Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  1 Sha'aban 1442 Na: 1442/09 H
M.  Jumapili, 14 Machi 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Amali Zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Kenya wakati wa Kampeni ya Kiulimwengu chini ya Kauli Mbiu:
"Katika Kumbukumbu ya Miaka Mia Moja ya Kuvunjwa Khilafah… Isimamisheni Enyi Waislamu!"

Kwa mwongozo wa Amiri wa Hizb ut Tahrir Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amlinde, Hizb ut Tahrir / Kenya imefanikiwa kumaliza kampeni ya kiulimwengu kukumbuka miaka 100 katika kalenda ya Hijria tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah, 28 Rajab Muharram 1442 H / 2021 M.

Hizb ut Tahrir / Kenya iliweza kufanya maandamano baridi baada ya swala za Ijumaa kwa wiki nne za mwezi mtukufu wa Rajab. Hili lilifanywa haswa katika miji ya pwani ya Mombasa, Malindi, Shimoni na LungaLunga. Katika mji mkuu wa Nairobi, maandamano baridi yalifanywa katika Msikiti wa Jamia, Eastleigh, Huruma na Majengo. Katika maandamano baridi ya kwanza, taarifa kwa vyombo vya habari kwa anwani: "Tokea Kuvunjwa kwa Khilafah, Kubomolewa kwa Majumba ya Ibada Yamekuwa ni Maafa kwa Waislamu Wote" iligawanywa maeneo yote ya pwani na vile vile Nairobi. Na katika wiki ya tatu, makala kwa kichwa: "Umma wa Kiislamu Kamwe Hauwezi Kushindwa na Maadui Zake".

Kampeni hii pia ilijumuisha msururu wa mihadhara ya umma katika misikiti tofauti tofauti pamoja na ugawanyaji kadi zilizo na ujumbe wa utukufu wa Khilafah, athari ya kutokuwepo kwake, ufaradhi wa kuisimamisha tena na kurudi kwake. Mnamo Machi 10, 2021 Radia  Rahma ilimkaribisha Ustadh Shabani Mwalimu - Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir / Kenya katika kipindi cha saa moja cha mazungumzo ya moja kwa moja hewani ambapo alizungumza juu ya Bishara Njema za Kurudi kwa Khilafah, msururu wa matembezi mitaani na ziara kwa watu mashuhuri na watu wenye ushawishi zilifanywa ili kuwakumbusha Umma dori yao ya chanya katika jukumu tukufu la kusimamisha tena Khilafah.

Amali hizi zilikuwa sehemu ya kampeni ya kiulimwengu iliyofanywa na Mashababu na Shababat wanyofu wa Hizb ut Tahrir kote ulimwenguni katika mwezi wa Rajab Muharram wa mwaka huu wa 1442 H - 2021 M. Hii ilikuwa kwa ajili ya kuukumbusha Umma miaka mia moja ya tukio la kusikitisha la kukomeshwa kwa Nidhamu ya Kipekee wa Kiutawala ya Kiislamu ulioanzishwa na Bwana wa Mitumbe wote Muhammad (saw), (Khilafah) iliyoangaza pembe za dunia kwa kipindi cha karne 13.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa’la kuharakisha kusimamishwa kwa Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume kwetu, na hilo sio jambo kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Yeye (swt) asema,

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 24:55].

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

#ReturnTheKhilafah

أقيموا_الخلافة#

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu