Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  17 Jumada II 1446 Na: HTY- 1446 / 10
M.  Alhamisi, 19 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mahouthi Wanaendelea na Jinai na Uhalifu wao... Kuwakamata Wanachama wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Kuanzia Alhamisi, tarehe 10 Jumada al-Akhir 1446 H sawia na tarehe 12 Disemba 2024 M, wanamgambo wa Houthi walifanya uvamizi kwenye nyumba za wanachama wa Hizb ut Tahrir bila ya kuzingatia vifungu vya sheria ya Kiislamu au hata kanuni na desturi za kikabila! Walivamia nyumba zao katika kurugenzi tatu za Jimbo la Taiz (Taiziyah, Mawiah, na Khadir); na kuwakamata: Suleiman al-Muhajri, Khaled al-Hami (waliyemwekwa kizuizini miezi sita iliyopita kwa tuhuma za kubeba Dawah pamoja na Hizb ut Tahrir), Mhandisi Taqi al-Din al-Zayla'i, Amir al-Sabry, na Muhammad al-Faqih. Wafuasi watatu wa Hizb ut Tahrir pia walikamatwa: Abdul Malik al-Jundi, Abdul Qader al-Sarari, na Adnan al-Zayla'i, ambao wanasalia chini ya ulinzi wa wahalifu hao mpaka kufikia wakati wa kuandika taarifa hii.

Mashtaka ya wanachama hao wa Hizb ut Tahrir ni kulingania kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah, kuwafundisha Waislamu njia ya Mola Mlezi wa walimwengu wote, na kueneza ufahamu baina yao kuhusu ufisadi wa mfumo wa kirasilimali ambao wanatawaliwa  nao leo, na kufichua mipango na njama za Kafiri Magharibi na watawala vibaraka wake wanaofanya kazi usiku na mchana kuwapiga vita Waislamu wanaotaka kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Waasi wa Houthi wanaamiliana na watu wa Yemen kwa fikra ya magenge, wakiwakamata watu wenye ikhlasi bila ya mashtaka au kesi. Hawajajifunza kutokana na yale yaliyompata Bashar jana, na bado wangali wanaendelea na jinai zao na ukandamizaji dhidi ya wale wanaofanya kazi ya kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu, na wana chuki na Uislamu na Waislamu. Yote haya ni katika kumtumikia bwana wao, Marekani, ambayo inaogopa kuanzishwa kwa Khilafah Rashida na inaogopa sana Hizb ut Tahrir na wanachama wake, kiasi kwamba kutajwa tu jina la Hizb ut Tahrir kunawatia hofu. Vibaraka wa kikoloni kutoka kwa Mahouthi walikasirishwa wakati wanachama wa Hizb ut Tahrir walipogawanya toleo lenye kichwa: “Marekani, kupitia Usitishaji vita, Inafikia Malengo Mawili Muhimu kwa Uvamizi wa Kiyahudi: Kuondolewa kwa Vikosi vya Hezbollah vinavyoungwa mkono na Iran Kaskazini mwa Mto Litani, na Kutenganishwa kwa Maeneo Miwili!” ambalo lilisema: “Mnamo tarehe 27 Novemba 2024, usitishaji mapigano ulitangazwa katika upande wa Lebanon kati ya umbile la Kiyahudi na Hezbollah… Wakati huo huo, Amerika, Mayahudi, na tawala za kisaliti zinazozunguka Palestina walipanga makubaliano yatakayohakikisha ushindi kwa Mayahudi dhidi ya Gaza chini ya masharti wanayoamuru. Haya yanatokea wazi mbele ya watawala wasiomcha Mwenyezi Mungu wala hawaoni haya.

[قَاتَلَهُمُ اللهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ]

“Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Munafiqun: 4]

Toleo hili liliwatia hofu na kuwafanya waandae majeshi yao ili wamkamate aliyeligawanya kwa watu. Kidhahiri wanaonekana kutangaza uungaji mkono wao kwa Gaza, lakini kiuhalisia, wako karibu na maadui wa Gaza! Kila mtu anajua kwamba Hizb ut Tahrir ndicho chama pekee kilicho makini katika kuondoa ushawishi wa kafiri Magharibi kutoka katika ardhi zetu kwa kuwapindua vibaraka wake na mfumo fisadi wa kirasilimali.

Hizb ut Tahrir imekuwa ikifanya kazi kwa zaidi ya miaka sabiini, na inaendelea kwenye njia yake iliyo wazi na mwelekeo angavu. Si Magharibi wala Mashariki wala vibaraka na wapambe kama nyinyi wameweza kuizuia. Haiogopeshwi na matendo yenu ya kitoto, wala kwa majaribio ya kuitisha au kuwakamata wanachama wake. Inatangaza kwa uwazi na hadharani kwamba inaendelea na mapambano yake ya kifikra na kisiasa na inaendelea kuwafichua vibaraka wa ukoloni wanaotabikisha mfumo wake na kuwakamata wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah ya Kiislamu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Yemen, tunawaambia viongozi wa Kihouthi: Fikirieni kuhusu hali ya wale waliokuja kabla yenu, na mregee kwenye fahamu zenu, na muwaachilie huru wanachama wa Hizb ut Tahrir wasio na silaha isipokuwa neno la uaminifu na ikhlasi, na watu wengine wasio na hatia katika jela zenu, na watoleeni njia wana wa Umma waaminifu na wenye utambuzi kuwatawala watu kwa mujibu wa sheria ya Mwenyezi Mungu. Ama nyinyi, uwongo na hadaa zenu zimefichuliwa, kwenu Uislamu si chochote ila ni kauli mbiu tu ambazo mnazipigia kelele usiku na mchana kwa kauli mbiu isemayo: “Mauti kwa Marekani” huku mkitabikisha mfumo wake wa kijamhuri wa kisekula! Mnachofanya ni uovu!!

Tunawakumbusha wanachama wa vyombo vya usalama na majasusi na watoa habari wote wanaotekeleza amri za Mahouthi kwamba ni wajibu wao kusimama na wana watiifu wa Umma na kutofuata maelekezo ya watawala wasaliti, vyenginevyo watapata hasara, na hawataepuka adhabu kwa sababu wao ndio mkono unaosababisha mateso kwa watu. Tunawakumbusha kuwa adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kubwa zaidi kesho Akhera na watakuwa pamoja na watawala wasaliti, basi msidhani kuwa wao wamesalimika na adhabu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا * وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا * رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْناً كَبِيراً]

“Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume! Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia. Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa.” [Al-Ahzab 66-8].

Khilafah kwa njia ya Utume itaregea hivi karibuni, InshaAllah. Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu, na bishara njema ya Mtume wetu, rehma na amani zimshukie. Hizb ut Tahrir imejitolea kufanya kazi usiku na mchana ili kuisimamisha.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu