Jumanne, 14 Shawwal 1445 | 2024/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  16 Rabi' II 1445 Na: 1445/06 H
M.  Jumanne, 31 Oktoba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ziara ya Mfalme Charles: Muendelezo wa “Mzigo wa Mtu Mweupe”

(Imetafsiriwa)

Mfalme Charles III ameanza ziara ya siku nne katika koloni ya zamani, Kenya. Hii ni ziara ya kwanza ya mfalme huyo tangu kutawazwa kwa koloni zozote za Uingereza. Ziara hiyo inajiri wakati mateso, mauaji na unyakuzi mkubwa wa ardhi ambayo bado ni ya raia wa Uingereza na makampuni unatawala rai jumla ya Kenya.

Kuhusiana na suala hili, tunasisitiza yafuatayo:

Uingereza kama bwana wa kikoloni kwa ujanja na hila za kisiasa, ilikoloni Kenya rasmi kinguvu na moja kwa moja hivyo basi, mateso na mauaji yalikuwa ndio njia ya kuwanyorosha raia katika mstari wa utawala wao. Kwa sasa, Ubepari huiwezesha nguvu ya kisiasa ya Uingereza kutawala mataifa ya raia wake, ikiwemo Kenya, kupitia operesheni za mashirika ya kimataifa badala ya kwa njia ya utawala wa moja kwa moja. Zaidi ya hayo, Waingereza walitumia fikra mbovu na haribifu ya Ukoloni kutekeleza sera yao ya nje na kulinda maslahi yake ya kisiasa na kiuchumi nchini Palestina. Urithi ambao umeshuhudia mauaji ya binadamu yakitekelezwa na umbile la Kiyahudi kwa usaidizi kamili kutoka Marekani na Uingereza.

Ama kuhusu matarajio makubwa ya Wakenya kwamba Serikali ya Uingereza inajuta na kufidia unyanyasaji huo kama dhihirisho la ukombozi wa kweli kutoka kwa makucha ya ukoloni si lolote ila ni udanganyifu tu. Ukweli ni kwamba sera ya kigeni ya Uingereza imejikita katika ubeberu wa kiuchumi na ukoloni. Taasisi kama vile Oxfam, Jumuiya ya Madola na UKAid kwa kweli huingia kwenye ‘ulimwengu wa tatu’ na kufuata mtindo wa ukoloni mamboleo, kuanzisha afisi, kupata mishahara mikubwa na kutenda kama jasusi asiyejulikana kwa bwana wa kikoloni.

Tunasisitiza ziara hii ni ya kumakinisha zaidi ushawishi wa kikoloni wa Uingereza katika nchi ambayo historia yake ya hivi majuzi imeshuhudia mapambano ya Uingereza na Marekani yakidhihirishwa kupitia tawala zinazotawala na upinzani wa kisiasa. Katika kilele cha ushindani wa kikoloni kati ya (Marekani na Uingereza), Kenya inajikuta ikitekeleza ajenda za kikoloni kama vile ‘vita dhidi ya ugaidi’ kupeleka majeshi yake nchini Somalia, DRC na hivi majuzi Haiti.

Hatimaye uingiliaji kati wa wakoloni nchini Kenya na Afrika kwa jumla umezua masaibu na misukosuko zaidi. Ni kwa kuondolewa kwa ushawishi wa kikoloni na kuregea kwa Dola ya Khilafah ndipo usalama na ustawi vitaregea kwa ajili ya kusini mwa dunia.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu