Ijumaa, 09 Muharram 1447 | 2025/07/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  6 Muharram 1447 Na: 1447/01 H
M.  Jumanne, 01 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Uamuzi wa Mahakama ya Upeo Unaipa Zinaa Nafasi sawa na Ndoa

(Imetafsiriwa)

Mahakama ya Upeo imeamua kuwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa na baba Waislamu wana haki ya kurithi mali ya baba yao, jambo linaloashiria maendeleo makubwa katika tafsiri ya sheria za kibinafsi za Kiislamu nchini Kenya. Hii ni baada ya Mahakama ya Juu mnamo Jumatatu tarehe 30 Juni kutupilia mbali rufaa ya Fatuma Athman Abud Faraj, ambaye alitaka kuwatenga watoto wa marehemu mumewe, Salim Juma Hakeem Kitendo, katika mali yake kwa madai kwamba walizaliwa nje ya ndoa inayotambulika ya Kiislamu.

Kwa muktadha huu Hizb ut Tahrir Kenya ingependa kubainisha yafuatayo:-

Kwa kuwa utawala wa Kenya ni wa kisekula (unaofuata itikadi ya kutenganisha Dini na Maisha), uamuzi huu sio wa kushangaza hata kidogo. Hii ni kwamba, usekula – itikadi ya kimagharibi unaamini kwamba dini na serikali hupaswa kutenganishwa na mwanadamu hupawa uhuru kamili. Kwa muktadha huu, mahakama ya upeo sio taasisi ya kuzingatia maadili ya Kidini, badala yake inashikilia mawazo ya kibinidamu. Kuwapa haki ya mirathi watoto waliozaliwa nje ya ndoa, kwa maana nyengine kuhalalisha uzinzi (uovu), yaani kwa ibara nyengine kusawazisha uchafu wa zinaa na ndoa, hili likiwa ni dhihirisho wazi kuwa itikadi ya kisekula hutukuza uhuru wa mwanadamu na mawazo kuliko maadili na sheria za dini.

Kutetea na kulinda “haki” za watoto waliozaliwa nje ya ndoa ni sehemu tu ya kampeni kubwa inayoendeshwa na dola kuu za Kimagharibi dhidi ya Uislamu. Hakikisho hili la kikanuni sambamba na propaganda dhidi ya Sheria za Kiislamu yote huenezwa kwa ngazi zote za jamii kuhalalisha uzinzi na maovu mengine. Hali hii imepelekea kuongezeka idadi ya watoto randaranda mitaani ambao wamekuwa ni tishio la usalama katika miji mikubwa.  Inafahamika wazi kwamba chokoraa nchini Kenya wanakabiliwa na masaibu mengi ikiwa ni pamoja na umaskini, ukosefu wa mahitaji ya kimsingi, matatizo ya afya, na kuathiriwa na aina mbalimbali za unyanyasaji. Hata hivyo, changamoto hizi zinachangiwa zaidi na kushindwa kwa familia katika kutekeleza wajibu wake kamili unaochangiwa na uzembe wa serikali katika kusimamia kusimamia mambo ya watu.

Kinyume chake, Uislamu umefaradhisha na kubaini kwamba asili jukumu la kuchunga mambo ya watoto ni la wanafamilia kisha na serikali. Ama kuhusu mirathi, Uislamu huwapa mirathi watoto waliozaliwa katika ndoa, ama wale waliozaliwa nje ya ndoa na wanaotoka kwenye familia masikini hawastahiki kurithi ingawa ni jukumu la Serikali kuwasimamia: Mtume (saw) amesema:

«أَنَا أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ، مَنْ تَرَكَ مَالًا فَلِأَهْلِهِ، وَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضِيَاعًا، فَإِلَيَّ، وَعَلَيَّ»

“Mimi niko karibu zaidi na Waumini kuliko nafsi zao, basi atakayekufa (miongoni mwao) na kuacha baadhi ya mirathi, urithi wake utapewa ‘Asaba yake, na atakayekufa akiwa ameacha deni au watoto basi hao ni wangu na juu yangu kuwasaidia.”

Hatimaye, tunawaomba Waislamu wasilipuuzilie mbali jambo hili kwa vile ni sehemu ya vita vya kimataifa dhidi ya Uislamu. Tunahisi kuwa uamuzi huu utachukuliwa kama mfano katika taasisi nyingine za kimahakama duniani kote ili kuhujumu sheria ya Kiislamu kuhusu mirathi. Tunatoa mwito kwa Waislamu wote wenye ushawishi nchini Kenya ikiwa ni pamoja na mawakili Waislamu na wale walio katika nyadhifa za kisiasa kupaza sauti zao katika kuutetea Uislamu.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu