Alhamisi, 28 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  21 Jumada II 1447 Na: BN/S 1447 / 12
M.  Ijumaa, 12 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mashirika ya Mamlaka ya Palestina na Majambazi Wao Yamkamata Mwanafunzi Saif Abu Al-Hawa
(Imetafsiriwa)

Mamlaka ya Palestina (PA), ambayo ni tiifu kwa Mayahudi, ilimkamata mwanafunzi Saif Abu al-Hawa alipokuwa akiondoka Chuo Kikuu cha Bethlehem mnamo Jumanne, 9 Disemba 2025. Kwa kutumia majambazi wasaliti na kisha kikosi kutoka kwa vyombo vya usalama vya PA, katika tukio linaloakisi mbinu za ujambazi na vitisho vya PA dhidi ya watu wa Palestina, hawazuiwi na Dini wala sheria, wala hata utakatifu wa chuo kikuu ambacho Saif alitoka. Kisha alifikishwa mbele ya mahakama mnamo Alhamisi, ambapo jaji aliongeza kifungo chake kwa siku kumi na tano, licha ya kwamba hakufanya uhalifu wowote. Kosa lake pekee lilikuwa kutaja Hukm Shari’ kwamba Waislamu hawaruhusiwi kushiriki katika sherehe za sikukuu za Kikristo!

Je, huyu amefanya kosa gani ambalo limesababisha ghasia kubwa kutoka kwa Mamlaka ya Palestina? Je, Saif aliiuza Palestina mithili ya PLO ilivyofanya? Je, Saif alishiriki katika uratibu wa usalama pamoja na Mayahudi, akiwaua watu wa Palestina kwa ajili yao, kama vikosi vya usalama vya Mamlaka ya Palestina vilivyofanya? Je, Saif alisaliti ardhi kwa Mayahudi, kama maafisa wafisadi wa PA walivyofanya? Je, Seif alikataa posho zilizotolewa kwa familia za mashahidi na wafungwa, au kuwatukana na kuwalaani wapiganaji wa upinzani, kama mkuu wa PA alivyofanya? Je, Seif aliruhusu mashirika ya wanawake katika nchi yetu kushambulia Dini na maadili yetu na kukosoa hukmu za Kiislamu? Je, Seif aliwajumuisha wanawake katika kuandika katiba ya mpito ili kufurahisha Magharibi na Mashariki? Na kadhalika na kadhalika...? Nani anapaswa kukamatwa? Nani anapaswa kufikishwa mahakamani?

Laiti Mamlaka ya Palestina na vyombo vyake vya usalama vingeonyesha ari hiyo wakati Mayahudi waliponajisi Msikiti wa Al-Aqsa mchana na usiku—unajisi ambao haukuisukuma hata PA kusitisha ushirikiano wake na Mayahudi. Laiti PA ingeonyesha ari hiyo wakati Msikiti wa Ibrahimi ulipokuwa ukibadilishwa kuwa sinagogi. Laiti Mamlaka hiyo ingeonyesha bidii hiyo wakati watu wa Gaza walipokuwa wakitendewa ukatili na Mayahudi mchana na usiku. Laiti PA ingeonyesha ari hiyo wakati kambi za wakimbizi katika Ukingo wa Magharibi zilipokuwa zikiharibiwa na wakaazi wake kufukuzwa chini ya pua za PA na vikosi vyake vya usalama.

Laiti vikosi vya usalama vya PA vingeonyesha ari kama hiyo wakati walowezi walipokuwa wakishambulia vijiji na miji: Kuua watu, kung'oa miti, kuchinja mifugo, na kuchoma ardhi ya kijani kibichi. Yote haya yalikumbana na kimya kama kile cha kaburi, isipokuwa kulaani au wito wa upinzani—wito ambao PA inaonekana kutojua kabisa. Nyinyi ni “simba” wa aina gani linapokuja suala la watu wa Palestina na vijana wake, kuwashambulia kwa dhulma? Na nyinyi ni kondoo wa aina gani linapokuja suala la kuwalinda watu wa Palestina, wanawake wake, na watoto wake?!

Ingawa utekaji nyara wa Seif mbele ya Chuo Kikuu cha Bethlehem ni uhalifu ambao Mamlaka ya Palestina, vyombo vyake vya usalama, majambazi, na wahuni wanawajibika, hii haiondoi chuo kikuu jukumu lake, kwani mmoja wa wanafunzi wake alitekwa nyara kizingitini mwake. Chuo kikuu kina jukumu la kumtetea na kusimama dhidi ya PA, ambayo inaingilia haki za watu wa Palestina na vyuo vikuu vyao. Haikubaliki kwa chuo kikuu kukaa kimya, na hivyo kukuza mazingira ya uvamizi dhidi ya wanafunzi wa chuo kikuu.

Kwa kumalizia, mamlaka ambayo haina chochote cha kuwapa Mayahudi, wanaokanyaga hadhi yake huku na huko, na ambayo imegubikwa na udhalilifu hadi ifunikwe kabisa, na inazama katika unyenyekevu kwa Mayahudi na Magharibi hadi masikioni mwake, itakuwa bora zaidi, pamoja na vyombo vyake vya usalama na wasaidizi wake, ikiwa ingeinua mikono yake kutoka kwa watu wa Palestina na wabebaji wa ulinganizi huko. Kwani wale ambao kiunganishi chao ni kamba ya Mwenyezi Mungu si sawa na wale ambao mafungamano yao yamefungwa kwa idhini ya kafiri na wanakaribia kuyakata, lakini watawajibishwa vikali na Ummah katika ulimwengu huu, na kisha kurudi kwa Mola wao kupata adhabu kali.

[وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَاناً وَإِثْماً مُبِيناً]

“Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.” [Al-Ahzab 33:58]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 0598819100
www.pal-tahrir.info
E-Mail: info@pal-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu