Jumapili, 27 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  25 Shawwal 1445 Na: HTS 1445 / 32
M.  Jumamosi, 04 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Nazir (Kiongozi Mkuu) wa Makabila ya Nuba nchini Sudan Apokea Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan katika Makaazi yake mjini Port Sudan
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, ulioongozwa na Ustadh Yaqoub Ibrahim, na mwanachama: Ustadh Mwanasheria Ahmad Abkar, Mjumbe wa Baraza la Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, na Ustadh Suleiman Al-Dasis, na Ustadh Daoud Abdullah, wanachama wa Hizb ut Tahrir, walimtembelea, Bw. Azraq Tilfone, Nazir (Kiongozi Mkuu) wa Makabila ya Nuba nchini Sudan, katika makaazi yake mjini Port Sudan mnamo siku ya Ijumaa, 24 Shawwal 1445 H sawia na 3/5/2024 M.

Ujumbe huo ulieleza madhumuni ya ziara hiyo; kwamba ni kuitambulisha Hizb ut Tahrir na kadhia nyeti ambayo hizb inaifanyia kazi, ambayo ni kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Nazir (Kiongozi Mkuu) aliupokea ujumbe wa Hizb ut Tahrir kwa moyo mkunjufu, na akasikiliza ruwaza ya hizb ya kutoka katika migogoro inayoikumba nchi, kwani ni hukmu za Shariah ambazo Waislamu wanapaswa kuzitekeleza ndani ya Dola ya Khilafah. Nazir alisema kuwa suala la Uislamu ni mstari mwekundu usioweza kuvukwa, na kwamba anaunga mkono Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu