Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Rabi' I 1445 Na: HTS 1445 / 03
M.  Alhamisi, 21 Septemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Dori ya Wanawake ni Kubwa Zaidi kuliko Kupigana katika Vita Visivyo na Maana!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Septemba 20, 2023, Chaneli ya Al Jazeera ilipeperusha picha kutoka katika sherehe ya kuhitimu ya kundi la kwanza la wanawake waliohamasishwa wilayani Marawi katika jimbo la kaskazini, kuitikia wito wa Mkuu wa Majeshi, Luteni Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, kuwahamasisha watu kupigana pamoja na jeshi!

Enyi, muliohamasishwa kujiunga na vita ambavyo kamanda wa jeshi la Sudan alitangaza kutoka siku ya kwanza kuwa upuuzi. Je! Kushiriki kwenu katika vita hivi kutaleta athari ambayo wanaume wenye nguvu, imara, walioundwa kubeba ngao, kuendesha magari ya kivita, na kukabiliana na hatari zote, hawakuweza kuleta?! Je! Kushiriki kwenu katika vita ambavyo Muislamu anamuua ndugu yake Muislamu kuna hoja ya kisheria ambayo itakuokoeni kutokana na hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt), ambaye anasema:

[وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisa 4:93].

Enyi Mliohamasishwa: Ni njama kuhamasisha watu wa Sudan kupigania viti vya serikali vyenye miguu mibovu, na kukamilisha mpango wa kugawa mabaki ya Sudan. Hapana shaka kuwa Jeshi halihitaji kuhamasishwa, lakini badala yake linahitaji dola ambayo ina uamuzi wake wenyewe wa kisiasa kumaliza vita hivi. Kwa hivyo, uhamasishaji sio hatua ya kijeshi, lakini ni hatua ya kisiasa iliyokusudiwa kuwapanga watu wa Sudan nyuma ya Burhan ili kumpa kasi ya kutekeleza mpango wa bwana wake Marekani katika nchi yetu.

Jeshi la Sudan ni la 77 duniani katika orodha ya majeshi yenye nguvu zaidi ulimwenguni, kati ya nchi 145. Tuliona na kusikia wanajeshi wakilia kwa maumivu kwa sababu ya kucheleweshwa kutatua vita hivi na kuakhirishwa mwisho wake hadi kitoweo chenye sumu cha Marekani kikapikwa kupitia mazungumzo ya Jeddah.

Uislamu, kwa upande wa mapigano halali, haukuwalazimisha wanawake kupigana, na umefunga ushiriki wao vitani katika kutoa msaada wa vifaa na huduma tu. Huwatibu majeruhi, kuleta chakula, na kadhalika. Hakuna hata Sahabiya (ra) mmoja aliyefundishwa kupigana, licha ya hitaji kubwa la Mtume (saw) kwa mtu kupigana. Msihadaiwe kupigana vita kuegemea ushindi wa Marekani na ushawishi wake, ambayo inatumikiwa na viongozi wa jeshi, dhidi ya ushawishi wa Ulaya, ambayo inawakilishwa na raia na wale walio karibu nao.

Dori ambayo wanawake lazima waichukue ni kubeba ulinganizi wa kurudisha tena maisha kamili ya Kiislamu, na mfano wake unaong’aa ni Masahabiyat (ra) ambao walikuwa ni mojawapo ya sababu kubwa ya Ummah huu kuchukua dori yake, na dori yao, na mapambano ya kisiasa, mfano wao ni Umm Amara na Umm Mani' katika Bay’ah ya Aqaba. Katika vita, Rufaida Al-Aslamia na kikundi cha wafanyikazi wa kujitolea wa kike huenda kwa Mtume (saw) wakiomba ruhusa ya kushiriki katika kuwatibu waliojeruhiwa, na katika mashauriano ya kisiasa, Umm al-Mu'minin, Umm Salamah, na wengine wengi kwenye viwanja kuliko kupigana. Wanawake hutofautisha nafasi yao katika jamii na dori yao maishani kwa kurudi kwenye maisha yao ya zamani kama Waislamu, wenye ufahamu, wanaojitolea katika vifungu vya wazi vya sharia', sio kuhadaiwa na miito au njama ambazo zinadhoofisha Ummah na kuuchana vipande vipande. Badala yake, wanafanya kazi kwa ajili ya mabadiliko ili Mwenyezi Mungu aturuzuku ushindi na tamkini katika Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu