Jumatatu, 16 Muharram 1446 | 2024/07/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  20 Muharram 1444 Na: 1444/01 H
M.  Alhamisi, 18 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chaguzi za Kidemokrasia: Hadaa Inayorudiwa rudiwa kwa Umma

(Imetafsiriwa)

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC) imemtangaza naibu wa Rais William Samoei Ruto kuwa Rais mteule katika uchaguzi uliomalizika hivi punde. Muda mfupi kabla ya tangazo hilo, makamishna wanne wa IEBC walikanusha matokeo ya Urais kwa kusema; "yalifikishwa kwa njia isiyo wazi".  Raila Odinda, mshindani mkuu wa Ruto katika uchaguzi huo, alikataa matokeo na kuapa kwenda Mahakama ya Upeo juu ya kushindwa uchaguzi. Ukisifiwa na waangalizi wa kimataifa kuwa kwa kiwango kikubwa ulikuwa wa amani na "juu ya wastani", uchaguzi huo ulikuwa na idadi ndogo kabisa ya wapigakura waliojitokeza katika kipindi cha miaka 15 huku wengi ya vijana wakisusia upigaji kura.

Sisi katika Hizb ut Tahrir Kenya tungependa kusema yafuatayo:

Chaguzi za Kidemokrasia huwa ni mbinu tu za kimpito kuondoa utawala mmoja na kwa kuuleta mwengine kwa maana huhalalisha utawala ufuatao. Mchakato huu kwa hakika hauakisi wala kuonesha uhakika wa zoezi la upigaji kura kama kigezo msingi bali huwa ni kupeana uhalalishaji tu wa uongozi mpya. Kwa hivyo, zoezi zima la uchaguzi ni sura ya kidanganyifu ya kidemokrasia na ukweli kuwa uteuzi badala ya uchaguzi. Fauka ya haya misemo ya ‘Uchaguzi huru, haki na wa uwazi' ni turufu tu ya Wakoloni Magharibi ili kutunga udanganyifu unaoweka kikomo mabadiliko ya uchaguzi na ratiba inayoitwa vikomo vya muhula.

Kuhusiana na suala la ususiaji wa wapiga kura, hii inaonesha bayana kwamba raia wengi na hasa vijana wamekosa imani kwa uongozi ambao kwa muda mrefu wameshindwa kutatua matatizo yao sugu. Raia wametambua kwamba viongozi wa kisiasa wana ubinafsi wa kisiasa ambao ndio kipaumbele kwao na nambari moja kuliko maslahi ya raia. Kiasili na kimaumbile mfumo wa Kibepari husababisha unyama wa kisiasa na uchu wa kupapia mali hivyo kuwanyima raia wa kawaida mahitaji msingi.

Tunaeleza bayana kwamba mfumo batili wa Kirasilimali ndio kiini kikubwa cha matatizo yote Kenya inayokumbana nayo miongoni mwake ni ubabe wa kutojali kwa wanasiasa, ufisadi uliozagaa, mfumko wa bei na utovu wa usalama. Matatizo haya sio kwa Kenya tu bali ni kwa ulimwengu kwa ujumla. Ubepari umejikita katika kuwatajirisha matajiri na kuwanyonya maskini hatimaye kusababisha pengo kubwa kati ya matajiri na maskini. Tuna hakika kwamba katika uchaguzi wowote wa kidemokrasia katika kipindi na wakati wowote hautawahi kutoa uongozi unaodhihirisha uimarikaji wa kweli badala ya uongozi unaofanya kazi kwenye mduara wa  ushawishi wa dola za kibepari za kikoloni.

Kenya na dunia nzima inauhitaji pakubwa Uislamu na mfumo wake wa utawala (Khilafah) ulio na suluhisho la wazi la matatizo yanayowakabili wanadamu wote. Uislamu unaifafanua siasa kuwa ni kujali kwa dhati mahitaji ya watu na wala sio kuwania madaraka miongoni mwa wanasiasa wanaopigania manufaa yao binafsi. Mfumo ambapo dori ya vyama vya kisiasa haitakuwa kama vyombo dhidi ya maslahi ya Ummah. Badala yake vitapewa dori ya uangalizi ili kuhakikisha uongozi unatimiza wajibu wake na kuwafikishia raia wake wote.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari

Hizb ut-Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: [email protected]

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu