Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  16 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444 / 43
M.  Jumanne, 04 Julai 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Umma wa Kiislamu kamwe "hautahalalisha mahusiano" ya ukiukaji matukufu. Badala yake, Khilafah Itaifunga Mikono na Ndimi Ovu Kunyamaza Kimya

(Imetafsiriwa)

Nchi za Magharibi zinaushambulia Uislamu bila kuchoka. Zinachafua heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa kuchora katuni, na kuchoma Quran Tukufu. Hii ni ili Waislamu wasiwe na hisia na "kuhalalisha mahusiano" na ukiukaji wa matukufu ya Uislamu. Msururu huu wa mashambulizi ulianza katika zama za hivi karibuni na Salman Rushdie na Taslima Nasrin. Uliendelea kwa kuungwa mkono vitendo vya uhasama kutoka kwa serikali za Ufaransa, Denmark, Norway, India na Marekani. Makafiri wanatumai Waislamu watarudi nyuma kutokana na kusimama kwa ajili ya ulinzi wa matukufu yao, na polepole kukubali utukufu wa uhuru wa Kimagharibi, kama Wakristo walivyofanya hapo awali. Walakini, ndoto yao hii itabaki bila kutimizwa. Umma wa Kiislamu utaendelea kufanya juhudi zozote katika kulinda matukufu yake. Zaidi ya hayo, Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni itaufunga kila mkono na ulimi muovu kunyamaza kimya, kama ilivyofanya kwa karne nyingi, katika historia yake tukufu.

Kila mfumo na hadhara zina mkusanyiko wake wa kipekee wa maadili. Kuenea na kukubalika kwa maadili haya ni ishara ya utawala na ushawishi wake, bila kujali uhalali wake. Maadili ya hadhara ya kiliberali wa Kimagharibi yanatokana na kupuuza matendo na nembo za kidini, na kuifunga dori ya dini. Kwa mujibu wao, kutafuta anasa za kimwili, muozo wa maadili, ndicho kipimo cha mafanikio. Magharibi haithamini sifa za kipekee, za lazima za mwanamke, na kusisitiza wanawake kuwachukua wanaume kama kipimo cha usawa, na kumbebesha mwanamke majukumu ya ziada ya wanamume. Aina zisizohesabika za upotovu wa kijinsia sasa zimekuwa kitambulisho mpya kwa hadhara ya Kimagharibi. Mambo yamefikia hatua ya ubadilishaji jinsia, ambapo wanaume wanajiona kama wanawake, au wanawake kama wanaume, yote kulingana na mapenzi na matakwa yao. Yote haya yanajengwa, bila shaka, kwa msingi wa uhuru huria, ambao unatetewa kama haki za kimsingi, za kilimwengu.

Hivyo basi, maafisa wa Kimagharibi walizungumza kwa sauti moja, wakisema hata waone kitendo fulani kuwa ni upotovu kiasi gani, hawatanyima uhuru wa kujieleza. Kwa hakika, kuchukia dini na kuweka mipaka katika utekelezaji wa dini ni mojawapo ya maadili msingi ya hadhara ya kiliberali ya kilimwengu. Viongozi na serikali za Kimagharibi sasa wanajaribu kuficha sura ya kuchukiza ya hadhara hii mbovu ya kiliberali ya Magharibi kutoka kwa Waislamu. Wanaonyesha kutoridhia kwao kunajisiwa kwa Quran Tukufu, hata wakati wao pia wanaona kuwa ni haki ya mtu anayefanya unajisi huo. Hata hivyo, sura ya kuchukiza ya Magharibi sasa inaonekana waziwazi, kwa jinsi ilivyo, kwa Ummah.

Katikati ya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Uislamu, ukweli mwingine umedhihirika kwa kila mtu. Katika mgongano huu wa mifumo na hadhara, watawala haramu wa ardhi za Waislamu ndio watetezi wa maadili ya Kimagharibi. Hamu yao pekee ni kuwadhibiti Waislamu, badala ya kuwaadhibu wale waliosubutu kuunga mkono kuchafuliwa kwa Uislamu, wakitoa mfano wao wa kuwazuia wengine wote katika siku zijazo. Kwa hivyo, kama ilivyo kawaida yao, mbele ya shinikizo la umma, shutma za kinafiki, za maneno zilitolewa. Hata hivyo, hakuna kabisa hatua yoyote ya ufanisi, ya kivitendo. Hali hii ya mambo itaendelea, kwani kudhalilishwa kwa Dini hakumo ndani ya "maslahi yoyote ya kitaifa." Hakika, hakuna dola yoyote ya kitaifa katika ardhi za Waislamu itakayosimama kutetea matukufu ya Uislamu.

Ibada na nembo ambazo ni sifa ya hadhara ya Kiislamu zitalindwa tu na dola yenye msingi wa Uislamu, Khilafah Rashida ya Kiislamu kwa Njia ya Utume. Heshima ya Rehema kwa wanadamu wote, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), itakuwa ndio mstari mwekundu wa Khilafah iliyobarikiwa. Kuheshimu utakatifu wa Qur'an Tukufu kutakuwa ndio mstari mwekundu wa Khilafah. Mashambulizi kama hayo yanazingatiwa kama tangazo la vita dhidi ya Khilafah. Khilafah haitakuwa na mahusiano ya kidiplomasia na dola zinazopiga vita Uislamu. Mali zao hazitalindwa, ilhali mali zao hazitaruhusiwa katika anga zetu, ardhi zetu au bahari zetu. Kila meli ya mafuta na mizigo inayopeperusha bendera ya Uswidi inayopitia Mlango-Bahari wa Malacca, Mlango-Bahari wa Hormuz au Mkondo wa Suez itakamatwa, kama vile Marekani ilivyokamata meli za mafuta na mizigo za Iran na Korea Kaskazini.

Maadamu dola hizi za kitaifa zipo kwenye ardhi za Waislamu, mashambulizi kama hayo ya kuumiza moyo yataendelea. Magharibi imeridhika kikamilifu na utiifu wa watawala wa Waislamu. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume, itakayosimamishwa hivi karibuni inshaaAllah, ndiyo itakayofunga kila ulimi na mkono muovu kunyamaza kimya. Kwa hiyo, enyi majeshi ya Umma wa Kiislamu! Jitokezeni, wang'oeni watumwa hawa wa Magharibi na mutoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ili hatimaye muhamasishwe kumhami Mtume (saw) na Kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt). ) Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran Tukufu,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ]

“Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.” [Surah Al-Hujraat, 49:02].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu