Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Muharram 1360 Na: 1441 H /27
M.  Jumapili, 08 Disemba 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwamko wa Kiislamu Utaletwa na Khilafah Pekee, Kwa hiyo Watu wenye Nguvu Wajitokeze na Nussrah yao kwa ajili ya Khilafah kwa Njia ya Utume

Mjadala umetanda ndani ya mitandao ya kijamii nchini Pakistan kuhusiana na video kupitia twitter kutoka kwa mwanajeshi mkuu wa majeshi ya majini akilingania Uislamu kutawala dunia. Admiral Zafar Mahmood Abbasi alitangaza kwamba Pakistan inaweza kuwa ndio kianzio cha kurudi kwa utukufu wa Uislamu, na kuongezea kwamba Waislamu walitawala dunia kupitia Uislamu, ilhali Ulaya ilitawala dunia kupitia kuipinga dini. Hakika, mwito wa kutawala kwa Dini ya Ukweli ndio hitajio maarufu la Waislamu, ikijumuisha wale walioko ndani ya jeshi. Lakini, watawala walioko lazima wasiruhusiwe kuelekeza kombo hisia za Kiislamu ili kutoa mwanya kwa Demokrasia, kwa kulingania sura yake mpya ima ni ya kiubunge, kiurais au nyingineyo. Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya,

(وَلَا تَلْبِسُوا الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُوا الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ) “Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.” [Al-Baqarah 2:42]

Enyi Maafisa wa Majeshi ya Pakistan! Nguvu za kijeshi ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amewapa, zinawapa uwezo wa kuifanya Pakistan kuwa ndio kianzio cha kurudi kwa Uislamu kama mwenendo wa maisha. Izikeni maiti inayonuka ya Demokrasia kwa kutoa Nussrah kwa Hizb ut Tahrir ili isimamishe Khilafah kwa Njia ya Utume. Tumieni nguvu zenu kuisimamisha dola yenye katiba ambayo kila kipengee chake kina dalili kutoka katika Qur’an na Sunnah. Simamisheni dola itakayofanyakazi ya kuunganisha Ardhi za Waislamu kuwa dola moja, badala ya kuzigawanya na kuzidhoofisha kwa mujibu wa mchoro wa mataifa ya Wamagharibi. Itoeni Nussrah yenu kwa uongozi wa Kiislamu ambao utapambana na ukandamizaji kwa nguvu za kijeshi kinyume na mazungumzo mezani, post za twitter na makubaliano. Mwageni damu zenu kupitia silaha zenu kwa kuilinda dola inayozikusanya rasilimali za Waislamu ili kulinda ustawi wa raia wote wa Dola kinyume na kuzisalimisha rasilimali hizi ili zitumiwe na wakoloni.

Hakika, Khilafah sio chaguo tu miongoni mwa machaguo, ni faradhi juu yetu sote, ambayo kuitelekeza imefungwa kuwa ni moja katika vifo vibaya, kufa pasina Uislamu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema, «مَنْ مَاتَ وَلَيْسَ فِي عُنُقِهِ بَيْعَةٌ مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً» “Yeyote atakayekufa pasina ahadi ya utiifu shingoni mwake amekufa kifo cha Jahilliyah.” (Muslim). Na Khilafah ni faradhi juu yetu katika kila zama na ambayo Mtume (saw) alisema kuihusu:

«وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي وَسَتَكُونُ خُلَفَاءُ فتَكْثُرُ» قَالُوا: فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «فُوا بِبَيْعَةِ الْأَوَّلِ فَالْأَوَّلِ وَأَعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ فَإِنَّ اللَّهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ» “Hakuna Mtume baada ya mimi, lakini kutakuwepo Makhalifa. Wakauliza, “Watuamrisha tufanyeje? Akajibu, “Wapeni ahadi ya utiifu mmoja baada ya mwengine, kwani Mwenyezi Mungu atawauliza kuhusu amana Aliyowapa.” (Bukhari) Kwa hiyo simamisheni zama mpya ya utawala wa Uislamu kupitia Nussrah yenu, ili mpate radhi za Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu