Alhamisi, 24 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  11 Muharram 1444 Na: BN/S 1444 / 01
M.  Jumanne, 09 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Umbile la Kiyahudi ni Jinai Kuu Iliyojadidishwa

Inaweza tu Kumalizika kupitia Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Kutokomeza Mizizi na Maovu Yake

(Imetafsiriwa)

Katika uhalifu wa kikatili na wa khiyana, na uchokozi mpya wa kioga, vikosi vya uvamizi viliwaua vijana 3, akiwemo Mujahid Ibrahim Al-Nabulsi, alfajiri ya leo, Jumanne, na wengine 40 walijeruhiwa, watano kati yao walielezewa kuwa mahututi, wakati wa uvamizi wao wa mji wa Nablus.

Uhalifu huu, na mwengine mithili yake, umekuwa ni thibitisho zito, kwamba jinai kubwa zaidi na mama wa jinai ni kuwepo kwa umbile hili lenye kuleta ufisadi ardhini, na kwamba hakuna mipaka na hakuna mwisho wa uhalifu wake isipokuwa kwa kuliangamiza na kuling'oa kutoka kwenye mizizi yake. Hii ni kwa sababu ni umbile lililoasisiwa tangu siku ya kwanza juu ya uhalifu na umwagaji damu na bado linamwaga damu hadi saa hii. Halijaacha kwa zaidi ya miaka kadhaa. Usalama wake unajengwa juu ya mauaji ya watu wa Palestina. Bali mkono wa ufisadi na uchokozi wake unazichafua biladi zote za Waislamu, kupitia kuua, na kulipua mabomu, katika uadui wa wazi na jinai dhidi ya Ummah mzima.

Kuendelea kwa umbile la Kiyahudi katika mwenendo wake wa uhalifu kwa miongo kadhaa, kunathibitisha pia kwamba umbile hili halipingwi na kile kiitwacho sheria za kimataifa, wala halikomeshwi na upatanishi, wala halijawahi kukomeshwa kupitia usawazishaji wa aibu unaofanywa na tawala za usaliti. Bali ulafi wake katika kumwaga damu za watu wa Palestina haukomeshwi kwa kuzingatia lolote katika haya. Ni kana kwamba linaona kuwa uwepo wao tu katika ardhi yao unatishia usalama na uwepo wake.

Kwa hiyo, kuendelea kutafuta njia za kukabiliana na umbile hili nyakuzi hakumaanishi chochote ila ni kuendelea kwa uhalifu wake. Hakuna ushahidi mkubwa zaidi kwa hilo kama uhalifu wa leo huko Nablus baada ya uhalifu wa jana katika Ukanda wa Gaza. Miito ya ile iitwayo jumuiya ya kimataifa haikuzuia kumwaga damu ya watu wa Palestina, na Umoja wa Mataifa kamwe haukukomesha kabisa jinai yoyote, hata jinai moja, na haukumhisabu katili huyo kwa jinai hizo zake. Wanawezaje kutarajiwa basi ilhali wao ndio wafadhili, wafuasi na washirika wake, bali wao ndio waliolipanda katika ardhi zetu na wako makini kwa ajili ya usalama wake?!

Kadhalika, kufuata mbinu za kile ambacho kimekuja kujulikana kama waamuzi wa njama na tawala za usaliti, hakukulikomesha umbile hili, na kwa nini zifaanye hivyo, wakati wao ndio washirika katika uhalifu wake; kupitia kuufinika na kuratibu pamoja nalo katika uhalifu, kama ilivyo dori ya mamlaka ya uhaini. Dori yao ni kuelekeza ncha za kila uchokozi linaoufanya. Kila mtu ameona dori yao ya kushiriki, kama tulivyokwisha kutaja katika uvamizi wa Gaza siku chache zilizopita.

“Ama kuhusu kundi la watawala vibaraka, ni kundi linalomsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume wake, Waislamu na damu zao. Hawaguswi na ulinzi wa Uislamu wala kiburi cha wanadamu, na wao si chochote zaidi ya zana za khiyana. Dori yao katika kila jinai inayotendwa na maadui zetu ni kudhibiti athari zake na kukaza mshiko wao juu ya Waislamu ili kuwaweka pingu na kumeza udhalilifu. Jukumu lao baada ya kila uhalifu ni kuosha damu na kudhibiti matokeo kutokana na kujali kwao umbile la Kiyahudi, ambalo wana shauku juu ya ulinzi wake kama wanavyojishughulisha wenyewe. Wao ni watawala wasaliti, bali ni watumwa wa maadui zetu ambao hawana lolote ila kutekeleza amri za mabwana zao huko Washington na London, na dori yao imejulikana na kurudiwa mara kwa mara baada ya kila uhalifu unaofanywa na umbile la Kiyahudi; dori ya mshirika katika kunyamaza na kuficha na njama na uratibu wa usalama,” hadi suala hilo kufikia kwamba Waziri wa Vita wa umbile la Kiyahudi alizishukuru tawala za Misri na Qatar kwa yale waliyoyafanya katika vita vya hivi majuzi dhidi ya Gaza. Wao ni kama umbile la Kiyahudi kwa kuwa wanahamu tu ya kuinyamazisha kila nafsi inayo asi katika watu wa Palestina wanaowafedhehesha, kufichua woga wao, na kufichua uzembe wao.

Uhalifu wa mara kwa mara wa umbile la Kiyahudi dhidi ya Palestina na watu wake na matukufu yake unatosha kuwa cheche ya kuwakisha Umma wa Kiislamu. Imani ya Uislamu ndani ya nyoyo za watoto wake inatosha kuwa dhamira ya wao kuikomboa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa. Yale ambayo Ummah unamiliki ya nguvu, majeshi, utajiri na watu yanatosha kuliangamiza umbile hili ovu kuanzia asubuhi moja hadi Alasiri yake, na kuikomboa kutokana nalo na ufisadi wake milele. Hakuna kinachozuia Ummah kutokana na hili isipokuwa watawala hawa, mawakala waoga ambao viti vyao vya enzi ni hafifu mithili ya nyumba ya buibui na viti vyao (vya utawala) vimeoza na vinakadiriwa kuanguka. Hivyo basi, kuiregesha kadhia ya Palestina kuwa kadhia ya Umma wa Kiislamu, na kuirudisha kwenye mikono yake imekuwa jambo lisiloepukika. Pia, jambo lisiloepukika ni kuilingania kwa wito unaoisukuma imani yake na Uislamu na kuihamasisha kuinuka tena.

[وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

“Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.” [Al-Anfal: 10]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu