Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 12 Dhu al-Qi'dah 1446 | Na: H 1446 / 43 |
M. Jumamosi, 10 Mei 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kukabidhi Uendeshaji wa Operesheni za "Bohari la Kontena la New Mooring " kwa Kampuni ya Wakoloni yenye Ushawishi wa Marekani "DP World" kutatishia Ubwana wa Nchi
(Imetafsiriwa)
Bila kujali ubwana wa nchi, serikali ya mpito inaendelea na mchakato wa kukabidhi huduma na mabohari mbalimbali ya Bandari ya Chittagong muhimu kimkakati na kiuchumi kwa wageni kwa jina la kuongeza uwezo wa bandari kwa kisingizio cha uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI). Kama sehemu ya hili, mchakato wa kukabidhi Bohari Kuu la Kontena la New Mooring (NCT) la Bandari ya Chittagong linalojitosheleza na la juu zaidi la kuzalisha mapato kwa kampuni ya DP World uko katika hatua zake za mwisho (Daily Jugantor, Mei 6, 2025). Bandari ya Chittagong ni eneo la kimkakati la Bangladesh linalokabili Ghuba ya Bengal na Bahari ya Hindi. Kwa hivyo, bandari hii sio tu muhimu sana kama njia ya kiuchumi, lakini pia ni mali ya kimkakati kutoka kwa mtazamo wa siasa ya kijiografia na kijeshi. 90% ya biashara ya kimataifa inashughulikiwa kupitia bandari hii na 60% ya mapato yake makuu yanatoka Bohari la Kontena la New Mooring, kwa hivyo ikiwa uamuzi wa kujiua utafanywa kuikabidhi kwa kampuni ya kigeni, sio tu kwamba ubwana wa kiuchumi wa nchi utadhoofika, lakini pia tutakuwa katika hatari ya kukabiliwa na changamoto za siasa za kijiografia, kijeshi na kimkakati. Kama unavyojua, DP World ni kampuni ya kimataifa ya usafirishaji yenye makao yake makuu Dubai, ambayo inajulikana kimataifa kwa kutoa maendeleo ya bandari, huduma za baharini, mifumo ya kisasa ya logistiki, na huduma za biashara zinazotegemea teknolojia, lakini dola za Kikoloni za Makafiri, hasa Marekani na Uingereza, zinaitumia kwa madhumuni ya kijeshi kufikia maslahi yao ya kijiografia. Ni muhimu kuashiria kuwa, Dubai ni moja ya washirika wa kistratejia wa wakoloni wa kimagharibi katika Mashariki ya Kati na mshirika wa umbile haramu la Kiyahudi. Kwa mfano, Dubai ilishiriki katika zoezi la anga la kimataifa "INIOCHOS-25" lililofanyika "Kambi ya Anga ya Andravida" nchini Ugiriki kuanzia Machi 31, 2025 hadi Aprili 11, 2025, pamoja na Marekani, umbile haramu la Kiyahudi, na India [THE ECONOMIC TIMES, 13 Aprili 2025]. Ni wazi kutokana na hili kwamba kundi hilo la wahaini linaendelea na juhudi zake ovu za kuhamisha utendakazi wa "Bohari la Kontena la New Mooring" la Bandari ya Chittagong hadi kwa "DP World" kama mradi wa kumakinisha Ukoloni wa Marekani katika eneo hili. Mwenyezi Mungu (swt) anatuonya kuhusu utawala wa makafiri juu ya Waislamu, akisema:
[إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاء وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ وَوَدُّوا لَوْ تَكْفُرُونَ]
“Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu. Na wanapenda muwe makafiri.” [Surah Al-Mumtahinah: 2].
Enyi Watu, mnafahamu kwamba dikteta aliyeanguka Hasina, ili kudumisha mamlaka yake, alikabidhi bandari ya Matarbari iliyoko kusini mwa Bangladesh kwa Japan, mojawapo ya washirika wa Marekani katika Mkakati wa Indo-Pacifiki, ambayo kimsingi inahusiana na maslahi ya siasa za kijiografia za Marekani katika bandari za bahari kuu za Bangladesh chini ya kivuli cha ushirikiano wa Japan. Kwa kuongezea, serikali ya Hasina pia ilikubali kimsingi kukabidhi vitalu vyote 15 vya hydrocarbon vilivyo kwenye bahari kuu ya Bangladesh kwa kampuni kubwa ya nishati ya Amerika ya ExxonMobil (Daily Jugantar, Aprili 25, 2023), ambayo ExxonMobil inafanya kazi kwa karibu na Bunge la Amerika na Ikulu ya White House. Na serikali ya sasa ya mpito pia imefuata nyayo za serikali iliyoanguka ya Hasina na kuanza mchakato wa kukabidhi NCT kwa DP World kwa jina la uwekezaji wa kigeni katika miradi mbalimbali ya Bandari ya Chittagong muhimu sana kimkakati. DP World inashirikiana na Jeshi la Wanamaji la Marekani katika shughuli zake kama mshirika muhimu katika bandari za nchi mbalimbali duniani. Kwa hiyo, uwepo wa makampuni hayo yenye nguvu yenye ushawishi wa Marekani ndani ya bahari za Bangladeshi na katika mitambo ya kimkakati ina maana ya kuimarisha udhibiti wa Marekani ndani ya nchi, ambayo ni sawa na kuuza ubwana.
Enyi Watu, wafanyikazi wetu wanapotuma angalau dolari bilioni mbili za malipo kila mwezi, ni udanganyifu kueleza msisimko kuhusu uwekezaji wa mabilioni ya dolari wa 'DP World'. Ni muhimu kuimarisha uwezo wetu na usimamizi wetu wa bandari ili kulinda nyenzo za kimkakati kama bandari na maliasili dhidi ya ukaliaji wa kigeni; na hivyo basi, ubwana wa nchi utalindwa na uchumi wa nchi kuimarika. Hata hivyo, wanasiasa watiifu kwa nchi za Magharibi hawana malengo ya kisiasa kwa watu wa nchi hii. Badala yake, badala ya kufikia uwezo wao wenyewe, wana hamu ya kulinda maslahi ya makampuni ya kigeni na mabwana zao wa kikoloni. Ndio maana maamuzi na matendo yao yote yanatokana na kujipatia madaraka yao wenyewe kwa kulinda maslahi ya wakoloni wao. Kwa hivyo, rasilimali za kimkakati za nchi sio salama mikononi mwa matabaka haya tawala ya kisekula na hayatakuruhusuni kufurahia manufaa ya kisawa sawa ya rasilimali za nchi. Sisi, Hizb ut Tahrir, tunapenda kuwakumbusha kwamba ni Khilafah pekee yenye kusimamishwa kwa njia ya Utume ndio inayoweza kusimamia kwa mujibu wa Sharia na kuondoa rasilimali zetu muhimu kama vile mafuta, gesi na bandari kutoka kwa udhibiti wa maadui wa kigeni. Khilafah ijayo itaunganisha Umma wa Kiislamu na kutumia rasilimali zake za kimkakati kuibuka kama dola inayoongoza duniani.
[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَكَفَى بِاللَّهِ شَهِيدًا]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki, ili aitukuze juu ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi.” [Surah Al-Fath: 28].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |