Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  17 Sha'aban 1443 Na: HTY- 1443 / 12
M.  Jumapili, 20 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Kunyanyua Kauli Mbiu ya "Kujitosheleza" Kunawiana na Kuomba Usaidizi wa Kimataifa, Ee Serikali ya Wokovu Kaskazini mwa Yemeni?

 (Imetafsiriwa)

Serikali ya Wokovu jijini Sanaa ilizindua ombi kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, Hisham Sharaf, kwa mawaziri wa mambo ya nje wa Sweden na Switzerland, katika nafasi zao kama wenyeviti wa Kongamano la Wafadhili kuhusu Hali ya Kibinadamu nchini Yemen kwa mwaka wa 2022. Ombi hilo la serikali lilikuja katika gazeti la kila siku la Al-Thawra lililochapishwa jijini Sanaa mnamo tarehe 16/3/2022 kwa jumuiya ya kimataifa kuhusiana na kuendelea kutoa ruzuku za kila mwaka zinazowasilishwa kwake chini ya jina la Mwitikio wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa tangu 2016 hadi leo, likiambatana na ripoti ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengineyo kama vile Shirika la Chakula na Kilimo, Mpango wa Chakula Duniani na Shirika la Mama na Mtoto, ambayo yalisema katika ripoti yake haja ya msaada wa watu milioni 17.4 mpaka 19, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2022.

Inashangaza na kustaajabisha kwamba ombi hili la Serikali ya Wokovu linakuja katika wakati ambapo inazungumzia kuhusu kuwa katika udhibiti wa uamuzi wake huru, na utekelezaji wake wa mipango na vitendo vinavyofanikisha kujitosheleza kwa watu katika maeneo yote: chakula, viwanda, dawa, silaha, nk., na kusambaza bidhaa kutoka nje zinazoweza kuzuia mipango na kazi ya Serikali ya Wokovu, na kuipokonya matakwa yake, na kuisalimisha katika kutii amri kutoka nje! Kwa hiyo, watu wa Yemen wamechanganyikiwa. Watamwamini nani: ombi la Serikali ya Wokovu kwa msaada kutoka nje na kuutegemea, au katika kauli zake za kufikia kujitosheleza?! Kwa sababu yeyote yule ambaye kwa hakika anataka kutoroka kutoka kwenye unyenyekevu na utegemezi kiuhalisia na sio kama kauli mbiu tupu, ni lazima aondoe mikono ya makafiri tangu siku ya kwanza, na awe na udhibiti wa maamuzi yake huru, asiwe kibaraka mikononi mwa wengine anaye endeshwa kulingana na maslahi yao na kumakinisha ushawishi wao.

Ingawa tukichunguza suala la ruzuku na misaada ya kimataifa inayotolewa kwa Yemen, tutagundua kuwa jumuiya ya kimataifa ndiyo chanzo cha moja kwa moja cha matatizo na masaibu ya dunia, ikiwemo Yemen kupitia mizozo baina ya nchi zake kuhusu maeneo yao yenye ushawishi wa kisiasa unaozunguka ulimwengu, ikijumuisha mapambano ya zamani ya Uingereza dhidi ya Yemen na Amerika, upande mpya unaopendelea kugawanyika kwa Yemen, ili kurahisisha kuidhibiti, na kuchora upya ramani ya Sykes-Picot baada ya zaidi ya miaka 100 ya kutiwa saini kwake, na kuibadilisha na Mashariki ya Kati mpya. Wananchi wa Yemen lazima watambue kwamba, kiasi kikubwa cha fedha ambacho Umoja wa Mataifa hupokea kila mwaka kwa kisingizio cha kuwaokoa wananchi wa Yemen na hali ngumu waliyonayo, hakiwezi kuwaletea manufaa yoyote.

Umoja wa Mataifa hautafuti suluhisho la kimsingi kwa watu wa Yemen ili kuwaondolea dhiki hii, kwani uingiliaji kati na miradi yake yote ni sindano tu za ganzi na hazina athira yoyote inayoonekana ardhini zaidi ya kuwaweka watu wa Yemen katika hali mbaya, na kuwarushia makombo ya misaada ili kuwanyamazisha wasiinuke na kuwawajibisha wahusika kwa uhalisia huu mchungu. Hii ni kwa sababu serikali za Aden na Sanaa, sawa na watangulizi wao, zimewasalimisha watu wa Yemen kwa Kafiri Magharibi, wakati mwingine kupitia kuomba misaada na wakati mwingine kupitia uingiliaji wa moja kwa moja, pamoja na kutabikisha mifumo ya kisekula katika uhalisia wa maisha ya watu. Mifumo inayokinzana na ghariza na Dini.

Je, ni lini watu wa Yemen watatambua kwamba wanaweza kukomesha uingiliaji wa kigeni wa Magharibi katika nchi yao na kuuondoa; kwa kurudisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu katika nchi ya Imani na Hekima, kwa kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi kwa bidii, na inawalinganieni kujiunga nayo katika kazi ya kusimamisha faradhi hii na kuwakomesha Makafiri na kuwahisabu watawala madhalimu katika nchi za Kiislamu.

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ) “Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum: 4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu