Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  6 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 034
M.  Jumatano, 09 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauaji Yasiyokwisha ya Wanawake na Watoto wa Gaza Kamwe Hayatamalizika hadi Mlinzi na Ngao ya Ummah, Khilafah, Itakaposimamishwa tena

(Imetafsiriwa)

Mwaka mmoja umepita tangu kampeni ya hivi punde zaidi ya mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza mikononi mwa umbile la mauaji la Kiyahudi kuanza, ikiwa na zaidi ya mashahidi 41,000. Uvamizi huu wa umwagaji damu haujatofautisha kati ya mwanamume, mwanamke, mtoto au mtoto mchanga katika kushambulizi lake, kwani 70% ya waliouawa ni wanawake na watoto. Kwa mujibu wa Oxfam, wanawake na watoto wengi zaidi wameuawa mjini Gaza na jeshi la Kizayuni katika kipindi cha mwaka mmoja kuliko kipindi sawia cha mzozo mwingine wowote katika muda wa miongo 2 iliyopita. Zaidi ya watoto 25,000 huko Gaza wamepoteza mzazi mmoja au wote wawili katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kutokana na vita hivi, na kwa uchache watoto 3000 wamepoteza miguu na mikono kutokana na mashambulizi ya mabomu (kulingana na Al Jazeera). UNRWA imeripoti kuwa kila siku watoto 10 huko Gaza wanapoteza mguu mmoja au yote miwili kwa wastani, na kufanya hili kuwa kundi kubwa zaidi la watoto waliokatwa viungo katika historia, wengi wakifanyiwa bila ganzi.

Haya yote ni pamoja na kuendelea kwa njaa, vifo vinavyotokana na njaa, ukosefu wa maji safi, kunyimwa huduma za afya na kuenea kwa magonjwa hatari ya kuambukiza, yanayotokana na kuzingirwa kikatili kwa Ukanda huo na uharibifu wa usambazaji wa maji, mifumo ya usambazaji wa chakula, na hospitali - ambazo zimeathiri hasa - wanawake na watoto wa Gaza. Jarida la matibabu la Lancet lilisema mwezi Julai kwamba vifo kutokana na uvamizi huu wa Gaza vinaweza kufikia hadi 180,000 ikiwa vifo visivyo vya moja kwa moja kutokana na njaa, ukosefu wa huduma za afya na uharibifu wa miundombinu muhimu ya kiraia itazingatiwa. Shirika la ‘Save the Children’ limesema kuwa karibu 90% ya majengo ya shule huko Gaza yameharibiwa au kuvunjwa. Lengo la wazi la haya yote ni kuharibu mustakabali wowote unaowezekana kwa watoto wa Gaza na vizazi vijavyo.

Huu ni mwaka ambao umeonyesha kwa mara nyingine tena ugumba wa mfumo wa sasa wa dunia, na serikali zake, Umoja wa Mataifa na kila mahakama na taasisi za kimataifa kuwalinda Waislamu wanaodhulumiwa dhidi ya dhalimu wao. Umbile la Kiyahudi limevuka kila mstari mwekundu, limevunja kila mwiko na limekiuka kila kanuni na sheria ya kibinadamu, lakini hakuna serikali ambayo ina utashi wa kisiasa wa kukomesha mauaji haya yasiyokoma. Dola za magharibi zimedhihirisha nia yao ya kuruhusu uvamizi wa kihalifu kutekeleza kampeni yake ya mauaji ya kikabila ya Wapalestina bila ya kuadhibiwa, na kwa hakika zimesaidia mauaji yake ya halaiki bila wasiwasi wowote - zikiupatia msaada wa kifedha na kisiasa bila masharti bila kujali kina cha uharibifu huo. Mnamo Agosti, utawala wa Biden uliidhinisha nyongeza ya dolari bilioni 20 za mauzo ya silaha kwa umbile la Kiyahudi ili kusaidia kufadhili mauaji haya makubwa na uvamizi wa kikatili. Wakati huo huo, watawala na serikali za nchi za Waislamu zilizopandikizwa na nchi za Magharibi na zinazoungwa mkono na nchi za Magharibi zimeonyesha kwa mara nyengine tena kwamba utiifu wao upo kwa mabwana zao wa Magharibi na koloni lao la Kiyahudi – kuendeleza uhusiano wao wa kidiplomasia, kiuchumi na wa kuhalalisha mahusiano na uvamizi huo, hata kuruhusu kambi zao za kijeshi, anga na ujasusi kutumiwa kulinda umbile la Kiyahudi kutokana na madhara, kama vile Jordan na Saudi Arabia.

Ni uthibitisho gani zaidi unaohitajika kuona kwamba hakuna uongozi, hakuna dola, hakuna mtawala leo ambaye anasimama kwa dhati kwa ajili ya Waislamu na yuko tayari kutumia jeshi lake kutetea damu yao?!! Je, tunahitaji kushuhudia nini zaidi ili kuelewa kwamba jeshi halitakusanywa kuikomboa Palestina bila ya kusimamishwa dola inayotawala kwa Uislamu pekee, mtetezi wa Dini, na inayowajibika kuwa walinzi na ngao ya Ummah?!! Dola hiyo ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume - Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo, kukomesha mauaji haya ya halaiki kunahitaji zaidi ya kulaani mauaji na kuomba dua. Inatuhitaji tufanye kazi ya kulaani mauaji na kuomba dua. Inatuhitaji tufanye kazi kwa ajili ya kusimamishwa kwa haraka kwa Khilafah ambayo Dini yetu imeifafanua kuwa ni chombo cha kulinda na kukomboa Ummah wetu na ardhi zake. Hii ni pamoja na kuwataka wale waliomo katika majeshi ya Waislamu kutoa Nusrah yao (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamishwa kwa dola hii, ambayo itawahamasisha kung'oa uvamizi huu wa saratani kutoka kila shubiri ya Palestina, na kusimamisha mamlaka ya Uislamu juu ya ardhi hii iliyobarikiwa kwa mara nyingine tena, na kwa hayo kuhakikisha ulinzi, utu na usalama kwa wote wanaoishi chini ya utawala wake! Mtume (saw) amesema: «إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao, watu hupigana nyuma yake na hujihami kwaye.”

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu