Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Rabi' II 1443 Na: 1443 / 20
M.  Jumamosi, 06 Novemba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bila ya Uislamu Kututawala, Watawala wa Sasa Husababisha Tufani ya Mfumko wa Bei kwa Kujisalimisha kwa Mfumo wa Kiuchumi wa Amerika  

(Imetafsiriwa)

Hotuba ya tarehe 3 Novemba 2021 ya Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan, kuhusu mfumko wa bei ilikuwa ni kuandaa maoni kwa kundi jengine la sera angamivu za kiuchumi za IMF. Kifurushi kinachojulikana kama "msaada" wa Rupia bilioni 120 kilichotangazwa kwa watu milioni 20, ni sawa na Rupia 1,000 pekee kwa kila mtu kila mwezi, kwa miezi sita. Hii ni huku watu wa matabaka ya wastani na maskini wakikandamizwa na mfumko wa bei, huku sukari ikiwa karibu Rs.150 kwa kilo, mafuta ya kupikia ni Rs.350 kwa kilo na gharama ya uniti ya umeme ni zaidi ya Rs.20. Ilhali, kwa kujisalimisha kwa mfumo wa kiuchumi wa Amerika, watawala wa Pakistan wanaifunga sarafu ya nchi kwa dolari, na kusababisha Rupia kushuka thamani kwa zaidi ya asilimia 55 dhidi ya dolari tangu Agosti 2018, na kusababisha mfumko wa bei uliokithiri na kushuka kwa nguvu ya ununuzi ya Rupia. Hata hivyo, utawala wa "tabdeeli" (mabadiliko) unakataa kutoa sarafu inayotegemezwa juu dhahabu na fedha, kama Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alivyotangaza, licha ya madai yake kwamba inataka kusimamisha dola kama ya Madina. Hakika, kufeli kwa kila uongozi wa kiraia na kijeshi ni kwa sababu wote wameufunga uchumi wa Pakistan kwa minyororo ya mfumo wa sasa wa kimataifa.

Mfumko wa bei ndani ya dola ya Khilafah huondolewa kupitia hukmu za kisheria za mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Kwa vile Riba (riba) ni Haraam, Khilafah itakataa kulipa Rs.3,000 bilioni zinazotumika kila mwaka kwa sasa kwa malipo ya riba, ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya majukumu ya Kiislamu. Dola ya Khilafah itaendeleza viwanda vizito, miradi ya miundombinu na mawasiliano ya simu kama mali ya serikali. Itasimamia ipasavyo mali ya umma ya nishati na madini. Kwa hivyo itamaliza uporaji wa matrilioni ya rupia kutoka kwa mwananchi wa kawaida, ili kujaza mifuko ya wawekezaji binafsi na makampuni ya kimataifa, baada ya ubinafsishaji. Khilafah itamaliza utawala wa dolari kwa kutoa sarafu ya dhahabu na fedha, na kukomesha mfumko wa bei uliokithiri kwa kuzuia uchapishaji usiokoma wa pesa zisizo na thamani halisi, pesa za karatasi ili kulipa deni la serikali. Khilafah italeta unafuu wa moja kwa moja kwa watu wote, wafanyibiashara na vitengo vya viwanda, kwa kuondoa kodi zote zisizo za moja kwa moja na nyingi ya kodi za moja kwa moja za bidhaa na huduma zinazojirudia rudia. Khilafah haitatoza ushuru wowote kwa uagizaji bidhaa kwa wafanyibiashara wake wa ndani, Waislamu au Madhimmi wasiokuwa Waislamu, hivyo manufaa yoyote ya bei ya chini katika soko la kimataifa yanaweza kupitishwa kwa wananchi. Tofauti na utekaji nyara wa kipote cha wachache katika Demokrasia, ambapo sheria zinatungwa kwa manufaa ya kipote cha warasilimali wachache waliochaguliwa, katika Khilafah sheria za serikali haziwezi kubadilishwa, kwa kuwa zinatokana na Quran na Sunnah Tukufu. Khilafah itatoa adhabu mara moja kwa wakiritimba, makundi na wenye kuhodhi. Hakuna mtu anayeweza kununua mahakama za Khilafah, pamoja na maamuzi yake ya haraka kwa kuzingatia hukmu za Shariah. Khilafah itatoa usalama wa chakula kwa eneo hilo kwa kutekeleza sheria kali za Kiislamu kuhusu ardhi ya kilimo. Na Dola ya Khilafah itadhamini moja kwa moja mahitaji yote ya kimsingi kwa raia wake wote, bila ya kujali rangi wala dini.


Enyi Watu wa Nguvu! Ukweli umedhihiri. Huku mfumo wa kiuchumi wa Amerika ukitutawala, hakuna haja ya jaribio jengine lenye kufeli, katika wakati ambapo Waislamu wa Pakistan wananyimwa hata milo miwili kwa siku. Ni wakati wa kuuzika nidhamu na mfumo huu mbovu. Wakati wa msimu wa kikao cha ‘Ukaz, na sherehe nyengine kama hizo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mwenyewe alikuwa akitangaza sio tu habari njema zinazohusu Pepo bali pia habari za matarajio ya matumaini kwa waumini wa kweli katika Ulinganizi wa Uislamu. Angewaambia waziwazi kwamba bila shaka wangefanikiwa, watatawala Arabuni yote na kuinyenyekesha Uajemi, endapo watabeba nguzo zito zaidi ya Uislamu, yaani Kumpwekesha Mwenyezi Mungu (Tawhid). Hivyo basi, tunawalinganieni kumfuate Kipenzi chetu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na uwe Maanswari wa Dini hii. Jitokezeni ili kuifanya Tawhid kuwa msingi wa dola na Khilafah. Kataeni mfumo huu wa kiuchumi wa Kiamerika na anzisheni mfumo mpya wa kiulimwengu juu ya msingi wa Uislamu. Toeni Nussrah kwa Hizb ut Tahrir ili iweze kukuongozeni katika mradi huu. Hivyo basi, itikieni!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu