Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 18 Rajab 1446 | Na: 1446 / 25 |
M. Jumamosi, 18 Januari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Baada ya Kutazama Tu Mauaji ya Kinyama kwa Siku 467, Watawala wa Pakistan Sasa Wanasherehekea Usitishaji Vita
(Imetafsiriwa)
“Watu wa Pakistan wanaungana nami katika kukaribisha tangazo la usitishaji mapigano uliosubiriwa kwa muda mrefu nchini Palestina,” Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, aliandika kwenye ukurasa wa Twitter mnamo tarehe 16 Januari 2025. Hata hivyo, ukweli ni kwamba, kwa zaidi ya mwaka mmoja, utawala wa Munir-Sharif umekuwa ukitizama tu vifo na uharibifu huko Gaza, ambako mauaji ya halaiki ambayo hayajawahi kuonekana yalitokea, na walionusurika sasa kuganda kwa baridi hadi kufa. Walikuwa wakiyatazama haya yote, kana kwamba Pakistan haina jeshi kubwa zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu, na kana kwamba jeshi hilo nimeundwa kwa watu wasio na uwezo, dhaifu, waoga na vilema, kwa hivyo watawala hawawezi kufanya chochote kujibu ukatili huu isipokuwa kulaani, kushutumu na kupinga. Hata hivyo, tabia ya watawala ilikuwa kiasa kwamba hawakufanya hata hivyo. Kutia chumvi kwenye kidonda kikubwa, Shehbaz Sharif alitoa wito wa kuwepo kwa suluhisho la dola mbili, ambao ni mpango wa Marekani wa kusalimisha sehemu kubwa ya Palestina kwa umbile la Kiyahudi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awapige vitana watawala hawa. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[مَا لَکُمۡ ٝ کَیۡفَ تَحۡکُمُوۡنَ] “Mna nini? Mnahukumu vipi?” [Surah Al-Qalam, 68:36].
Wakati vita dhidi ya Gaza vimetayarisha kaburi kwa fahamu ya hadhara ya Kimagharibi, pia vimepomoa barakoa za watawala wote wa Waislamu. Shehbaz Sharif aliandikwa tweet, “Thamini juhudi bila kuchoka za Qatar, Saudi Arabia, Marekani, Misri na washirika wengine wa kimataifa ambao walifanya kazi kwa bidii ili kufanikisha makubaliano haya muhimu.” Je, watawala hawa wanazungumzia juhudi gani? Watawala hawa wamelipatia umbile la Kiyahudi njia za ardhini, anga na baharini kwa zaidi ya mwaka mmoja, wakiwapa silaha muhimu na ujasusi, huku likiua zaidi ya watu 50,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Ukweli ni kwamba watawala hawa vibaraka wanaisaliti Al-Masjid Al-Aqsa, Kibla chetu cha kwanza, na viunga vyake yaliyobarikiwa. Hakika, jukwaa limewekwa la kuwazika watawala hawa wa vibaraka katika kaburi lilelile ambalo hadhara ya kimagharibi itazikwa!
Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Watu wasio na hatia wa Gaza wamekuonyesheni kwamba ni kwa nguvu ya Iman pekee ndiyo iliyolizuia umbile la Kiyahudi kufikia malengo yake yoyote ya kijeshi. Silaha zote za dola za ulimwengu zilikuwa bure mbele ya Iman ya watu wa Gaza, ambao walifanya tawwakul (kumtegemea) Mwenyezi Mungu (swt) Peke Yake. Tayari mulishaiona Marekani ikifedheheshwa nchini Afghanistan, ambapo muungano wa mataifa arubaini na mbili ulilazimishwa kushindwa kwa kufedheheshwa, na wanamgambo dhaifu wenye idadi ya elfu chache, ambao walipigana Jihad huku wakifanya tawwakul kwa Mwenyezi Mungu (swt). Basi itakuwaje mutakapowang'oa watawala hawa na kusimamisha Khilafah Rashida, kuunganisha Pakistan, Afghanistan, Asia ya Kati na Mashariki ya Kati na kuliondoa umbile la Kiyahudi? Je, kisasi cha mashahidi hawa elfu hamsini bado hakiko shingoni mwenu? Ikiwa pia mutafanya tawwakul (kumtegemea) Mwenyezi mungu (swt) mithili ya Waislamu wa Gaza, basi ni nguvu gani katika ardhi hii inayoweza kukuzuieni kuliangamiza umbile hili la Kiyahudi?
Amesema Mwenyezi Mungu (swt): [وَمَنْ یَّتَوَكَّلْ عَلَی اللّٰهِ فَهُوَ حَسْبُهٗ] “Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha.” [Surah At-Talaq, 65:3].
Usaliti wa uongozi wa kijeshi na kisiasa uko wazi kwenu. Aidha, kuporomoka kwa nchi za Magharibi, na uhalisia wa utawala dhalimu wa mfumo wa sasa wa dunia, ni dhahiri. Sasa ni kiungo cha mwisho tu katika mlolongo wa mabadiliko kinachosalia. Huko ndiko kufanya kwenu tawwakul (kumtegemea) Mwenyezi Mungu (swt) huku mkitoa Nusrah yenu kwa uongozi ulioandaliwa kikamilifu, Hizb ut Tahrir, kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida. Hizb ut Tahrir ina zaidi ya miaka sabiini ya maandalizi ya dola ya Khilafah, na ufahamu kamili wa hali ya kisiasa ya kimataifa. Hii ni hatua ya mwisho kabla ya kuanza mwamko wa Umma wa Kiislamu, kukombolewa ardhi za Waislamu kutoka kwa ukoloni, na kusambaratika mfumo dhalimu wa dunia wa Marekani. Hii ndiyo njia ya kivitendo ya misheni ambayo Ummah umenyanyuliwa mbele ya wanadamu katika ulimwengu huu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ]
“Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [Surah At-Tawbah 9:33].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |