Alhamisi, 19 Dhu al-Hijjah 1442 | 2021/07/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 H / 03
M.  Jumatano, 07 Julai 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara kwa Ubalozi wa Pakistan Jijini Vienna ili Kutaka Kuachiliwa Huru Mara Moja kwa Mhandisi Naveed Butt!
(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Hizb ut Tahrir kutaka kuachiliwa huru kwa Naveed Butt, msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan, ambaye alitekwa nyara na wakala wa ujasusi wa Pakistan mnamo tarehe 11 Mei 2012 na tangu wakati huo ametoweka na haijulikani alipo, ujumbe wa Hizb ut Tahrir katika Nchi zinazozungumza Kijerumani ulioongozwa na Mhandisi Shaker Assem, mwakilishi kwa vyombo vya habari wa Hizb ut Tahrir katika Nchi zinazozungumza Kijerumani ulitembelea ubalozi wa Pakistan katika jiji la Vienna kufikisha taarifa kutoka kwa Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika suala hili. Mfanyikazi mmoja wa ubalozi huo alipokea taarifa hiyo, akaahidi kuipeleka kwa serikali ya Pakistan na akahakikisha kuwa ubalozi huo utawasiliana na ujumbe huo juu ya suala hilo

Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aifanye kampeni hii izae matunda yake na aulete uachwaji huru wa haraka wa ndugu yetu Naveed Butt, mbebaji mashuhuri wa Ulinganizi wa Kiislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Nchi Zinazungumza Kijerumani

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Nchi Zinazozungumza Kijerumani
Address & Website
Tel: 0043 699 81 61 86 53
Fax: 0043 1 90 74 0 91
E-Mail: shaker.assem@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu