Jumatatu, 23 Shawwal 1446 | 2025/04/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  19 Ramadan 1446 Na: H 1446 / 33
M.  Jumatano, 19 Machi 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wakati wa Ziara yake nchini India, Tulsi Gabbard katika Taarifa yake Alieleza Kujitolea kwa Ushirikiano wa Marekani na India na Mapambano dhidi ya Uislamu na Waislamu

(Imetafsiriwa)

Ingawa maoni ya chuki yaliyotolewa na Mkuu wa Ujasusi wa Kitaifa wa Kruseda Amerika, Tulsi Gabbard wakati wa ziara yake nchini India juu ya mateso ya watu walio wachache nchini Bangladesh na 'Khilafah ya Kiislamu' hayakuwashtua watu wanaozingatia siasa na wapenda Uislamu wa nchi hii, yaliondoa aibu ya mwisho ya vibaraka wa Amerika nchini Bangladesh. Kwa sababu vibaraka hawa walikuuza kukubalika kusiko epukika kwa Amerika kama rafiki wa Bangladesh ili kukabiliana na India na kuwahakikishia watu wapenda Uislamu wa nchi hii kwamba Amerika ilikuwa imeacha sera ya "vita dhidi ya Uislamu". Ingawa ukweli ni kwamba, hata kama uongozi wa Amerika utabadilika, 'sera yao ya kigeni' haibadilika. Badala yake, Trump shupavu au utawala wake hupenda kuwatusi vibaraka wake na kufichua nia za ‘sera zao za kigeni’. Kwa hili ametaka uwajibikaji wa dolari milioni 29 ambazo zililipwa kwa vibaraka ili kubadilisha mazingira ya kisiasa ya Bangladesh, huku kutumia pesa kama hizo kudhibiti siasa za nchi huru ni uhalifu mkubwa na ni sawa na kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine.

Vibaraka wa Marekani nchini Bangladesh daima wamekuwa wakiwapotosha watu, wakisema kwamba hata kama Marekani itaunga mkono umbile la Kiyahudi lililolaaniwa kufanya mauaji na kuwaondoa Waislamu wa Palestina, itasimama upande wa nchi yetu katika kukabiliana na uvamizi wa India. Ingawa katika hali halisi, kama ambavyo Amerika inapigana vita dhidi ya Uislamu na Waislamu kupitia ugaidi kwa kuunga mkono umbile haramu la Kiyahudi katika eneo la Kiarabu, katika eneo hili Amerika vile vile inaendeleza vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu, kwa kutumia India kama mlinzi wake wa kieneo. Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya kwa uwazi kabisa kuhusu Wakoloni makafiri na vibaraka wao katika suala hili:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ مِنْكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [Al-Maidah: 51]. Kwa sababu Marekani inajua kwamba Waislamu ni adui mkubwa wa umbile haramu la Kiyahudi la ‘Israel’ na dola ya washirikina ya India;

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. [Surah Al-Maidah: 82].

Mumeona kwamba serikali ya mpito, ili kuficha aibu yake, imetuma kile kinachoitwa kulaani kauli ya Tulsi Gabbard, lakini imesisitiza dhamira yao ya kuwakandamiza Waislamu kwa kuyataja matakwa ya utawala wa Kiislamu yanayofanywa na watu wa nchi hii inayotawaliwa na Waislamu kuwa ni 'ugaidi wa Kiislamu'. Vibaraka hawa ni watiifu na wapumbavu kiasi kwamba hawajasubutu kuiuliza Amerika swali hata moja katika kupinga dhidi yao! Kwa nini Tulsi Gabbard hajaonyesha wasiwasi wake kuhusu kwa nini Waislamu walio wachache nchini India wanaendelea kuteswa kwa kuungwa mkono na Dola ya India? Ulimwengu umeshuhudia jinsi Waislamu walio wachache nchini India wanavyoteswa na watu wenye msimamo mkali wa Hindutva wakati ambapo Tulsi yuko India. Hawajasema hata neno moja kwa nini India imempa hifadhi 'fashisti Hasina'? vibaraka wa Marekani hawajauliza maswali haya kwa sababu wanafahamu uhusiano wa Marekani na India katika eneo hilo.

Enyi Watu! Iulizeni dhamiri yenu, licha ya msimamo wa Marekani-India dhidi ya watu wa nchi hiyo, ni kisingizio gani chengine kinachoweza kuwa cha kutoichukulia Marekani kafiri ya kikoloni na kiongozi wake wa kieneo India kama maadui wa Umma wa Kiislamu? Wengi wanahisi hata kurekebishwa kwa dhalimu Hasina katika taarifa ya Tulsi Gabbard. Kwa hiyo, wito wa Hizb ut Tahrir kwa watu wenye ufahamu, wanasiasa wenye ikhlasi na wasomi, na wanajeshi ni kwamba, lazima tuungane kupinga ajenda ya Marekani-India ya kumregesha dhalimu Hasina au kuanzisha kibaraka mwengine yeyote mahali pake na kuzima njama za Marekani-India dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Enyi Watu! Mnajua kwamba Marekani, mtetezi wa mfumo wa kirasilimali wa kisekula, sasa ni ‘mtu mgonjwa’ na mfumo wa kirasilimali wa kisekula unalaaniwa kuwa ni mfumo mbaya na kandamizi duniani kote. Kwa hiyo, Marekani inaogopa kuregea kwa utawala wa adilifu- mfumo wa Khilafah. Katika miaka mia saba ya utawala wa Waislamu katika eneo hili, wakati Waislamu na wasiokuwa Waislamu waliishi kwa amani, 'simulizi' ya athari mbaya ya kuibuka kwa Khilafah ya Kiislamu kwa wasio Waislamu na mkuu wa kijasusi wa Marekani Tulsi ni uongo mkubwa na kielelezo cha kufilisika kwao kisiasa. Kwa hakika, mfumo ujao wa Khilafah pekee ndio utakaokomboa eneo hili kutoka kwa njama za kijiografia za Nchi za Kikoloni za Magharibi na tabaka tawala la Hindutva lililomrithi Mfalme Dahir dhalimu, na kuregesha utulivu wa kikanda, insha’Allah. Kwa hiyo, watu wote lazima waungane na Hizb ut Tahrir na kuendeleza kazi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

[وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا]

Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu. [Surah Al-Baqarah: 143].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu