Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  4 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 03
M.  Jumatatu, 07 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaka Umepita na Kimbunga cha Al-Aqsa Kingali Kinatuma Mafunzo na Maadili
(Imetafsiriwa)

Mwaka mmoja umepita na watu wa Gaza wako imara na wenye subira. Mwaka mmoja sasa na Mayahudi wangali wanaendelea kushambulia, na wanaendelea na uhalifu wao dhidi ya wanawake na watoto wasio na hatia, na hata miti na mawe. Mwaka mmoja na watawala wasaliti wa Waislamu wamepotea kiupofu katika upotofu wao. Mwaka mzima sasa na majeshi ya Waislamu yamejikunyata katika kambi zao, bila kukerwa na vilio vya watoto, wala kusukumwa humo na vilio vya wanawake wa Kiislamu vya kuomba msaada, uungwana wa al-Mu'tasim!

Ulimwengu mzima umeona katika mwaka huu tangu kutekelezwa kwa Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa hadi leo ukweli kuhusu Mayahudi na sifa zao ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu alitueleza katika Kitabu chake Kitukufu. Hao ni watu wa kashfa, na wanawakanusha manabii na hata kuwaua na kila anayesema ukweli. Hao ni wavunja ahadi, viumbe waoga zaidi wa Mwenyezi Mungu, na walio makini zaidi katika maisha.

Ulimwengu umeziona sifa hizi zote, haswa uoga na hofu yao. Baada ya kushindwa kufikia malengo yao waliyotangaza walipoanza kuelekea Gaza, wakidhani ni safari ya siku moja, walishangazwa na mashujaa wanaopigana nao uso kwa uso na kutoka umbali wa pua na mdomo, na kuwaua bila hofu na kwa ujasiri usio na kifani. Waoga hawa hawakuwa na budi ila kumwaga hasira zao kwa wanawake dhaifu, wasio na hatia, watoto na wazee, na kuharibu nchi kwa kulipua mahospitali na majengo. Hatimaye, baada ya kukata tamaa ya kuwapigisha magoti mashujaa wa Gaza, umbile la Kiyahudi lilikwenda kutafuta ushindi mbali na Gaza hadi Lebanon, likinufaika na mahakikisho ya mkuu wa ukafiri, Amerika, kupitia kuzidhibiti tawala kwa midundo ya siasa za Kimarekani. Kwa hivyo, lilianza kutishia, kuahidi na kutekeleza, bila kizuizi chochote, na kuanza kuzungumza kama paka, akijivunia nguvu za simba!

Enyi Umma wa Kiislamu, na Enyi Watu Wenye Nguvu na Mamlaka ndani yake: Je, inaingia akili kwamba kundi kama hili linacheza na hisia za Waislamu karibu bilioni mbili, na lisipokee jibu ambalo lingewasahaulisha minong'ono ya Shetani?!

Enyi Majeshi ya Waislamu: Hizb ut Tahrir, tangu siku ya kwanza ya uvamizi wa Kiyahudi dhidi ya Gaza, imewaita na kuwaelezeni wajibu wa kidini kwenu. Lau mungeitikia, damu ya Waislamu 41,000 wa Gaza yenye fahari isingemwagika.

Je, nyinyi sio vizazi vya huyo babu?! Pindi Myahudi mmoja kutoka Banu Qaynuqa' alipofunua sehemu za siri za mwanamke mmoja wa Kiislamu, alipiga mayowe. Kisha akaja Muislamu, ambaye hakuwa jemedari wa jeshi wala si kiongozi wa kijeshi, bali alilelewa kwa uungwana, na akamuua Myahudi aliyefanya hivyo. Kisha Mayahudi wa Banu Qaynuqa' wakamzunguka yule Muislamu na kumuua. Jambo hilo lilipomfikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye alikuwa mtawala wa Waislamu, mara moja aliwakusanya Waislamu na kuandaa jeshi. Upesi alihamia kwenye ngome za Banu Qaynuqa' na kuzizingira. Alisisitiza kumaliza mzingiro iwapo Mayahudi watatii amri yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alihamisha jeshi kwa ajili ya mwanamke mmoja ambaye sehemu zake za siri zilifunuliwa, na mtu mmoja ambaye aliuawa bila ya haki.

Leo hii, maelfu ya Waislamu wanauawa, na sehemu za siri za maelfu ya wanawake wa Kiislamu zinafichuliwa sehemu zote za dunia mikononi mwa Mayahudi na makafiri wengine wahalifu, na hakuna hisia ya uungwana iliyokuchocheeni, Enyi Majeshi ya Waislamu mpaka sasa!

Enyi Majeshi ya Waislamu, Enyi Kizazi cha Khalid, Abu Ubaidah, na Al-Qaqa: Ni wakati sasa wa nyinyi kuregea kwenye fahamu zenu, ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, na mrekebishe dhambi ya kukaa kwenu nyuma, ili mutoke kubomoa viti hivi vibovu vya utawala kwa kutoa nusra kwa Hizb ut Tahrir; kiongozi asiyedanganya watu wake, ili kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na mutangaze jihad dhidi ya kila anayesubutu kuwashambulia Waislamu, kwani nyinyi munastahiki hilo munamiliki vifaa na idadi, juu ya yote, Aqidah (itikadi) ambayo haisimami katika njia ya matatizo yoyote.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu