Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
| H. 25 Jumada I 1447 | Na: 14 / 1447 |
| M. Jumapili, 16 Novemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pakistan, Nchi Safi, Haiwakaribishi Wala Haiwasalimu Vizazi vya Khiyana vya Wasaliti
(Imetafsiriwa)
Baada ya kimya cha wafu makaburini cha serikali za vibaraka zinazobebesha mzigo ardhi za Waislamu, kuhusu mauaji ya Kiyahudi mjini Gaza kwa zaidi ya miaka miwili, vibaraka wa Amerika na Uingereza, washirika wa Mayahudi, walianza kuchukua hatua na kuwa wachangamfu katika kutekeleza mpango wa Trump wa kufilisi kile kilichobaki cha upinzani huko Palestina, kukandamiza na kuua watu mjini Gaza, na kubomoa kile ambacho Mayahudi hawakubomoa cha mawe. “Jenerali anayependwa zaidi wa Trump” Asim Munir alitembelea Jordan mnamo 26 Oktoba, na kwa badali yake, mnamo 16 Novemba 2025, Mfalme Abdullah II bin Al-Hussein, Mfalme wa Ufalme wa Hashimiya wa Jordan na Kamanda Mkuu wa Vikosi vya Wanajeshi wa Jordan, alitembelea Pakistan, akifuatana na binti yake Salma binti Abdullah II bin Al-Hussein, na ujumbe wa maafisa wa kiraia na kijeshi wa Jordan. Walitembelea Kampuni ya Suluhisho la Viwanda na Ulinzi Duniani, ambapo walipokelewa katika maeneo ya kijeshi na Asim Munir, Mkuu wa Wafanyikazi wa Jeshi, na maafisa kadhaa wakuu. Wakati wa ziara hiyo, Mfalme alipokea maelezo mafupi kuhusu muundo wa kampuni hiyo, uwezo, na vitengo vya bidhaa. Mkutano huo uliakisi maendeleo ya Pakistan katika uzalishaji wa ulinzi wa ndani na uvumbuzi wa kiteknolojia. Baadaye, Mfalme Abdullah wa Pili alitembelea vituo vya kulenga shabaha kwenye vilima, ambapo Waziri Mkuu Muhammad Shehbaz Sharif pia alihudhuria hfla hiyo.
Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan, tunalaani ziara hii na kuthibitisha yafuatayo;
Kwanza: Hakuna makaribisho au salamu kwa Mfalme Abdullah wa Pili, mlinzi wa kwanza wa umbile la Kiyahudi katika eneo hilo, na ziara hii haiheshimu Pakistan, Ardhi Safi. Abdullah wa Pili alikuwa wa kwanza kula njama dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na watu wake katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ya umwagaji damu mjini Gaza. Dori yake ilizidi usaliti wa watu wa Gaza kwa kuzuia jeshi la Jordan kuwanusuru watu wake, kuwakandamiza wote walioonyesha kulaani mauaji hayo, na kwenda zaidi ya hapo kwa kushirikiana na dola ya Kiyahudi kuwaua watu wetu mjini Gaza, kama ilivyofichuliwa hivi karibuni na vyombo vya habari, ikithibitisha kwamba Jordan ilikuwa miongoni mwa nchi sita zinazoshiriki katika kuwaua watu wa Gaza, pamoja na umbile la Kiyahudi, pamoja na mahitaji na vifaa vinavyopita Jordan na Saudi Arabia, kutoka Imarati na kwengineko. Je, msaliti huyu alipaswa kukaribishwa kwa zulia jekundu nchini Pakistan, Ardhi Safi?! Watu wa Pakistan lazima waisafishe ardhi ambayo mfalme msaliti alitembea kwa maji mara saba, ili ardhi irudi kwenye usafi wake.
Pili: Je, ukweli kuhusu mfalme huyu umekwepa uongozi wa kijeshi nchini Pakistan?! Je, hawajui kwamba yeye ni mzao wa familia ya kisaliti iliyotengenezwa na Waingereza waovu?! Babu yake mkubwa Hussein bin Ali, Sharif wa Makka, aliidunga kisu Khilafah ya Uthmani mgongoni ndani ya Hijaz, baada ya kushirikiana na Waingereza, pamoja na mwanawe Abdullah I, na wote wawili walikuwa sehemu ya kuanguka kwa dola ya Khilafah?! Je, hawajui kwamba baba yake mfalme huyu, Mfalme Hussein, alikuwa mpelelezi wa Moshe Dayan na Golda Meir, akisambaza habari kuhusu nchi zinazozunguka umbile la Kiyahudi baada ya ziara zake Misri, Syria, na zengine?! Je, hawajui kwamba mfalme huyu pia atawasilisha yote aliyoyashuhudia nchini Pakistan kwa ndugu zake Mayahudi katika dola yao kama baba yake alivyofanya hapo awali?! Je, uongozi wa kijeshi haujui kuhusu dori la Binti Mfalme Salma, kama rubani katika Jeshi la Anga la Jordan, katika kuangusha droni kadhaa za Iran zilizoingia anga ya Jordan, zikiwa njiani kuelekea dola ya Kiyahudi mwaka jana?!
Tatu: Tunajua ukaribu huu kati ya vibaraka wa Marekani na Mayahudi si kwa maslahi ya Uislamu na Waislamu. Hawajawahi kukusanyika kuunga mkono lengo lolote la Kiislamu; mikutano yao na ukaribu wao hutumika tu kudhuru Umma huu, kula njama dhidi ya masuala yake, na kutekeleza mipango ya mabwana zao jijini Washington na London. Kinachowaunganisha vibaraka hawa leo ni kutekeleza mpango wa Trump katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, kufanya kazi chafu inayofanywa na umbile la Kiyahudi nchini Palestina, kwa kuunda vikosi vya kijeshi kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu zilizo karibu na mbali, ikiwemo Jordan na Pakistan, na kuwa na vikosi hivi kuwakandamiza watu wa Palestina, na kuwalinda Mayahudi miongoni mwao, kulingana na mpango wa bwana wao Trump. Kwa hivyo, watu wa Pakistan lazima wachukue msimamo mkali dhidi ya vibaraka hawa na kuwazuia kutuma vikosi vya mamluki kulinda dola ya Kiyahudi, na kulitaka Jeshi lenye ikhlasi la Pakistan liwapindue makamanda wao wasaliti na kuelekeza vikosi vya jeshi hilo kuelekea Ardhi Iliyobarikiwa ili kuikomboa na kuisafisha kutokana na unajisi wa Kiyahudi.
Enyi Maafisa Wanyofu katika Jeshi la Pakistan! Usaliti wa vibaraka hawa umefika kingi, jambo ambalo hakuna akili timamu au moyo wa ushujaa timamu unaoweza kustahimili. Usaliti wa makamanda wenu wa kijeshi, ambao hawakukataa njama yoyote ya Amerika, iwe ni nchini Afghanistan chini ya kivuli cha “Vita dhidi ya Ugaidi,” au kujisalimisha kwa Kashmir, au kuwa na ukaribu na adui wa Uislamu na Waislamu, Mabaniani, sasa munawaona wakitii amri ya Trump katika kula njama dhidi ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na watu wake. Ni lini roho ya mujahid, ambaye hakubali ukiukaji wowote wa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt), itainuka ndani yenu? Je, mujahid anawezaje kuwakubali watu kama Mnafiki, Ubdullah ibn Ubay ibn Salool kama makamanda wake?! Sisi, katika Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan, tunatoa wito wa nusra yenu ya kijeshi kwa Uislamu na Waislamu, sio ulinzi wenu kwa Mayahudi chini ya uongozi ambao ni wasaliti kwa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), na waumini. Tunatoa wito kwa nusra yenu ya kijeshi katika kusimamisha Khilafah Rashida nchini Pakistan, Ardhi Safi, ili kuongoza majeshi katika ukombozi (tahrir) wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Al-Masjid Al-Aqsa, kutoandamana kuwaua Waislamu huko, na kuwapa nguvu Mayahudi, kama makamanda wenu na kizazi cha hila cha Mfalme Abdullah hila kinavyotafuta. Kimya chenu kuhusu viongozi wenu wa khiyana katika miongo iliyopita, na hasa katika miaka miwili iliyopita, kuhusu kuwatelekeza kwao watu wa Palestina, kinahitaji toba ya dhati ikifuatiwa na hatua inayolingana na ukubwa wa usaliti wenu na utelekezaji wenu siku ya vita, ambao mliufanya kwa kushindwa kuwanusuru watu wetu mjini Gaza. Kwa hivyo njooni musimame na Uislamu na Waislamu kwa kutoa nusra yenu ya kijeshi kwa Hizb ut Tahrir sasa, amali inayompendeza Mwenyezi Mungu (swt) na kufidia uzembe wenu katika kuwanusuru watu wenu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawba 38-39]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |



