Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  3 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 H / 039
M.  Jumatatu, 14 Juni 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Majeshi ya Waislamu! Uhangaishwaji wa Watoto wa Kipalestina na Umbile la Kiyahudi Hautakoma Isipokuwa kwa Kwenda Kwenu Kuung'oa Uvamizi Huu Katili kwa Mizizi Yake!

(Imetafsiriwa)

Kulingana na wanaharakati na mawakili wa Palestina, umbile vamizi la Kiyahudi limeimarisha ulengaji wao wa watoto wa Kipalestina kwa ajili ya kuwakamata kwa wiki chache zilizopita kama sehemu ya "Operesheni Sheria na Utangamano", ambao wengi wao wamepigwa kinyama na kuteswa kisaikolojia. Mnamo Mei 20, Mohammed Saadi mwenye umri wa miaka 13 alitekwa nyara, akafunikwa macho, akapigwa na kutishiwa na bunduki kichwani mwake na wanachama 5 wa Musta'ribeen, kitengo cha siri kinachojifanya kama Wapalestina wa polisi wa umbile la Kiyahudi. Mwishoni mwa Mei, jeshi la polisi la uvamizi huo lilitoa taarifa ambayo ilisema kwamba zaidi ya Wapalestina 1550 wamekamatwa tangu Mei 9, ikiwemo mjini Haifa, Yafa, Lydd, al-Jalil na al-Naqab, na kwamba maelfu ya vikosi vya usalama kutoka vitengo vyote vitatumwa kutekeleza uvamizi wa nyumba katika miji na majiji yanayokaliwa zaidi na Wapalestina. Makumi ya wale waliokamatwa katika kampeni hii ya ugaidi wamekuwa watoto, wengine wakiwa na umri wa miaka 10, 11 na 12, ambao wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka 20 jela.

Wimbi hili la sasa la kukamatwa kwa watu wengi na kuwekwa kizuizini linalenga kuadhibu vijana na familia za Wapalestina ambao walijitokeza kusaidia ndugu na dada zao huko Sheikh Jarrah, na pia dhidi ya mashambulizi ya Al-Aqsa na mashambulizi ya kijeshi juu ya Gaza ya umbile la Kiyahudi. Kampeni hii inayolenga kukihangaisha kizazi kichanga cha Wapalestina pia inakusudia kuzima na kuzuia uasi wowote wa siku za usoni dhidi ya uvamizi huu wa kinyama. Mawakili wametoa maoni yao kwamba visa hivi majuzi vya kukamatwa vimeashiria kiwango chake cha ukatili, ambao umesababisha mifupa kuvunjika kwa wale waliowekwa kizuizini. Youssed al-Zayed, wakili wa al-Jalil alisema kuwa hii ilikuwa mara ya kwanza kuona "watoto wakikamatwa kwa idadi kubwa na kwa unyonge kama huu." Aliuelezea ukamatwa kama njia ya, "kutisha kizazi kizima kutokana na kulizungumza hili ... Ni jaribio la kuzima ari yao."

Bila shaka, hii ni sura tu ya hivi majuzi ya kuenea na utaratibu wa kutisha na unyanyasaji wa umbile la Kiyahudi kwa watoto wa Kipalestina. Kulingana na shirika la Defence for Children International - Palestina (DCIP), tangu 2000, jeshi la umbile la Kiyahudi "limewaweka kizuizini, kuwahoji, kuwashtaki na kuwafunga" karibu watoto 13,000 wa Kipalestina, na kwamba kawaida hushtaki watoto 500 hadi 700 kila mwaka katika mahakama za kijeshi. Ripoti ya Wizara ya Habari ya Palestina iliyochapishwa Machi 2019 ilisema kuwa asilimia 95 ya watoto wa Kipalestina waliokamatwa na umbile la Kiyahudi waliteswa wakati walipokuwa kizuizini.

Enyi Watoto wa Majeshi ya Waislamu! Watoto na vijana wa Palestina wanatishwa kwa kutetea matukufu ya Dini yao, wakisimama kuunga mkono Umma wao, na kukabiliana na uvamizi huu katili… wakati nyinyi munabaki katika kambi zenu, mumeacha jukumu lenu la Kiislamu la kuikomboa Ardhi hii Iliyobarikiwa na Al-Aqsa aliyetekwa na serikali za nchi za Kiislamu ambazo zimeuza roho zao kwa mabwana zao wa Kimagharibi, kusawazisha mahusiano na mchinjaji wa watoto wa Gaza, na kusaidia na kukuuza uvamizi huu wa jinai kupitia kupitia kutochukua hatua kwao na mafungamano yao ya kiuchumi. Mnawezaje kuvumilia kuhudumu chini ya watawala hawa wasaliti na wasio na msimamo ambao hawajali chochote katika Dini yenu, Ummah wenu na wameliaibisha jina lenu? Ni wazi kabisa kwamba jinamizi hili la muda mrefu la miongo 7 ambalo Waislamu wa Palestina wamelivumilia halitaisha kamwe isipokuwa kila shubiri ya uvamizi huu katili wa kinyama ung'olewe kutoka katika Ardhi hii Iliyobarikiwa, na hili halitatekelezeka isipokuwa kwa uhamasishaji wa jeshi la Kiislamu. Kwa hivyo Ummah huu wa Kiislamu unakutazameni nyinyi - ndugu zetu, baba na watoto wa nguvu za kijeshi - kujibu Amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na kufuata nyayo za majenerali wakuu wa Kiislamu wa zamani kama Khalid bin Walid (ra), Salahuddin Ayyubi na Muhammad ibn Qasim kupitia kusonga mbele na kuuhami Ummah wenu na Dini na kutoa Nussrah yenu kwa ajili ya kusimamishwa Khilafah kwa njia ya Utume ambayo itakuwa ngao na mlezi wa Waislamu na kuleta heshima kwa jina lenu!

]وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako?’"[4: 75]

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu