khilafah iko karibu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kurudi, Rayah (bendera) yake iko tayari kupeperushwa kwa mara nyengine tena juu ya ardhi za Waislamu. Kwa hakika, tunaishi katika wakati unaokumbusha usiku ule watu wa Madina walipokuwa wakishauriana, wakikubaliana kwamba wakati umefika wa kumpa Bay'ah bwana wetu Muhammad (saw) kama kiongozi wao wa kisiasa na mkuu wa dola.
Imesimuliwa na Swahaba Jabir ibn Abdullah (ra) katika Hadith iliyopokelewa na Ahmad na Al-Bayhaqi katika As-Sunan. Hadith hii inaelezea hali ya Waislamu mjini Madina katika mkesha wa kufanya uamuzi mkubwa zaidi uliowaweka katika kurasa za dhahabu za historia ya Kiislamu. Akasema: "حتى لم يبق دار من دور الأنصار إلا وفيها رهط من المسلمين، يظهرون الإِسلام، ثم ائتمروا جميعاً... فقلنا: حتى متى نترك رسول الله ﷺ يطرد في جبال مكة ويخاف" “...Mpaka hapakuwa na nyumba hata moja ya Ansari isipokuwa ilikuwa na kundi la Waislamu wanaotekeleza Uislamu waziwazi. Kisha wakashauriana wote pamoja na kusema: ‘Mpaka lini tutamwacha Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akifurushwa hadi kwenye milima ya Makka akiwa anaishi kwa khofu..?’” "وأخذ بيده أسعد بن زرارة وهو أصغرهم فقال: فتبينوا ذلك فهو أعذر لكم عند الله. قالوا: أمط عنا يا أسعد، فوالله لا ندع هذه البيعة أبداً، ولا نسلبها أبداً، فبايعناه فأخذ علينا، وشرط، ويعطينا على ذلك الجنة" Akaendelea kufafanua jinsi gani idadi ya Ansari, Wanaume 73 na wanawake 2, walitoka na kumpa Bay’ah Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwenye Bay’ah ya pili ya Al-Aqabah, Bay’ah ya vita. Pia alitaja wakati uliohusisha mmoja wa Ansari ambao unaakisi kikamilifu wasiwasi ambao Ummah unapitia leo. Akasema: “As’ad bin Zurarah, ambaye ndiye aliyekuwa mdogo miongoni mwao, akamshika mkono wake na kusema: رويداً يا أهل يثرب، فإنا لم نضرب إليه أكباد الإبل إلا ونحن نعلم أنه رسول الله، وأن إخراجه اليوم مفارقة العرب كافة وقتل خياركم، وأن تعضكم السيوف، إما أنتم قوم تصبرون على ذلك وأجركم على الله، وإما أنتم تخافون من أنفسكم خبيئة فتبينوا ذلك فهو أعذر لكم عند الله “Punguzeni kasi enyi watu wa Yathrib, kwani hatukuifanya safari hii na kuwachosha ngamia wetu ila kwa sababu tunajua kwamba yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, lakini kumtoa nje leo kunamaanisha uadui wa wote Waarabu, na kufa kwa walio bora wenu, na kuchomowa panga juu yenu. Na ikiwa mnaogopa kuwa mna udhaifu katika nafsi zenu, basi semeni sasa, kwani hilo ni udhuru zaidi kwenu mbele ya Mwenyezi Mungu.” Wakasema: أمط عنا يا أسعد، فوالله لا ندع هذه البيعة أبداً، ولا نسلبها أبداً، فبايعناه فأخذ علينا، وشرط، ويعطينا على ذلك الجنة 'Kaa kando nasi, ewe As'ad, twaapa kwa Mwenyezi Mungu, sisi hatutaiacha ahadi hii, wala hatutaifuta. Basi tukatoa kiapo cha utiifu kwake, na akachukua ahadi yetu na kwa hilo akatuwekea Pepo kuwa ni yetu.”
Imesimuliwa pia katika Seera ya Ibn Hisham kupitia riwaya nyengine. Ibn Ishaq amesema: وَحَدَّثَنِي عَاصِمُ بْنُ عُمَرَ بْنِ قَتَادَةَ: أَنَّ الْقَوْمَ لَمَّا اجْتَمَعُوا لِبَيْعَةِ رَسُولِ اللهِ ﷺ قَالَ الْعَبَّاسُ بْنُ عُبَادَةَ بْنِ نَضْلَةَ الْأَنْصَارِيُّ، أَخُو بَنِي سَالِمِ بْنِ عَوْفٍ: يَا مَعْشَرَ الْخَزْرَجِ، هَلْ تَدْرُونَ عَلَامَ تُبَايِعُونَ هَذَا الرَّجُلَ؟ قَالُوا: نَعَمْ، قَالَ: إنَّكُمْ تُبَايِعُونَهُ عَلَى حَرْبِ الْأَحْمَرِ وَالْأَسْوَدِ مِنَ النَّاسِ، فَإِنْ كُنْتُمْ تَرَوْنَ أَنَّكُمْ إذَا نُهِكَتْ أَمْوَالُكُمْ مُصِيبَةً، وَأَشْرَافُكُمْ قَتْلاً أَسْلَمْتُمُوهُ، فَمِنْ الْآنَ، فَهُوَ وَاللهِ إنْ فَعَلْتُمْ خِزْيُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَإِنْ كُنْتُمْ تَرَوْنَ أَنَّكُمْ وَافُونَ لَهُ بِمَا دَعَوْتُمُوهُ إلَيْهِ عَلَى نَهْكَةِ الْأَمْوَالِ، وَقَتْلِ الْأَشْرَافِ، فَخُذُوهُ، فَهُوَ وَاللهِ خَيْرُ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، قَالُوا: فَإِنَّا نَأْخُذُهُ عَلَى مُصِيبَةِ الْأَمْوَالِ، وَقَتْلِ الْأَشْرَافِ، فَمَا لَنَا بِذَلِكَ يَا رَسُولَ اللهِ إنْ نَحْنُ وَفَّيْنَا (بِذَلِكَ)؟ قَالَ: الْجَنَّةُ. قَالُوا: اُبْسُطْ يَدَكَ، فَبَسَطَ يَدَهُ فَبَايَعُوهُ. “Aasim bin Umar bin Qatadah amenihadithia kwamba pindi watu walipokusanyika kwa ajili ya kutoa kiapo cha utiifu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ, Al-Abbas bin Ubadah bin Nadlah Al-Ansari, kutoka kabila la Banu Salim bin Awf alisema: “Enyi watu wa Khazraj. Je! Munajua asili ya ahadi yenu kwa mtu huyu?” Wakasema, Ndiyo. Akasema: “Nyinyi mnaahidi kupigana vita dhidi ya watu wekundu na weusi. Ikiwa mnadhani mali yenu itakapopungua na watukufu wenu wakauawa, mtamuacha, basi ni bora kufanya hivyo sasa. Wallahi, mkifanya hivyo ni fedheha duniani na Akhera, lakini mkidhani kuwa mtatekeleza ahadi yenu kwake licha ya kupoteza mali na kuuwawa watukufu wenu, basi mchukueni, kwani Wallahi hiyo ndiyo kheri ya dunia na Akhera.” Wakasema: “Tutamchukua licha ya upotevu wa mali yetu na kuuwawa kwa watukufu wetu. je, malipo yetu ni nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tukifanya hivyo?” Akasema, “Pepo”. Wakasema: “Nyosha mkono wako.” Akaunyosha mkono wake, nao wakampa kiapo cha utiifu kwake.”
Na huu ndio wakati ambao Ummah unapitia leo. Unafikiri na kupiga hesabu, ujitafakari na kupima uwezo wake, kisha kuutazama ulimwengu na kutathmini uwezo wake. Unahisi matumaini na wasiwasi, ukijiuliza: Je, unaweza kutangaza Uislamu kama mradi wa kisiasa? Au lazima uafikiane na Magharibi na vibaraka wake?
Nchi za Magharibi na vibaraka wake zinautishia kwa umaskini, vikwazo, na kifo! Hata hivyo watu wa Ummah huu wanaendelea kupaza sauti zao katika viwanja vya umma, wakitoa wito wa kuregeshwa kwa Uislamu. Wanatamani maisha ya Kiislamu lakini wanasitasita kufanya uamuzi madhubuti.
Hili limekuwa dhahiri huko Ash-Sham baada ya kuanguka kwa utawala wa mhalifu Bashar na kutoroka kwake kutoka Damascus. Tangu dakika ya kwanza kabisa, tuliona Magharibi yote ikiwa na wasiwasi, ikirudia kuwauliza watu wa Ash-Sham: “Je, mtatabikisha Sharia ya Kiislamu? Je, mtasimamisha Khilafah?”
La muhimu zaidi ni kwamba hili halikomei kwa watu wa Ash-Sham peke yao. Ummah mzima wa Kiislamu unawatazama watu wa Ash-Sham, ukifikiri nao na kujadiliana nao jambo hilo. Hili limejaza mawimbi ya majukwaa ya mitandao ya kijamii na mijadala miongoni mwa vijana na mabinti wa Ummah kote ulimwenguni wanapotafuta majibu ya maswali haya muhimu.
Kwa hivyo, je, Ummah – na hatumaanishi watu wa Ash-Sham pekee – wataamua kuunusuru Uislamu na kuusimamisha licha ya “kupungua kwa mali na kuuawa kwa watukufu”? Au utaakhirisha kwa raundi nyengine tena?
Tangu Mapinduzi ya Kiarabu, Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, na kuanguka kwa mashini ya mauaji ambayo iliachiliwa juu ya watu wa Ash-Sham, vikwazo vya kuregea Khilafah vimeendelea kupungua. Miradi ya uzalendo imeanguka kutoka kwa upendeleo wa Ummah, na hawa hapa watu wa Ash-Sham wakikaribisha kurudi kwa Uislamu kwenye mitaala ya elimu licha ya miaka 60 ya utawala wa kisekula. Kwa kila tukio jipya, Ummah unasogea mbali zaidi na fikra za Kimagharibi na kutafuta kurudisha kitambulisho chake kupitia fahamu za Kiislamu.
Zaidi ya hayo, kwa kila tukio kubwa linaloathiri Ummah, wazo la mipaka ya Sykes-Picot linayumba mbele ya fahamu ya kukomesha mipaka, kama ilivyoonyeshwa waziwazi katika vita dhidi ya Gaza, sherehe za kuanguka kwa dhalimu wa Ash-Sham, na sherehe za kuashiria mwisho wa uvamizi huko Gaza.
Vizuizi vilivyosalia vya kuregea Khilafah sasa hivi ni mabaki tu. Wale wanaozielewa jamii wanajua kwamba kinachotutenganisha na kusimamishwa kwake si chochote zaidi ya uamuzi—uamuzi muhimu kama ule uliofanywa na Ansari (ra) walipochagua kuishi kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na kufa katika kutafuta Jannah Yake. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ * لَا شَرِيكَ لهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ]
“Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. (162) Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.” [Al-An’am: 162-3].
Hizb ut Tahrir inaunyoosha mkono wake kwa Ummah na majeshi yake yote kufanya kazi pamoja nasi kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Tumetayarisha kila kinachohitajika kwa ajili yake. Kwa hivyo fanyeni kazi nasi ili kuufanya mwaka huu kuwa mwaka wa mwisho wa kukumbuka kumbukumbu ya kuvunjwa kwake, na mwaka ujao, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, tuanze kusherehekea kurudi kwake kila mwaka.
Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |