Alhamisi, 24 Sha'aban 1447 | 2026/02/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  17 Sha'aban 1447 Na: HTM 1447 / 03
M.  Alhamisi, 05 Februari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuikaribisha Ziara ya Modi: Khiyana ya Wazi kwa Damu na Heshima ya Umma wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amepangwa kufanya ziara ya kikazi nchini Malaysia mnamo Februari 7-8, 2026, na inaripotiwa kwamba anatarajiwa kupokea mapokezi makubwa kutoka kwa serikali na jamii ya Mabaniani nchini Malaysia. Kibaraka huyu wa Amerika mara nyingi hupokea mapokezi ya heshima katika nchi nyingi kote duniani na hupewa tuzo nyingi na nchi anazotembelea, wakiwemo watawala Ruwaibidha wa Waislamu, kiasi kwamba baadhi wako tayari kukita masanamu ili tu kumfurahisha kiongozi huyu mshirikina.

Ulimwengu wa leo unaendelea kushuhudia jinsi watawala wa Waislamu wanavyoonyesha usaliti wao dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), na Waumini kwa kushirikiana na maadui wa Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hayo, watawala hawa wanaonyesha kupuuza kabisa hisia na hadhi ya Waislamu kwa kumwalika mchinjaji huyu wa Ummah kwenye ardhi zao. Uhalifu wa Modi dhidi ya Waislamu nchini India hauna tofauti na uhalifu wa Mayahudi dhidi ya Waislamu nchini Palestina au uhalifu wa China dhidi ya Waislamu wa Uyghur. Mauaji, mateso, na aina zote za dhulma zinazofanywa na wahalifu hao zinashuhudiwa na ulimwengu mzima, na kudhihirisha chuki yao kali dhidi ya Uislamu na wafuasi wake. Ni kweli kauli ya Mwenyezi Mungu (swt):

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةً لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟]

“Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina.” [Al-Ma’idah (5): 82].

Hizb ut Tahrir / Malaysia inaeleza pingamizi yake kali, na inatoa onyo kali kwa serikali ya Malaysia kuhusu ziara ya Modi. Modi sio tu mkuu wa nchi ya kigeni; ni adui dhahiri wa Uislamu. Yeye ni ishara ya itikadi kali ya Hindutva ambayo ni uadui dhidi ya Uislamu na Ummah wa Kiislamu. Chini ya uongozi wake, Waislamu nchini India wanaendelea kukandamizwa, kuuawa, na kutendewa kikatili. Zaidi ya hayo, anashiriki katika ubomoaji wa misikiti na uwekaji wa aina zote za ubaguzi dhidi ya Waislamu katika jaribio la kuwafukuza kutoka kwenye dini yao, akilenga kuigeuza India kuwa dola ya Kibaniani iliyojengwa juu ya itikadi ya chuki dhidi ya Uislamu. Mauaji na ukandamizaji huko Kashmir pia ni damu mikononi mwake. Kwa kifupi, mikono yake bado ina damu ya Waislamu hadi leo. Kumkaribisha mtu kama huyo kwa kutandia zulia jekundu ni kitendo kinachokiuka Sharia, kusaliti damu na hadhi ya Ummah wa Kiislamu, na kuumiza sana nyoyo za Waislamu, haswa wale walio nchini India na Kashmir.

Kumkaribisha “Muuaji wa Gujarat” kwa misingi ya urafiki, uhusiano wa kidiplomasia, na maslahi ya kiuchumi ni ushahidi zaidi kwamba watawala na mfumo wa kidemokrasia unaotekelezwa leo wametenganisha waziwazi dini na siasa na utawala wa serikali. Kwao, urafiki na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) na kuzingatia faida za kibiashara ni muhimu zaidi kuliko kutii amri za Mwenyezi Mungu (swt), na muhimu zaidi kuliko kulinda maisha na heshima ya ndugu zao. Wanasubutuje kukiuka amri ya Mwenyezi Mungu (swt) wakati Yeye (swt) asema:

[لَا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِ الْمُؤْمِنِينَ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ]

“Waumini wasiwafanye makafiri kuwa wapenzi wao badala ya Waumini. Na anaye fanya hivyo, basi hatakuwa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu.” [Aali Imran (3): 28].

Hakika, usaliti wa watawala wa Waislamu na udhaifu wa Ummah—matokeo ya mipaka ya dola za kitaifa—umewapa ujasiri maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) sio tu kukanyaga ardhi za Waislamu bali pia kuhisi bora kuliko Waislamu, ambao wanalazimika kuwaheshimu licha ya kuonyesha wazi uadui wao dhidi ya Uislamu. Viongozi wa Waislamu leo ​​wako tayari zaidi kulinda hazina zao na “maslahi ya kitaifa” finyo huku wakipuuza mateso ya ndugu zao ng'ambo ya mipaka.

Tungependa kukariri kwamba serikali ya Malaysia haipaswi kukubali ziara ya Modi; badala yake, inapaswa kukata uhusiano wote na utawala unaomwaga damu ya Waislamu. Kumbuka kwamba adui hapaswi kamwe kutendewa kama rafiki, na adui wa Mwenyezi Mungu (swt) hapaswi kamwe kuchukuliwa kama mshirika. Chini ya uongozi unaopuuza sheria ya Mungu, ni mara ngapi ardhi ya Malaysia imekanyagwa na maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) kutoka Uingereza, China, Amerika, na sasa India imepewa fursa ya kuinajisi. Watawala hawa wanasahau kwamba mamlaka ni ya muda tu, na watawajibika mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) kuhusu ni nani waliyemfanya rafiki na ni nani waliyemruhusu kudhulumiwa.

Hakika, Ummah huu unahitaji sana uongozi wa Khalifa ambaye ni mcha Mungu, shujaa, na imara—ambaye ataamiliana na maadui kama maadui na marafiki kama marafiki. Khalifa huyu hatakataa tu kuwaacha ndugu zake wauawe, lakini pia hataruhusu heshima yao ichafuliwe hata kidogo. Adui yeyoye atakayesubutu kufanya hivyo, jibu watakalopewa itakuwa kile cha mtema kuni watakachokiona, sio kile watakachokisikia. Hakika, kurudi kwa Khalifa kumekaribia, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu