Jumanne, 13 Muharram 1447 | 2025/07/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  7 Muharram 1447 Na: H 1447 / 01
M.  Jumatano, 02 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uhamishaji wa Dola ya Hindutva ya India wa Waislamu hadi Bangladesh kwa Mtutu wa Bunduki ni Uadui wa Wazi kwa Waislamu kama ule wa Umbile Haramu la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Hindutva ya Modi inaendelea kuongeza kiwango cha ukandamizaji na mateso, ikiwa ni pamoja na kubomoa nyumba za Waislamu wa India na kuwapeleka uhamisho kwa nguvu usio wa haki. Kupitia hili kimsingi wanafuata nyayo za dola haramu ya Kiyahudi ‘Israel’. Hivi karibuni, hata wanawatendea Waislamu wa India kama wanyama kwa kuwaita wahamiaji haramu na kuwarudisha mamia yao nchini Bangladesh kwa mtutu wa bunduki, wakipuuza kile kinachoitwa michakato yao ya kisheria ya kitaifa na kimataifa. "Walitutendea kama wanyama," alisema mwanamke mmoja anayeitwa Rahima Khatun. "Tulipinga kwamba sisi ni Wahindi, kwa nini tuingie Bangladesh? Lakini walituelekezea bunduki na kutishia, 'Ikiwa hamtakwenda kwa huko, tutakupigeni risasi.' Baada ya kusikia milio minne ya risasi kutoka upande wa India, tuliogopa sana na haraka tukavuka mpaka kwa miguu". [Ripoti ya FP].

Wengi wamejaribu kuficha ukweli halisi kwa kuuita kuwa ni matokeo ya mahusiano ya sasa ya kiuadui ya India na Bangladesh. Kwa hakika, ni sehemu ya mchakato unaoendelea wa kutokuwa na taifa kwa Waislamu wa India na kufuta kitambulisho cha Waislamu nchini India, kama vile umbile haramu la Kiyahudi 'Israel' linavyoendelea kufanya hukoPalestina. Nchini India, ambayo ni nyumbani kwa Waislamu zaidi ya milioni 200, kuanzia kubomolewa kwa Msikiti wa kihistoria ya Babri hadi ujenzi wa hekalu, hadi kufutwa kwa mila ya miaka elfu ya utawala wa Kiislamu, hadi kufukuliwa kwa kaburi la Aurangzeb, hadi Sheria mpya ya Uraia (CAA) na Sajili ya Kitaifa ya Raia (NRC), mwishowe ni kupitisha Mswada mpya (wa marekebisho) wa Wakfu, India inaondoa kimpangilio kitambulisho cha Waislamu na kuwageuza Waislamu kutokuwa na taifa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Surah Al-Ma’idah: 82].

Swali ni je, kwa nini Dola ya Hindutva ya India inaonyesha ujasiri huu? Kwanza, ijapokuwa Waislamu wa eneo hili wamefungamanishwa na imani na damu moja, Mkoloni kafiri Uingereza imewagawanya na kuwadhoofisha Waislamu kwa msingi wa utaifa (Wahindi, Wabangladeshi, Wapakistani nk.), na imetulazimishia watawala wao wakala wa kisekula juu yetu ambao kamwe hawajitokezi kuwalinda Waislamu kwa njia yoyote ile. Kutokana na hili mshauri wa masuala ya usalama wa serikali ya mpito amesema, "Ikithibitika kuwa wao ni raia wa Bangladesh, basi tutawakubali", na mkuu wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa cha kisekula nchini humo ameweka wazi msimamo wake, "Si Delhi wala Pindi, wala nchi nyengine yoyote, Bangladesh kwanza!" Zaidi ya hayo, wanasiasa na wasomi wa kisekula ni wanafiki na wenye chuki sana dhidi ya Waislamu hivi kwamba wananguruma kama simba marara dhidi ya mateso ya Mabaniani walio wachache nchini Bangladesh, na wanaonekana kama paka dhidi ya ukandamizaji na utesaji wa Waislamu 'wachache' nchini India. Ilhali Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَّلَى عَصَبِيَّةَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ» “Si katika sisi anyelingani Asabiyyah (utaifa), na si katika sisi anayepigana kwa ajili ya Asabiyyah, si katika sisi anayekufa kwa ajili ya Asabiyyah” (Abu Dawud). Pili, India ni mwandani wa kikanda wa mkoloni kafiri Amerika, haswa mwanachama wa Quad, moja ya miungano ya kijeshi katika eneo la Indo-Pasifiki. Kama ambavyo kafiri mkoloni Amerika inavyolitumia umbile haramu la Kiyahudi katika Mashariki ya Kati kukandamiza Umma wa Kiislamu, wao vile vile wanaitumia Dola ya Hindutva ya India katika Asia Kusini.

Enyi Waislamu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Surah Al-Anfal: 72]. Iwapo Waislamu watashambuliwa katika sehemu yoyote ya dunia, ni faradhi kwa Waislamu wengine kuwasaidia. Mumeshuhudia kwamba hawa watawala wa kisekula wa kitaifa wa Waislamu hawapeleki vikosi vyetu vya kijeshi kuwasaidia Waislamu wa Palestina, Kashmir, na Arkan, huku wakituma vikosi vya kijeshi chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa kwa wito wa Marekani na kumwaga damu. Wao sio walinzi wa Umma wa Kiislamu, bali ni wasaliti. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao Waislamu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye” [Sahih Muslima]. Waislamu wanakandamizwa duniani kote kutokana na kukosekana mlinzi halisi wa Umma wa Kiislamu – Khilafah. Hivyo basi, ni lazima tushikamane katika kusimamisha Khilafah badala ya kuwatazama watawala hawa vibaraka. Wito wetu unapaswa uwe kwa wana wa Ummah wa Kiislamu wanaofanya kazi ndani ya jeshi ili watoe nusrah (wakabidhi mamlaka) kwa chama chenye ikhlasi cha Ummah wa Kiislamu - Hizb ut Tahrir - katika kusimamisha Khilafah. Munapaswa kukumbuka kwamba huu ni wajibu wenu kama muumini.

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لاَ يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Nur: 55].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu