Jumatatu, 06 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/06/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  1 Dhu al-Hijjah 1446 Na: HTS 1446 / 64
M.  Jumatano, 28 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ugonjwa wa Kipindupindu Waangamiza Sudan, na Serikali, kwa Uzembe wake, Inaomba Msaada kwa Mashirika ya Kimataifa!
(Imetafsiriwa)

Shirika la Afya Duniani (WHO) limefichua kuwa takriban wagonjwa 60,000 wa kipindupindu wamerekodiwa nchini Sudan, na kusababisha vifo vya zaidi ya 1640, likionya madhara ya kuporomoka kwa mfumo wa afya nchini humu. Ufichuzi huu unakuja wakati kipindupindu kikienea kwa kasi katika Jimbo la Khartoum, ambapo maambukizi mapya yanazidi 90% ya jumla ya nchi, haswa huko Karari, Omdurman, na Ombada. Mnamo Jumanne, 27/5/2025, Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza kurekodi kesi 2729, pamoja na vifo 172, katika wiki moja. Waziri wa Afya wa Sudan Dkt. Haitham Mohamed Ibrahim alisema kuwa kuenea kwa kipindupindu jijini Khartoum kunatokana na kuzorota kwa hali ya mazingira na matatizo ya vyanzo vya maji ya kunywa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu mpya Kamil Idriss anatoa wito kwa WHO, huku ripoti za vyombo vya habari zikisema kuwa anawasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ili kujadili kusaidia juhudi za kudhibiti kipindupindu nchini humu.

Kinachotokea katika sekta ya afya nchini Sudan ni kufeli kwa wazi kwa upande wa serikali, ambayo imekuwa na ikiendelea kukabiliana na janga la kipindupindu kwa uzembe wa wazi. Katika wakati ambapo suala hilo linahitaji uharaka, Waziri Mkuu anatafuta msaada kutoka kwa Shirika la Afya Duniani, ambalo, ikiwa litachukua hatua hiyo, itafanyika tu baada ya janga hilo kuenea na kupoteza maisha. Kwa upande wa Waziri wa Afya aliyepewa amana ya kushughulikia suala hilo, anatuzungumzia sababu zake bila kutimiza wajibu wake wa kutokomeza janga hilo, jambo ambalo ni rahisi kulifanya ikiwa serikali ina nia ya dhati juu ya hilo.

Watawala hawa waliochukua mambo yetu na kutuharibia, hawajali kabisa ustawi wa watu, iwe wanaugua, wana njaa au wanakufa. Janga hili la kipindupindu lingeweza kuepukika ikiwa serikali ingeshughulikia usalama wa watu kwa uwajibikaji. Sio vigumu kutoa maji safi ya kunywa, kisha kuwatenga na kuwatibu walioambukizwa. Hii ni kazi rahisi na ya gharama nafuu. Matibabu hayaendi zaidi ya kutoa maji kupitia mishipa, ambalo ndilo jambo rahisi zaidi linaloweza kutolewa. Hata hivyo, serikali haikutoa hata maji haya, na yanapopatikana, ni ghali mno na masikini hawezi kuyamudu.

Tawala hizi fisadi, zilizotungwa na wanadamu hazistahili kusimamia mambo ya watu. Waislamu nchini Sudan lazima wajitahidi kuanzisha mfumo unaojali mambo yao na kujali afya zao, usalama na utulivu wa akili. Hili litatokea tu chini ya hukmu za Uislamu, ambazo zinamlazimu mtawala kuchunga mambo ya watu. Mtume (saw) amesema:

«فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam (mtawala) wa watu ni mchungaji na ataulizwa kuhusu raia wake” Pia alisema:

«مَنْ أَصْبَحَ مِنْكُمْ آمِناً فِي سِرْبِهِ مُعَافًى فِي جَسَدِهِ عِنْدَهُ قُوتُ يَوْمِهِ فَكَأَنَّمَا حِيزَتْ لَهُ الدُّنْيَا»

“Yeyote miongoni mwenu anayepambaukiwa akiwa na usalama wa familia na afya njema, na kuwa na riziki ya siku yake ni kama anamiliki dunia nzima.”

Basi jitokezeni, enyi watu wa Sudan, enyi Waislamu, tusimamishe dola inayochunga mambo, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. [Al-Anfal: 24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah of Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu