Afisi ya Habari
Tanzania
H. 7 Rabi' I 1446 | Na: 1446 / 03 |
M. Jumanne, 10 Septemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Tanzania Inalaani Kutekwa Nyara na Kuuwawa Muhammad Ali Kibao
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Tanzania inatoa mkono wa pole na kuifariji familia na jamaa kufuatia kuuwawa kada wa Chadema Muhammad Ali Kibao ambaye alitekwa nyara mnamo Septemba 6, 2024 na kisha kuuwawa.
Tunalaani vikali utekaji nyara huo na mauaji hayo ya kikatili, kisha tungependa kutamka yafuatayo:
1. Vitendo vya utekaji nyara vinavyopelekea kupotezwa au kuuliwa kikatili si vigeni Tanzania, vimekuwapo kwa muda sasa, ambapo wahanga wakubwa wa ukatili huo ni Waislamu kwa Uislamu wao. Kwa mfano, kuna wahanga zaidi ya 380 hawajulikani walipo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji kufuatia kamata kamata ya serikali ndani ya mwaka 2017 iliyoambatana na mateso na mauaji ya kiholela’ (The East African, May, 2018).
2. Matukio kama haya sio tu yanaleta hofu, ukosefu wa amani, kuchafuka na kuathirika haiba ya serikali, bali pia ni kielelezo cha wazi cha kukosekana uwajibikaji wa serikali, kwa kuwa dola ndio mdhamini mkuu na mlinzi wa usalama wa raia, mali zao na heshima zao.
3. Aidha, matukio kama haya yanaonesha wazi wazi kushindwa kwa mfumo wa kibepari na demokrasia yake ulimwenguni kote, kwa kuwa mfumo huo unazua machafuko, vurugu na utovu wa amani kwa wanadamu.
Ni wazi, ulimwengu unahitaji mfumo wa haki na uadilifu ambao si mwengine bali ni Uislamu. Mfumo huo una uwezo wa kudhamini ulinzi wa raia, maisha, mali na heshima zao.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |