Jumamosi, 18 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  10 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 1446 / 12
M.  Ijumaa, 06 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongeza kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Iraq kwa Sikukuu ya Idd al-Adha 1446 H
(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, there is no god but Allah… Allahu Akbar, Allahu Akbar, na Sifa Njema zote ni za Mwenyezi Mungu

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Iraq inatoa pongezi na baraka zake nyingi kwa Umma wa Kiislamu kwa mnasaba wa Idd al-Adha iliyobarikiwa. Hasa tunatoa salamu hizi kwa wabebaji da’wah, na kwa mwanachuoni mkubwa, Amiri wa Hizb utTahrir, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Mwenyezi Mungu amlinde na amhifadhi na ampe ushindi na tamkini kupitia mikono yake.

Enyi Waislamu: Idd hii inakuja kama zile za kabla yake, ilhali hali yenu haimfurahishi rafiki wala haimkasirishi adui tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Ni aina gani hii ya Idd wakati Gaza inaangamizwa?! Ni aina gani hii ya Idd huku wanawake watukufu wa Kiislamu wakidhalilishwa?! Ni aina gani hii ya Idd ilhali ardhi za Misikiti Miwili Mitukufu ambayo hufika mahujaji wakiitikia wito wa Mwenyezi Mungu, zimegeuka na kuwa mahali ambapo machafu yanaruhusiwa, zilizojaa ufisadi na upotovu chini ya utawala wa viongozi watepetevu?!

Enyi Waislamu: Wakati tunapofurahia katika Idd hii na nyoyo zetu zikitamani kuitikia wito wa Mola Mlezi wa walimwengu wote kwa kuhiji nyumba Yake tukufu, nyoyo zetu pia zimejaa maumivu tunaposhuhudia hali ya Umma wa Kiislamu - Umma wa kheri na uongofu - katika hali yake ya sasa ya hasara na kuchanganyikiwa, unyonge na udhalilifu. Watu wanaochukiwa zaidi na waoga zaidi wa viumbe Mayahudi wanaukandamiza, na umbile lao linashambulia kushoto na kulia, na kuzidisha jinai zake huko Palestina, Lebanon, na Syria, kwa msaada wa Magharibi kafiri, kusalimu amri kwa watawala wa Waislamu, na kimya cha majeshi ya Waislamu, kana kwamba wamekufa. Kama mshairi alivyosema wakati mmoja: "Ungesikika lau ungewaita walio hai ... lakini hakuna uhai kwa wale unaowaita!"

Enyi Waislamu: Kama vile Mwenyezi Mungu (swt) Amewajibisha juu yetu Hija, Swala, Zakat na Saumu, Vile vile Amewajibisha juu yetu kufanya kazi kwa ajili ya utabikishaji wa Sheria yake na kusimamisha Khilafah. Faradhi hii ndio taji la faradhi kwa sababu usimamishwaji wa faradhi nyengine zote kwa pamoja unategemea juu yake. Khalifa ndiye anayetekeleza hudud (adhabu za Kiislamu), anawawajibisha wale wanaopuuza swala au wanaokataa kutoa zaka, kuwasimamia mahujaji, kutangaza jihad, na kuyakusanya majeshi kubeba da’wah na kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwa Waislamu.

Enyi Umma wa Uislamu: Nyinyi ni umma unaostahiki kuiongoza dunia, huku dola yenu ikiwa ya kwanza miongoni mwa nyengine zote, bila mpinzani, na yenye uwezo wa kuchora upya ramani ya ushawishi wa kimataifa. Hili halitapatikana isipokuwa kwa kusimamishwa kwa dola hii. Wakati wa mabadiliko umewadia, wakati wa kuamka baada ya usingizi wa muda mrefu umefika. Basi inukeni, enyi Umma wa Uislamu, kunjeni mikono ya shati yenu na mufanye haraka kufanya kazi pamoja na wale wanaojitahidi kusimamisha Khilafah ngome yenu ya ulinzi na taji la faradhi zote zilizofaradhishwa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Afisi ya Habari ya Hizb utTahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 
E-Mail: hutiraq@yahoo.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu