Jumatatu, 17 Safar 1447 | 2025/08/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  13 Safar 1447 Na: 1447 / 02
M.  Alhamisi, 07 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mbwa Mwitu Hapaswi Kulaumiwa kwa Uvamizi wake ikiwa Mchungaji ndiye Adui wa Kondoo
(Imetafsiriwa)

Watoto watatu walifariki katika Jimbo la Khartoum baada ya kupokea dozi ya chanjo ya ukambi. Wizara ya Afya imefungua uchunguzi kuhusu dhurufu za vifo vyao. Sudan Tribune iligundua kuwa watoto wawili walikufa ndani ya saa moja baada ya kupokea chanjo ya ukambi, huku mtoto wa tatu akifa siku tisa baada ya kusaidiwa kupumua katika Hospitali ya Al-Balak mjini Omdurman. (Sudan Tribune, Agosti 5, 2025)

Ikiwa tu haya ni mara ya kwanza, na haitakuwa ya mwisho, kwamba watoto hufa kutokana na chanjo. Badala ya kuchunguza kinachoendelea na kuhakiki hatari ya sumu hizi kwa watoto wetu, tunafungua mlango wazi, pasi na kujali ni nani kati ya watoto wa Sudan anayekufa!

Mkasa huu unakwenda sanjari na mkutano kati ya Waziri wa Afya na Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), kujadili shughuli za shirika hilo kuhusiana na watoto, utoaji chanjo, ufikishaji wa chanjo, na udhibiti wa magonjwa. Alisisitiza kuwa UNICEF imepata imani ya washirika, ikiwemo Benki ya Dunia, Msaada wa Kimataifa, na Muungano wa Kimataifa wa Chanjo, katika kupata ufadhili wa zaidi ya dolari milioni 200 kutekeleza miradi nchini Sudan.

Watoto wa Sudan, na kile kinachowatokea, wako chini ya huruma ya serikali hii ya kitumwa. Inafanya biashara kwa maisha yao na mashirika ya kibepari ambayo hayana dini, maadili, na hayathamini kima cha kibinadamu. Hakika, kila kitu kinategemea maslahi wanayopata, hata ikiwa inahusisha maiti za watoto. Haya ndiyo yanayotokea kwa watoto wa Gaza, wanaokufa kwa njaa, huku mashirika haya yakisimama na kutazama. Na kabla ya hapo watoto wa Sham, Iraq na Yemen. Orodha inaendelea! Je, tunawezaje kuyaamini mashirika ya mauti ambayo yanatumia visingizio vya kibinadamu kuendeleza mipango yao na kuzifanyia majaribio chanjo kwa watu ambao hawana mchungaji au mlinzi?! Mwenyezi Mungu amekidhia katika Kitabu chake kitukufu kwamba makafiri ni maadui zetu. Kwa hivyo tunawezaje kuwaamini wao na matendo yao kwa watoto wetu?!

Nani atawalinda watoto wa Kiislamu kutokana na njama ambazo tawala hizi dhaifu zinahusika? Ni nani atakayeikata mikono ya walaji njama? Ni nani atalinda mustakabali wao, kuwapa maisha mazuri, maisha ya utulivu, mazingira mazuri, na mustakabali mzuri?! Chombo hiki hakika kitakuwa si chengine ila Dola ya Khilafah, ambayo, ilipotawala, Amiri wa Waumini, Umar, angekuja na kwenda kumuona mtoto mmoja analia ambaye mama yake alitaka kumwachisha ziwa. Mama angepokea zawadi kutoka kwa hazina. Aliposwali swala ya alfajiri (Mwenyezi Mungu amuwiye radhi), watu hawakuweza kuelewa kisomo chake kutokana na shaki ya kilio chake. Akasema (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake): “Ole wake Omar! Ameua watoto wangapi wa Kiislamu!”

Enyi Waislamu, je hamtambui pengo kubwa kati ya Khalifah, mlinzi wa Waislamu, na watawala wenu vibaraka, ambao wanawasalimisha watoto wenu kwa adui zenu? Jueni kwamba hamtaondolewa jukumu lenu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isipokuwa kwa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah, taji la faradhi zote za dini.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu