Jumanne, 25 Safar 1447 | 2025/08/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  20 Safar 1447 Na: 1447 / 05
M.  Alhamisi, 14 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kauli za Netanyahu kuhusu "Israel Kubwa" ni Tangazo la Vita ambalo linafuta Mikataba, na, kwa sababu hiyo, Majeshi Yasonge, na Jambo jengine lolote lisokuwa hilo ni Usaliti
(Imetafsiriwa)

Huyu hapa mhalifu wa kivita Netanyahu anatangaza waziwazi na bila kufasiriwa kwa watawala waoga wa Kiarabu na wasemaji wao, akisema katika mahojiano na chaneli ya Kiebrania i24: “Mimi niko kwenye misheni ya vizazi na kwa jukumu la kihistoria na la kiroho, ninaamini kwa dhati ruwaza ya Israel Kubwa, ambayo ni pamoja na Palestina ya kihistoria na sehemu za Jordan na Misri.” Mhalifu Smotrich alikuwa amemtangulia kwa kauli zile zile na kunyakua sehemu za nchi za Kiarabu zinazoizunguka Palestina, ikiwemo Jordan. Katika muktadha huo huo, adui namba moja wa Uislamu na Waislamu, Rais Trump wa Marekani, alimpa idhini ya upanuzi wake akisema, “Israel ni sehemu ndogo sana ikilinganishwa na ukubwa wa ardhi hizo, na najiuliza ikiwa inaweza kupata ardhi zaidi kwa sababu kweli ni ndogo sana.”

Kauli hii inakuja baada ya umbile la Kiyahudi kutangaza nia yake ya kuukalia kimabavu Ukanda wa Gaza, baada ya Knesset kutangaza kunyakua Ukingo wa Magharibi na upanuzi wa ujenzi wa makaazi, na hivyo kuondoa suluhisho la dola mbili uwanjani. Kadhalika, kulikuwa na kauli ya Smotrich leo kuhusu mpango mkubwa wa makaazi katika eneo la E1 na kauli zake juu ya kuzuia kuanzishwa kwa dola ya Palestina, ambayo inaondoa matumaini yoyote kwa dola ya Palestina.

Kauli hizi ni sawa na tangazo la vita, ambalo umbile hili lenye ulemavu lisingesubutu kamwe kulisema lau viongozi wake wangewapata wale ambao wangewatia adabu, kuwakomesha kiburi chao, na kukomesha jinai zao ambazo zimeendelea tangu kuasisiwa kwa umbile lao na kupanuka kwake kwa msaada wa Wakoloni wa Magharibi na khiyana ya watawala wa Waislamu.

Hakuna haja tena ya taarifa za kuelezea kile ambacho kimekuwa ruwaza ya kisiasa iliyo wazi zaidi kuliko jua la mchana, na kile kinachotokea uwanjani katika matangazo ya moja kwa moja ya hujuma za umbile la Kiyahudi nchini Palestina, na tishio la kuteka sehemu za ardhi za Waislamu zinazoizunguka Palestina, ikiwemo Jordan, Misri na Syria, na kauli za viongozi wake wahalifu, ni tishio kubwa ambalo halipaswi kuchukuliwa kuwa ni madai ya kipuuzi yanayobebwa na wenye misimamo mikali ndani serikali yeke yanayoakisi hali yake ya dhiki, kama ilivyokuja katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan, ambayo, kama kawaida, ilitosheka na kulaani tu kauli hizi, kama zilivyofanya baadhi ya nchi za Kiarabu, kama vile Qatar, Misri na Saudi Arabia.

Vitisho hivyo vya umbile la Kiyahudi, na kwa hakika mauaji ya halaiki linayoyatekeleza mjini Gaza, kuunganisha kwake Ukingo wa Magharibi, na nia yake ya kutaka kujitanua, yanaelekezwa kwa watawala wa Jordan, Misri, Saudi Arabia, Syria na Lebanon, kama vile yanavyoelekezwa kwa watu wa nchi hizi. Ama kuhusu watawala, Ummah umejua majibu yao ya juu zaidi ni: kulaani, kukashifu, kusihi mfumo wa kimataifa, na kwenda sambamba na mikataba ya Marekani kwa eneo hilo licha ya Marekani na Ulaya kushiriki pamoja na umbile la Kiyahudi katika vita vyake dhidi ya watu wa Palestina. Hawamiliki chochote isipokuwa utiifu kwao, na hawana uwezo hata wa kumnywesha mtoto wa Gaza tama la maji bila idhini ya Mayahudi.

Ama watu, wanahisi hatari na vitisho vya Mayahudi kuwa ni vya kweli sio udanganyifu wa kipuuzi, kama wizara za mambo ya nje za Jordan na Kiarabu zinavyodai, ili kukwepa jibu la kweli na la kivitendo kwao. Wanaona uhalisia wa ukatili wa umbile hili huko Gaza.

Kwa hiyo, haijuzu kwa watu hawa, na hasa watu wenye nguvu na ulinzi miongoni mwao, hususan majeshi, kutokuwa na sauti katika kujibu vitisho vya umbile la Kiyahudi. Dori msingi ya majeshi, kama wanavyodai wakuu wao wa majeshi, ni kulinda ubwana wa nchi zao, hasa pale wanapowaona watawala wao wakishirikiana na maadui zao wanaotishia nchi zao kwa uvamizi. Bali, ilikuwa ni faradhi juu yao kuwanusuru ndugu zao huko Gaza kwa muda wa miezi 22 iliyopita, kwani Waislamu ni Umma mmoja kando na watu wengine, wasiogawanywa kwa mipaka wala kwa watawala wengi.

Hotuba maarufu za mavuguvugu na makabila katika kujibu vitisho vya umbile la Kiyahudi zinabakia maadamu mwangwi wa hotuba zao unabakia, kisha hupotea haraka - haswa wakati zikienda sambamba na lawama tupu za wizara ya mambo ya nje na uungaji mkono wa serikali - ikiwa hazitazuiliwa na hatua ya kivitendo ambayo haimngojei adui kwenye uwanja wake bali huhamia kumuondoa na wale wanaosimama kati yake nao. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَى سَوَاءٍ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ]

Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini. [Al-Anfal: 58].

Na kwa uchache kabisa, yeyote anayedai kulitazama umbile la Kiyahudi na vitisho vyake anapaswa kuuzuia utawala huo kwa kuufutilia mbali Mkataba wa khiyana wa Wadi Araba na kukata mahusiano na makubaliano nao, vyenginevyo chochote kisichokuwa hicho ni khiyana kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na Waislamu. Na bado suluhisho la masuala ya Waislamu linabakia katika kusimamisha dola yao ya Kiislamu kwa njia ya Utume - sio tu kuregesha maisha kamili ya Kiislamu bali pia kuwaondoa wakoloni na wale wanaowaunga mkono.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالاً وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Aal-e-Imran: 118]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu