Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 17 Rajab 1447 | Na: HTS 1447 / 83 |
| M. Ijumaa, 16 Januari 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vyombo vya Usalama jijini Umdurman Vyalikamata Kundi la Wanachama wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)
Kufuatia utekelezaji wa mashababu wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan wa visimamo vitatu katika maeneo tofauti tofauti katika jiji la Omdurman, asubuhi ya Jumatano iliyopita, 25 Rajab 1447 H, sambamba na 14/1/2026 M, ndani ya muundo wa kukumbusha tukio la kupita kwa miaka 105 tangu kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah mwezi Rajab 1342 H, vyombo vya usalama viliendelea kuwakamata wanachama watano wa Hizb: Al-Radi Muhammad Ibrahim, Fadlallah Ali Suleiman, Omar Al-Bashir, Hassan Fadl, na Mujahid Adam. Kisha waliachiliwa baada ya Magharibi siku ya Jumatano baada ya nambari zao za simu kuchukuliwa na baada ya kunyakua mabango ambayo Mashababu hao wa Hizb ut Tahrir walikuwa wamebeba katika visimamo hivyo vitatu. Kisha waliitwa mnamo alasiri ya Alhamisi, 15/1/2026, na wangali wako kizuizini hadi wakati wa kuandika taarifa hii!!
Uhalifu wa hawa Mashababu ni kwamba wanawakumbusha Umma kuhusu maisha ya heshima kwa kumtii Mwenyezi Mungu, wakati Ummah ulipokuwa na dola iliyoasisiwa kwa msingi wa Uislamu, na jinsi hali yetu ilivyo leo baada ya Dola ya Khilafah kuvunjwa, kwani tuko katika udhalilifu na fedheha, na katika utiifu kwa mkoloni kafiri wa Magharibi.
Haya ni baadhi ya yale yaliyoandikwa kwenye mabango yaliyoinuliwa kwenye visimamo:
- Chini ya Khilafah, matukufu ya Waislamu—maisha yao, damu yao, heshima yao, na utajiri wao, yanahifadhiwa na kulindwa.
- Kupitia Khilafah, umoja wa Waislamu unafikiwa, Sharia inatekelezwa, na Uislamu unapelekwa kwa walimwengu wote.
- Kwa kuvunjwa Khilafah, umbo la Ummah wa Kiislamu lilibomolewa, na damu yake ilitawanywa juu ya utaifa, uzalendo, na umadhehebu.
- Khilafah, enyi Waislamu, ni faradhi ya Mola wenu Mlezi na chanzo cha heshima yenu, na mengine ambayo yako katika mwelekeo na maana hii hii.
Kwa hivyo je, yule anayelingania kwenye heshima ya Uislamu na Waislamu, na kusimamisha faradhi ya Mola Mlezi wa Walimwengu chini ya Dola ya Uislamu Khilafah, atiwe hatiani na kukamatwa?! Hakika, kile ambacho vyombo vya utawala vimekifanya kinaangukia katika kundi la kuzuia njia ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
[الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجاً أُوْلَـئِكَ فِي ضَلاَلٍ بَعِيدٍ]
“Wale wanao fadhilisha maisha ya dunia kuliko Akhera, na wanawazuilia watu wasifuate Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanataka kuipotosha. Hao wamepotelea mbali.” [Surah Ibrahim: 3].
[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]
“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Surah Ash-Shu‘ara: 227]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



