Alhamisi, 03 Sha'aban 1447 | 2026/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  28 Rajab 1447 Na: H.T.L 1447 / 16
M.  Jumamosi, 17 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la kila Mwaka la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon
Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 105 ya Kuvunjwa kwa Khilafah
“Kuhalalisha Mahusiano na Kujisalimisha, au Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Dola ya Uislamu?!”
(Imetafsiriwa)

Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon ilifanya kongamano lake la kila mwaka la kisiasa kwa kichwa: “Kuhalalisha Mahusiano na Kujisalimisha, au Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Dola ya Uislamu?!”, ambapo wazungumzaji kutoka Lebanon, Syria, Uturuki, na Gaza walishiriki.

Kongamano hilo linakuja huku kukiwa na ongezeko la Marekani katika kanda hii, na njia ya uhalalishaji mahusiano ambayo Amerika inajaribu kuilazimisha juu ya ardhi za Waislamu.

Katika taarifa yake ya kuhitimisha, kongamano hilo lilithibitisha kwamba kile kinachoitwa mpango wa Amerika kwa Mashariki ya Kati sio majibu ya hali ya migogoro, bali ni mradi jumuishi wa udhibiti wa kimkakati, unaolenga kuimarisha umbile la Kiyahudi, kuzuia umoja wa Ummah wa Kiislamu, na kuendeleza utegemezi wa kisiasa na kiuchumi kupitia zana za ndani na tawala za tiifu.

Kongamano hilo lilisisitiza kwamba njia zinazofadhiliwa na Amerika chini ya majina ya “amani,” “mageuzi,” na “utulivu” hazipelekei kwenye ukombozi wa kweli wala kuregeshwa kwa ubwana, lakini zinasimamiwa ndani ya dari la Amerika na kuupa mradi wa udhibiti uhalali zaidi.

Pia ilithibitisha kwamba Khilafah kwa njia ya Utume inawakilisha njia badali kamili ya kisiasa inayoweza kukabiliana na miradi ya kuhalalisha mahusiano na kujisalimisha, kwani ni mfumo wa utawala uliojumuishwa kimaumbile, unaochipuza kutokana na Aqida ya Ummah na kutegemea ufahamu na nguvu zake, sio juu ya masuluhisho ya kivipande au masuluhisho yaliyolazimishwa.

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon ilihitimisha kongamano lake kwa kuthibitisha kwamba ardhi za Ash-Sham, kuu miongoni mwazo Palestina, Lebanon, na Syria, ndizo zinazounda mhimili wa mzozo na mradi wa Marekani, na kwamba kutambua umoja wa kulenga na muunganiko wa hali hiyo ni sharti muhimu kwa mabadiliko yoyote ya kweli, ikijadidisha ulinganizi wake kwa Ummah na watu wenye nguvu na ushawishi ndani yake kufanya kazi kubwa ya kusimamisha hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, katika kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na kunusuru Dini Yake.

[وَاذْكُرُوا إِذْ أَنْتُمْ قَلِيلٌ مُسْتَضْعَفُونَ فِي الْأَرْضِ تَخَافُونَ أَنْ يَتَخَطَّفَكُمُ النَّاسُ فَآوَاكُمْ وَأَيَّدَكُمْ بِنَصْرِهِ وَرَزَقَكُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ]

“Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, mkionekana wanyonge katika nchi, mnaogopa watu wasikunyakueni, naye akakupeni pahala pazuri pa kukaa, na akakutieni nguvu kwa nusura yake, na akakupeni riziki nzuri ili mpate kushukuru.” [Al-Anfal:26]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 009616629524
http://www.tahrir.info/
Fax: 009616424695
E-Mail: ht@tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu