Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 9 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: 1446 / 21 |
M. Alhamisi, 05 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Ndio Inayofanya Kazi Ipasavyo Kusimamisha Khilafah
Basi Acheni Kuvuruga Ulinganizi Wake na Kuwakamata Wanachama Wake
(Imetafsiriwa)
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Illallah, Allahu Akbar, Allahu Akbar wa lillahi Al-Hamd
Tangu kuanzishwa kwake kama chama cha kisiasa chenye msingi wa Uislamu mwaka 1953, Hizb ut Tahrir imefanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa Kiislamu wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Kiislamu, ambayo dola yake ya kwanza ilianzishwa na Mtume Muhammad (saw) mjini Madina. Ingawa inafuata njia ya Mtume (saw) ya kusimamisha dola hii, haijishughulishi na kitendo chochote cha kinguvu au kile kinachoitwa vurugu katika kufanya hivyo.
Imeeleza njia yake ya kufanya kazi na Ummah kupitia makumi ya vitabu na vipeperushi, kuelimisha juu ya Dini yake, kwa kuwasiliana moja kwa moja na wanachama wake, na juu ya faradhi ya kufanya kazi kwa ajili ya mwamko wake na kurudi kwenye nafasi yake ya kihistoria, utukufu, na heshima katika mstari wa mbele wa mataifa kupitia mradi wake wa mwanzo; kuuregesha Uislamu madarakani kupitia kuregea kwa Khilafah Rashida na kuregeshwa kwa mamlaka yake yaliyonyakuliwa kutoka kwa watawala wake vibaraka na tawala zao za kisekula zilizofungamana na Mkoloni Kafiri Magharibi.
Katika njia yake ya kufikia malengo yake yaliyo wazi na dhahiri, haipaki mafuta wala haipendelei mfumo wowote au uhalisia ambao umejikita katika kuutenga Uislamu kwenye medani ya maisha. Haifanyi kazi ndani ya uhalisia potovu au kutoka nao. Haishiriki katika kutawala na mifumo hii. Badala yake, inafanya kazi kubadilisha uhalisia huu kutoka kwenye mizizi yake ili kuubadilisha na Uislamu kama mfumo wa serikali. Ina ruwaza ya kina ya kifikra ambayo yanaitazama itikadi ya Kiislamu kama itikadi ya kisiasa na kwamba ubwana uko kwa Mwenyezi Mungu. Ina ukomavu wa kisiasa na utambuzi wa njama za maadui zake na imekuwa ikifanya kazi mara kwa mara kuzifichua kwa Ummah ili kusimama dhidi yake na kubadili mkondo wake kadiri inavyowezekana.
Ndio ambayo imefichua njama za watawala nchini Jordan ya kuukabidhi Ukingo wa Magharibi katika vita vya kejeli na Mayahudi mnamo Juni 1967 miezi kabla ya kutokea, ili kuhalalisha uhusiano nao. Hivi ndivyo tawala za kipumbavu zimekuwa zikifanyia kazi, kwa miongo kadhaa, kupitia nchi zao na kuwekwa wakfu kwa kile kinachoitwa utaifa na uhuru wa kidanganyifu, hadi kufikia hatua ya kusimama pamoja na umbile la Kiyahudi katika vita vya mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza. Hawana hisia na matukio ya mauaji ya watu wenye njaa yaliyofanywa na umbile oga la Kiyahudi.
Tangu kuanzishwa kwa Hizb ut Tahrir, vikosi vya usalama vya kidhalimu nchini Jordan vinazuia njia ya Mwenyezi Mungu na kutangaza vita dhidi ya Uislamu kwa kuwakandamiza, kuwakamata na kuwanyanyasa wanachama wa chama hiki, licha ya kujua kwamba ni chama cha kisiasa, kwa tuhuma za kuulingania Uislamu na kusema "Mola wetu ni Mwenyezi Mungu" na kisha kushikamana na njia hii. Wanauchokoza Ummah kwa ukamataji huu badala ya kuficha aibu na fedheha yao kwa kusimama pamoja na kafiri mkoloni wa Kimarekani Trump, ambaye anafanya kazi ya kufilisi kadhia ya Palestina na ambaye kiburi chake kimefanya ndimi zinyamaze. Mamlaka dhalimu nchini Jordan, katika siku hizi njema za Dhul-Hijjah, ziliwakamata ndugu wawili, Musa Abu Arqoub na Muhammad Najm Abu Arqoub, miongoni mwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, Ijumaa iliyopita, baada ya vikosi vya usalama kumnasa Najm kwa hila kwa kisingizio cha kumuokoa kaka yake kutokana na ajali.
Watawala wa Jordan na watawala wa Waislamu wamefichuliwa kwa kuwaunga mkono maadui wa Ummah. Wote ni kitu kimoja; wameupora Ummah mamlaka, wakautawala kwa ukafiri, na wakaulazimisha kushughulishwa na burudani na tasnia zake ndogo ndogo, kama vile sherehe za uhuru na mechi za kandanda, badala ya kuhuisha ibada za kumtukuza na kumhimidi Mwenyezi Mungu na kuyakusanya majeshi kupigana na umbile la Kiyahudi. Wamewadhalilisha na kuwafukarisha watu wao, na kuwafanya waishi kwa shida, umasikini, ukosefu wa ajira na madeni, huku matrilioni ya pesa zao zikienda kwa mkuu wa ukafiri, Trump, kwa pigo la kalamu.
Hizb ut Tahrir, huku ikifanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa mujibu wa njia ya Kisharia, inafahamu ukandamizaji, upinzani na kukamatwa kwake. Pia inafahamu ulaghai wa watawala, mabwana zao, na vyombo vyao vya kijasusi. Ukamataji huo wa kidhalimu hautaidhuru, kwani Khilafah ambayo inaifanyia kazi ndiyo Khilafah ya kweli, isiyopotoshwa na isiyo na shaka, na yenye msingi wa uaminifu kwa Waislamu na uadui kwa makafiri. Yaani, dola ambayo kwa hakika inashikamana na Neno la Mwenyezi Mungu na kuutekeleza Uislamu kwa njia ya kweli inayomaliza ushawishi wa Magharibi katika ardhi za Kiislamu na kuuzuia kurudi tena katika Umma. Hii ndiyo dola itakayojumuisha umoja wa Waislamu, kutoa matunzo mema, na kuregesha heshima na fahari ya Ummah. Hii ndiyo dola inayofedhehesha ukafiri na waungaji mkono wake, inauheshimu Uislamu na watu wake, na inaitikia wito wa kuwanusuru watu wa Gaza na Waislamu wote. Chama hiki kinautaka Ummah kujua kuwa kimeandaa katiba iliyo tayari kutekelezwa katika nyanja zote za maisha, vifungu vyake vinavyotokana na Qur’an na Sunnah, na kwamba dola ambayo chama hiki kinajitayarisha kuisimamisha imeandaliwa kikamilifu kwa kina.
[وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَاناً وَإِثْماً مُّبِيناً]
“Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.” [Al-Ahzab: 58]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |