Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  4 Rabi' I 1444 Na: 1444 H / 08
M.  Ijumaa, 30 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Viongozi wa Chama cha Chuo cha Eden Chhatra ni Matunda ya Mti wa Sumu wa Usekula Unaokuzwa na Serikali ya Hasina

(Imetafsiriwa)

Taifa zima limeshtushwa na madai dhidi ya viongozi wakuu wa kike wa Chama cha Chuo Eden Chhatra, mrengo wa wanafunzi wa chama tawala, Awami League. Wanaharakati wa chama chao wamedai mbele ya vyombo vya habari kuwa viongozi wao hurekodi video za uchi za wanaharakati wanawake wa chama hicho, kuwanyanyasa kingono na kuwalazimisha kuwaburudisha viongozi wakuu wa chama hicho. Biashara ya kashfa ya ngono ya viongozi wa Chama cha Chhatra imeharibu sifa ya taasisi hii ya elimu inayotambulika katika mji mkuu na kuwanyanyapaa kwa jumla zaidi ya wanafunzi 35,000 wa kike. Huu tayari ni ukweli uliothibitishwa kwamba Chama cha Sheikh Hasina cha Chhatra sasa ni shirika la wabakaji na wanyanyasaji wa ngono. Lakini wahalifu hawa hawawezi kutazamwa kuwa wako kando na utawala wa kisekula wa Kibepari wa Hasina. Ni matunda yenye sumu ya mti wa Kibepari wa kisekula uliopandwa na kukuzwa na Sheikh Hasina. Kwa miaka mingi, serikali ya Hasina imekuwa ikisukuma mabadiliko ya jumla ya jamii yetu kuelekea kupitisha maadili ya kiliberali ya Magharibi. Serikali ya Hasina imeruhusu kuenea kwa thaqafa haribifu ya Kimagharibi ya ngono huru, uzinzi na uasherati katika tamthilia, sinema, vipindi vya silsila vya mtandao, na medani za kitamaduni ili kuanzisha mtazamo huria kuhusu kujamiiana miongoni mwa vijana wa Kiislamu. Kwa jina la kile kinachoitwa ukombozi, wanawake wanaonyeshwa kama nembo za ngono kwenye vyombo vya habari. Wanageuzwa kama bidhaa na kutumiwa kama kichocheo kuunda mazingira ya unyanyasaji mkubwa wa kijinsia katika mujtamaa mzima. Utawala wa Hasina umekuwa ukifuatilia kidini kuwafisidi watu kwa kuwaingiza mtindo wa maisha ya utumiaji wa kimagharibi. Raha ya kimwili daima huwasilishwa kama kiwango cha juu zaidi cha furaha. Serikali haikuishia tu kwa kutoa leseni za vileo na kamari nchini - wasanii wengi wa Hollywood-Bollywood wakiwemo wasanii wa filamu za ngono mithili ya Sunny Leone wanaruhusiwa kufanya matamasha na maonyesho ya jukwaani nchini moja baada ya jengine wakipuuza ghadhabu kali za Waislamu wachaMungu nchini humu. Vijana 54 wa nchi hii walitumwa kwenye tamasha la dansi ya hip-hop na mapumziko na warsha ya mafunzo iliyoandaliwa na ubalozi wa Marekani jijini Dhaka hivi karibuni ili kuwafahamisha vijana wa Kiislamu utamaduni wa hip hop wa Magharibi. Kando na hilo, kwa lengo la kutangaza utamaduni wa K-pop wa Kikorea miongoni mwa vijana, mashindano na sherehe za K-pop hufanyika mara kwa mara jijini Dhaka. Serikali ya Sheikh Hasina inaingiza Hollywood-Bollywood na thaqafa ya Kikorea kwa upande mmoja huku ikiwa mpiganaji wa mstari wa mbele katika vita dhidi ya Uislamu kwa upande mwingine kwani Waislamu hawaruhusiwi kuwa na mikusanyiko yoyote ya mijadala ya kisiasa na kifikra ya Uislamu kote nchi.

Kulazimisha maadili ya kisekula daima imekuwa ndio ndoto thamani ya Sheikh Hasina na babake Sheikh Mujib! Lakini watu wa nchi hii wamekataa maadili mabovu ya kisekula ya Sheikh Hasina, ingawa wengine wameshawishiwa na falsafa ya kiliberali ya maadili ya kisekula. Vita vyake vya msalaba dhidi ya Uislamu na kuwezesha uvamizi mbaya wa thaqafa wa Kimagharibi kote nchini havijaupotosha Umma wa Kiislamu kutoka kwenye maadili matukufu ya Uislamu. Lakini amefungua mlango wa maangamizi kwa viongozi wa chama chake kwa thaqafa hii iliyooza ya kihuni ya Kimagharibi. Ndio maana visa vya uhalifu wa kijinsia na unyanyasaji wa mawaziri na viongozi wa chama tawala vinafichuliwa moja baada ya chengine. Tuliona jinsi wanyanyasaji wa kingono kama waziri wa zamani Murad walivyopata ulinzi kutoka kwa Hasina na bado kuendelea kubaki Mbunge hata baada ya kutishia kumbaka mwigizaji mmoja wa kike! Viongozi hawa wa Chama cha Chhatra cha Chuo cha Eden wanabeba urithi wa viongozi wengine wa kashfa wa Hasina mithili ya Papia na Helena Jahangir ambao pia walizaliwa katika tumbo moja la mfumo huu wa kiliberali uliolelewa na Hasina.

Enyi Waislamu! Hamupaswi kujitetea kutokana na maadili mabovu ya kiliberali ya Kimagharibi yaliyolazimishwa na serikali ya Hasina ambayo yanaangamiza miundombinu ya maadili ya mujtamaa wetu. Munapaswa kusimama dhidi ya mradi wa serikali isiyo na haya ya Hasina katika kutekeleza uvamizi wa kithaqafa wa Kimagharibi kwa kutokomeza siasa za kisekula pamoja na utawala wake wa kisekula unaoungwa mkono na Magharibi ambao unaingiza uasherati na uzinzi katika nchi hii. Tunatoa wito kwenu kubeba jukumu la kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah inayokaribia itatukuza heshima ya wanawake na kulinda fikra za Kiislamu na hisia za jamii kwa jumla na kuzuia njia zote za kupenyeza thaqafa ya Magharibi. Fanyeni kazi bega kwa bega na kundi la waumini la Hizb ut Tahrir kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida ya pili lililoahidiwa kabla ya mujtamaa wetu na vizazi vijavyo kuharibika mithili ya Magharibi na kuwa kuni za moto wa Jahannam.

Mwenyezi Mungu Subhanahu wataala asema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا۟ قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَاراً وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ)

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe.” [Surah At-Tahreem: 6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu