Alhamisi, 03 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kuwa "Mzayuni Mkubwa" Kunamaanisha kuwa kama Putin na Kusaidia Uvamizi Kikatili na Haramu

Katikati ya uchumi unaofeli, mfumko wa bei wa tarakimu mbili, viwango vya rehani vinavyoongezeka, bili za juu za kawi, mabadiliko ya kodi, kupanda kwa deni, mgogoro wa pesa za mfuko wa pensheni, vita nchini Ukraine, sarafu inayoshuka thamani, ongezeko la uhamiaji na idadi inayodidimia ya wapiga kura, Waziri Mkuu mpya wa Uingereza (na labda nusu ya baraza lake la mawaziri) alipata wasaa wa kujitokeza kwenye hafla ya kando ya CFI kwenye dhifa ya kongamano lao la chama ambapo alijitangaza kwa fahari kuwa "Mzayuni mkubwa."

Soma zaidi...

Kipindupindu Kinawaua Watu wa Syria, Hivyo Iko Wapi Dola ya Kuwanusuru?!

Wizara ya Afya ya Utawala wa Syria ilitangaza mnamo Jumatatu kuwa mkurupuko wa kipindupindu katika maeneo kadhaa umewauwa watu 29, vifo na majeruhi vilikolea katika jimbo la kaskazini la Aleppo, ambapo watu 25 walithibitishwa kufariki, na maelfu kadhaa ya visa vinavyoshukiwa kuripotiwa kote nchini kuanzia Septemba 19, kulingana na data iliyopatikana na chama cha misaada kutoka Kitengo cha Afya cha Serikali ya Syria (GoS), Idara ya Kibinafsi ya Mamlaka ya Afya ya Mitaa, Kaskazini na Mashariki mwa Syria.

Soma zaidi...

Iraq Mpya ambayo Amerika Iliahidi

Mnamo siku ya Jumatano na Alhamisi, Septemba 28-29, 2022, Iran ilishambulia vikali wilaya za majimbo ya Erbil na Sulaymaniyah kwa makombora ya balistiki na droni zilizonaswa, zikilenga makao makuu ya vyama vya upinzani vya Kikurdi. Mnamo Jumatano, Wakfu wa Kupambana na Ugaidi katika Mkoa wa Kurdistan ulitangaza kwamba "Walinzi wa Mapinduzi ya Iran walifanya shambulizi la kombora katika eneo hilo katika hatua nne, ambalo liliwaacha mashahidi 13 na 58 kujeruhiwa."

Soma zaidi...

Viongozi wa Chama cha Chuo cha Eden Chhatra ni Matunda ya Mti wa Sumu wa Usekula Unaokuzwa na Serikali ya Hasina

Taifa zima limeshtushwa na madai dhidi ya viongozi wakuu wa kike wa Chama cha Chuo Eden Chhatra, mrengo wa wanafunzi wa chama tawala, Awami League. Wanaharakati wa chama chao wamedai mbele ya vyombo vya habari kuwa viongozi wao hurekodi video za uchi za wanaharakati wanawake wa chama hicho, kuwanyanyasa kingono na kuwalazimisha kuwaburudisha viongozi wakuu wa chama hicho.

Soma zaidi...

Lau Tungekuwa na Ngao ya Ulinzi na Imam, Mayahudi Wasingesubutu Kunyakua Ardhi Yetu na Kuifisidi

Mnamo tarehe 9/23/2022, Al Jazeera Kiingereza ilichapisha ripoti kuhusu mateso ya watu wa Masafer Yatta [Palestina] kutokana na mashambulizi ya walowezi. Ripoti hiyo ilinukuu ushahidi wa wanawake wa eneo hilo, waliozungumzia mateso yao na familia zao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na wanajeshi wavamizi na makundi ya walowezi, ambapo wanapigwa, kupigwa risasi za moto, kushambuliwa kwa gesi na kukamatwa.

Soma zaidi...

Sheria ya Mtoto na Kanuni zake za Utendaji ni Utangulizi wa Kusambaratika kwa Familia, na Kisu chenye Sumu Upande wa Watu wa Palestina!

Sawia na jinai zake dhidi ya watu wa Palestina, Mamlaka ya Palestina (PA) imechapisha kanuni za utendaji kwa ajili ya hatua za kulinda na kumpa haki mtoto za mwaka 2022 katika toleo la hivi karibuni la Gazeti la Palestina, Na. 194, sheria ambayo inatoa njia ya kusambaratisha familia na kushambulia mfumo wa kijamii kwa kuharibu malezi ya baba kwa watoto wake na kuwatoa watoto katika familia zao na hukmu za dini yao!

Soma zaidi...

Watoto Wapendwa wa Ash-Sham Wafariki Baada ya Boti za Wakimbizi Kuzama. Je, Tunapoteza Wangapi Zaidi Bila Khilafah?!

BBC iliripoti mnamo tarehe 23 Septemba 2022 kwamba wakimbizi wahamiaji 71 walipatikana katika mashua inayozama nje ya pwani ya Syria. Makumi wameripotiwa kufariki. Watu 20 kati ya walionusurika walipelekwa katika jiji la Tartus kutibiwa hospitalini. Wanawake na watoto wa Lebanon, Syria na Wapalestina walikuwa miongoni mwa watu 120 hadi 150 waliokuwemo ndani.

Soma zaidi...

Rupia Kubanwa kwa Dolari, Inahakikisha Kushuka kwa Thamani Yake. Katika Uislamu, Sarafu Inayoegemezwa juu ya Dhahabu na Fedha Itaokoa Pakistan na Ulimwengu wa Kiislamu kutokana na Utumwa wa Dolari

Serikali ya PDM inakabiliwa na hasira kali ya umma kutokana na mgogoro mkubwa wa sarafu, na dhoruba ya mfumko wa bei. Ili kutuliza umma, serikali imetangaza kuwa Waziri wa Fedha, Miftah Ismail, amebadilishwa kwa Ishaq Dar, ambaye ndiye aliyepewa jukumu la kuimarisha thamani ya Rupia.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu