Jumatano, 11 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Rabi' I 1447 Na: HTS 1447 / 19
M.  Ijumaa, 29 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mvua ni Baraka na Rehema, lakini bila Uchungaji imekuwa ni Laana!

(Imetafsiriwa)

Mvua kubwa na mafuriko yaliyokumba maeneo mengi ya Sudan yamesababisha vifo vya watu 42, wengine 31 kujeruhiwa na kuharibu zaidi ya nyumba 4,000.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azirehemu na kuzisamehe familia zetu zilizokufa kutokana na mvua hii, na awajaalie hadhi ya mashahidi. Vile vile tunamuomba Mwenyezi aturehemu katika Hukmu yake.

Ni huzuni na pia inasikitisha kwamba msimu wa mvua hauji kwa ghafla, bali ni kipindi cha taarifa ambacho hurudiwa kila mwaka. Kinachoshangaza zaidi ni kwamba vituo vingi vya uchunguzi wa hali ya hewa vilionya kuhusu mvua kubwa, lakini asasi za serikali hazikuchukua hatua yoyote kuzuia madhara yake, ambayo yalikuwa mabaya zaidi kwa vijiji vya Jimbo la Mto Nile, mashariki mwa Sudan na hata Kordofan, miongoni mwa kwengine. Serikali haishughuliki na kutoa uchungaji. Vyenginevyo, ingeelekeza maafisa wake kufungua mitaro ya maji, kujenga madaraja, kukagua mabonde, kusongeza watu na mifugo kwenye maeneo ya miinuko, na kukagua makaazi ya watu kuona dalili za kuzuia mvua. Badala yake, inajishughulisha na masuala mengine, na kwa kufanya hivyo, imeacha kabisa jukumu lake la kuchunga ustawi wao, isipokuwa kutoa rambirambi kwa familia za wale ambao waliangukiwa na nyumba zao vichwani mwao! Mvua ambazo kimsingi ni rehema na baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu zimegeuka kuwa laana na janga!

Wajibu wa uchungaji kwenye shingo ya serikali ni jukumu ambalo Uislamu umeweka juu ya mtawala kwa raia. Mtume (saw) asema: «...وَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Na Imam (mtawala) ambaye yuko juu ya watu ni mchunga na anawajibika kwa raia wake.” Mtume (saw) alibeba jukumu hili kivitendo alipokuwa mtawala wa Waislamu mjini Madina. Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (ra) kuwa amesema:

«كَانَ النَّبِيُّ أَحْسَنَ النَّاسِ وَأَجْوَدَ النَّاسِ وَأَشْجَعَ النَّاسِ وَلَقَدْ فَزِعَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ ذَاتَ لَيْلَةٍ فَانْطَلَقَ النَّاسُ قِبَلَ الصَّوْتِ فَاسْتَقْبَلَهُمْ النَّبِيُّ قَدْ سَبَقَ النَّاسَ إِلَى الصَّوْتِ وَهُوَ يَقُولُ لَنْ تُرَاعُوا لَنْ تُرَاعُوا وَهُوَ عَلَى فَرَسٍ لِأَبِي طَلْحَةَ عُرْيٍ مَا عَلَيْهِ سَرْجٌ فِي عُنُقِهِ سَيْفٌ فَقَالَ لَقَدْ وَجَدْتُهُ بَحْرًا أَوْ إِنَّهُ لَبَحْرٌ»

“Mtume (saw) alikuwa mbora zaidi miongoni mwa watu (kwa sura na pia tabia) na alikuwa mkarimu zaidi miongoni mwao, na alikuwa shujaa zaidi wao. Wakati fulani, wakati wa usiku, watu wa Madina waliogopa (sauti). Basi watu wakaiendea sauti hiyo, lakini Mtume (saw) akiwa ameiendea sauti hiyo mbele yao, alikutana nao huku akisema: “Msiogope, Msiogope.” (Wakati huo) alikuwa anaendesha farasi wa Abu Talha na alikuwa uchi bila tandiko, na alikuwa amebeba upanga shingoni mwake. Mtume (saw) akasema, “Nimemkuta (farasi) kama bahari, au, hakika yeye ni bahari.” (Imepokewa na Al-Bukhari)

Wapendwa Watu wa Sudan: Imethibitishwa bila shaka kwamba mifumo hii ya urasimu haijali ustawi wenu; bali ni mzigo kwenu. Basi iacheni na fanyeni kazi kwa ajili ya radhi za Mola wenu pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha dola ya ustawi—Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Chini ya kivuli chake, mutaishi kwa furaha na ukarimu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu