Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Juu ya Tukio la Ukumbusho wa Ukombozi wa Konstantinopoli mnamo 857 H – 1453 M
(Imetafsiriwa)

 

[tafsiri ya Video kwa Kiswahili itakujia hivi karibuni]

Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu (swt), baraka, rehema na amani zimwendee Nabii wa Mwenyezi Mungu, familia yake na maswahaba zake na wale wanaomfuata…

Kwa Ummah wa Kiislamu, ummah bora ulioletewa wanadamu… na wabebaji Dawah wema na wazuri… na kwa wageni adhimu wanaozuru ukurasa,

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Zipo siku zinazong’aa katika historia za mataifa ambazo ni chanzo cha ufahari wa mataifa hayo. Kwa hiyo itakuwaje ikiwa siku hizo zitakuwa ni katika kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)? Bila shaka zitakuwa ni nyota zenye kung’aa angani, bali ni jua linalotoa nuru kwa ulimwengu na kulinyanyua taifa hilo juu angani… Na katika siku hizo tukufu, zipo siku za ukumbusho wa ukombozi wa Konstantinopoli… Al-Fatih alianza kuivamia na kuizingira Konstantinopoli kuanzia tarehe ishirini na sita ya Rabii’ al-Awwal mpaka ilipofunguliwa alfajiri ya tarehe ishirini ya mwezi huu wa Jumada al-Awwal 857 H, ikimaanisha kuwa kuzingira kulichukua muda wa takribani miezi miwili. Kisha Muhammad al-Fatih aliingia mjini kwa ushindi na kushuka kutoka katika farasi wake na kumsujudia Mwenyezi Mungu, akimshuruku Mwenyezi Mungu kwa ushindi huo na kufaulu huko. Kisha akaelekea katika Kanisa la Hagia Sophia ambapo Wabaizantino na watawa wao walikuwa wamekusanyika, akawapa ulinzi. Akaagiza kubadilishwa kwa Kanisa la Hagia Sophia kuwa msikiti na kuamrisha kujengwa kwa msikiti katika sehemu ya swahaba mtukufu Abu Ayoub Al-Ansari, ambapo alikuwa ni mmoja katika waliokuwa safu za mwanzo katika kampeni ya kuifungua Konstantinopoli na ndipo alifariki, rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake… Al-Fatih, ambaye aliitwa hivyo baada ya ukombozi na kuamua kuifanya Konstantinopoli kuwa mji mkuu wa dola yake ambayo kabla hapo ilikuwa Edirne, na kuita Konstantinopoli [Kostantiniyye] baada ya ukombozi wake kuwa “Islambol,” ikimaanisha mji wa Uislamu [Dar al-Islam] na kujulikana maarufu kama “Istanbul”. Al-Fatih kisha akaingia mjini na kwenda Hagia Sophia ambapo aliswali ndani yake na kuwa msikiti kwa neema, baraka na sifa za Mwenyezi Mungu… Na ulibakia kuwa msikiti uliotakasika na wenye taadhima, uliostawi chini ya waumini, mpaka zama za wahalifu, Mustafa Kamal alipofaulu kupiga marufuku kuswali ndani yake na kuutia najisi na kuwa makumbusho kwa wale wanaokuja na kuondoka!

Hivi ndivyo bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ilivyo timizwa; ambaye katika Hadith yake tukufu iliyopokewa kutoka kwa Abdullah ibn Amr ibn Al-As aliyesema: “Tulipokuwa na Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) tukiandika, Nabii wa Mwenyezi Mungu aliulizwa, ni upi kati ya miji miwili utakaofunguliwa kwanza, Konstantinopoli au Roma? Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) akasema:«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلاً، يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»“Mji wa Heraclius utafunguliwa kwanza, ikimaanisha Konstantinopoli.” Imesimuliwa na Ahmad katika Musnad yake na Al-Hakim katika Al-Mustadrak na akasema: “Hadith hii ni sahih kwa masharti ya msheikh wawili, na hawakuivua wao. Az-Zahabi ameizungumzia: “kwa masharti ya Bukhari na Muslim”. Pia katika Hadith tukufu iliyopokewa kutoka kwa Abdullah bin Bishr Al-Khathami kutoka kwa babake kwamba alimsikia Mtume (saw) akisema: «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»Mutaifungua Konstantinopoli, Amiri wake ni Amiri bora, na jeshi bora ni jeshi hilo.” Alisema, Maslama bin Abdul Malik aliniita na kuniuliza, kwa hiyo nikamtajia hiyo Hadith na hivyo basi akaivamia Konstantinopoli, imesimuliwa na Ahmad. Katika Mujma’ Az-Zawaa'id, aliizungumzia na kusema: “Imesimuliwa na Ahmad, Al-Bazzar, Al-Tabarani na wanaume wake ni waaminifu…”

Bishara njema hii ilitimizwa kupitia mikono ya kijana mwanamume, Muhammad al-Fatih, ambaye alikuwa na miaka ishirini na moja, lakini alikuwa ameandaliwa vyema tokea utotoni mwake. Babake Sultan Murad II alimlea na kumjenga kupitia mikono ya walimu bora wa zama zake, wakijumuisha Ahmad bin Ismail al-Kurani ambaye alitajwa na al-Suyuti kuwa mwalimu wa kwanza wa al-Fatih na alimzungumzia: “Alikuwa mwanachuoni wa kisheria, ambaye wanachuoni wa zama zake walishuhudia ubora na ustadi wake wa hali ya juu. Bali walikuwa wakimuita: Abu Hanifa wa zama zake.” Vilevile Sheikh Akshamsaddin Sungkar ambaye alikuwa wa kwanza kupanda akilini mwake hadith za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) juu ya “ukombozi wa Konstantinopoli” tangu utotoni mwake. Kwa hiyo kijana alikulia akilenga kufaulisha ukombozi kwa mikono yake… Sheikh Akshamsaddin alimfunza Muhammad al-Fatih misingi ya sayansi ya Qur’an, Hadith na Sunnah ya Mtume na Fiqhi pamoja na lugha za Kiarabu, Kifursi na Kituruki, pamoja na sayansi za maisha kama hesabu, falaki, historia… kwa kuongezea ujasiri wake katika kuongoza farasi na sanaa ya kupigana… Mwenyezi Mungu (swt) akamfadhilisha na kumbariki, kustahiki sifa kutoka kwa Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw). Al-Fatih alikuwa kiongozi bora na wanajeshi wake walikuwa bora, kwa kuwa mioyo yao ilikuwa imejaa Imani na nafsi zao zilikuwa zimejisalimisha katika maandalizi na kuwa na ikhlass kwa jihad, walimnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye akampa ushindi kwa ukombozi mtukufu, sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wa Ulimwengu.

Al-Fatih alikuwa mtu aliye na ruwaza na mwenye maono na utambuzi wa kina. Kila alipoona tatizo alilishughulikia kwa usahihi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kila kikwazo kinapomtokezea, alikiondosha kwa msaada wa Mwenyezi Mungu. Alikumbana na vikwazo vitatu ambavyo alivitatua kwa akili yake makini na werevu wa hali ya juu:

1. Wanajeshi wake walimlalamikia kuhusu baridi kali walipokuwa katika sehemu za wazi zilizozunguka kuta, kwa hiyo akawajengea ngome ili waweze kujihifadhi kila kunapokuwa na dharura. Hakutaka wanajeshi wasitishe uzingiraji lau ungeliendelea kwa muda na hivyo kurudi kama ilivyokuwa kwa majeshi ya Waislamu ya awali ambayo yaliivamia Konstantinopoli, lakini badala yake hakutaka kurudi isipokuwa mpaka kufunguliwa kwa Konstantinopoli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu…

2- Pia, kuta za Konstantinopoli zilikuwa kuta tatu; kila mita chache kulikuwa na kuta baina yake. Hivyo basi, al-Fatih alishangazwa na suala hilo. Katika zama zao, hakukuwa na silaha zenye nguvu za kuzivunja. Bali, yenye nguvu zaidi ya zote ilikuwa panda ya kutupa mawe, sio ndogo kiukubwa lakini haitoshi kutoboa tundu katika ukuta wa ukubwa huo. Na kwa sababu Muhammad al-Fatih alikuwa anafuatilia uwezo wa kijeshi duniani, alikuja kugundua kwamba mmoja miongoni mwa wahandisi (Urban) wa Hangaria alikuwa amekuwa na fikra za kutengeneza mizinga maalum yenye nguvu za kuweza kuvunja kuta na Urban akaomba kumfanyia kazi Mfalme wa Konstantinopoli, lakini hakumjibu, kwa hiyo al-Fatih akampokea kwa wema na kumpa mshahara mkubwa na kila kitu anachohitaji kukamilisha uvumbuzi wake,

Urban alijenga mizinga kwa msaada wa wahandisi wa Kiuthmaniya na al-Fatih aliwasimamia mwenyewe. Kabla hata miezi mitatu kupita Urban tayari alikuwa ametengeneza mizinga mitatu mikubwa, uzito wa kombora la mzinga lilikuwa takribani tani moja na nusu, hakupendelea kujaribu mizinga hiyo kwa kuhofia kwamba majibu yasiridhishe. Na hivyo Waroma wangelishuhudia hili wakiwa nyuma ya kuta zao na hili lingeathiri nguvu za Waislamu, kwa hiyo akafanya majaribio huko Edirne na yakafaulu. Akamshukuru Mwenyezi Mungu, na kuihamisha kutoka Edirne na kuipeleka mizinga karibu na kuta za Konstantinopoli ili kuzivunja na Waroma wangelijisalimisha…

3- Kisha kulikuwepo na jambo jingine ambalo lilikuwa linamshughulisha, kwa kuwa alijua kwamba kuta za eneo la Ghuba zilikuwa dhaifu pembezoni mwa Konstantinopoli na licha ya Waroma kufahamu udhaifu wa kuta za upande wa Ghuba, walikuwa na uhakika kwamba meli za Waislamu zisingeliweza kuwafikia kwa sababu ya kufungwa kwa lango la Ghuba kwa minyororo ya chuma, lakini al-Fatih kwa msaada wa Mwenyezi Mungu alikuwa amekatikiwa kuzitiririsha meli kupitia uso wa kilima cha Galata sawia na ukuta wa upande wa Ghuba (Pembe ya Dhahabu). Aliweka bao katika uso wa kilima na kumwaga viwango vikubwa vya mafuta na vilainishaji juu yake, kisha akazivuta meli juu yake. Na kwa usiku mmoja alifaulu kushusha meli 70 kwenda Ghuba. Hili liliwashtusha Waroma, ilipofika asubuhi na wakaona meli za Waislamu katika Ghuba, wakajaa uoga katika mioyo yao. Ushindi na ukombozi ulikuwa umefaulu, sifa zote ni kwa Mwenyezi Mungu, Bwana wa ulimwengu.

Ndugu zangu wapendwa, Nilitaka kuwakumbusha baadhi ya matukio ya ukombozi wa Konstantinopoli kwa sababu tatu:

Ya kwanza ni kukumbuka utukufu wake ili kila mwenye macho ataona utukufu wa Uislamu na Waislamu pale ambapo Uislamu wao unatekelezwa kivitendo. Ukafiri hautokuwepo, bali ukweli utakuwa juu na utanyanyuliwa kama Adhana (mwito wa kuswali) kwa Allahu Akbar (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa). Wafursi na Wabaizantino wakajisalimisha mbele yao, na hivi karibuni wataunganishwa, kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu, na dada wa Baizantino, Roma kwa kuamini sehemu ya bishara njema ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), ukombozi wa Roma.

Ama ya pili, itulizeni mioyo yenu kwa kujihakikishia kutimia kwa bishara tatu nyingine za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa kuwa ya kwanza ishatimia. Mtume (saw) alitoa bishara njema za ukombozi wa Konstantinopoli, ukombozi wa Roma, kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa nguvu kubwa… Mtume (saw) anazungumza kutokamana na Wahyi, bishara njema tatu zilizobakia za Nabii zitatimizwa kwa idhini Yake, utukufu ni wake Yeye Subhannahu; lakini, hazitotimia kwa kushuka kwa malaiki kutoka mbinguni, na kutukukabishi sisi. Badala yake ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kwamba tumnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye atupe ushindi Wake ili tuweze kusimamisha sheria Yake na kuutukuza muundo wa Dola Yake na kuandaa tunachoweza katika nguvu na kisha kupambana katika njia Yake. Kisha dunia itang’ara kwa bishara njema tatu zilizobakia na dunia itanawiri kwa kuwepo Khilafah kwa mara nyingine tena.

Ama ya tatu, Kafiri Mmagharibi, pamoja na makhaini wa Kiarabu na Kituruki waliweza kuivunja Khilafah mnamo 1342 H - 1924 M na kuzingatia kuwa kuvunjwa huku ni sambamba na ukombozi wa Konstantinopoli, na hili likampa tena nguvu Kafiri Mmagharibi ambazo alikuwa amezipoteza. Wasiwasi wa Magharibi ukawa ni kuweka juhudi kubwa ili kuzuia kurudi tena kwa Khilafah ili isiweze kupoteza tena nguvu walizozirudisha hususan kwa kuwa wamekuwa wakoloni wa nchi za Waislamu. Wanafuatilia kwa makini harakati ndani ya nchi za Waislamu, kwa hiyo ilipotangazwa kusimama kwa Hizb ut Tahrir mnamo 1372 H - 1953 M na ikawa wazi kwa Magharibi kwamba nguzo ya kazi za chama na suala lake nyeti ni kurudisha Khilafah tena na kwamba kiko makini katika kazi yake, Magharibi ikaamrisha vibaraka na watawala wake kukipiga marufuku chama na kukifuatilia kwa kuwashika na kuwatesa mpaka kupata shahada ndani ya baadhi ya maeneo na kuwafunga vifungo virefu na katika maeneo mengine kufikia kuwafunga maisha… Kisha wakaongeza njia za kudanganya, kughushi na kubadilisha ukweli pasina aibu…

Na kwa hiyo ili hawa wapotoshaji wawe na athari, wakawafanya watu wanaotekeleza hatua hizi kuwa na majina ya Waislamu na kuvaa kama wao, hawa walifuatiwa na upotoshaji huu, na baadhi yao walitoka, walivunja viapo (an-Nakitheen) na walioadhibiwa, kutoka miongoni mwa waliokuwa katika chama hapo awali…

Hivyo basi, aina hii wakajumuika na kushiriki katika upotoshaji, kughushi na kubadilisha ukweli na kila mmoja wao ana dori yake: makafiri, wanafiki na wale wanaoeneza uvumi, kisha baadhi yao wakaondoka, wakaadhibiwa na wakavunja viapo, na wale walio na maradhi katika mioyo yao, wameshiriki katika upotoshaji na mashambulizi dhidi ya Hizb. Walifuatilia hili kwa hatua zilizojaa sumu na kudanganya katika kila hatua. Walipokuwa wamefeli kusambaza uongo, wakaja na jingine, wakisahau kwamba wanachama wa chama wana akili zilizo makini na utambuzi wa haraka unaowawezesha kutofautisha baina ya baya na zuri, kwa hiyo hawakuruhusu uongo kupenya katika njia yao… Hivyo basi, licha ya njia za kuupamba uongo waliouzua licha ya kukithirisha majaribio ya udanganyifu dhidi ya ukweli ambao wamejikita ndani yake, hawakupata sikio linalosikiza kutoka katika wanachama wa chama au kutoka katika kila Muislamu aliye timamu. Badala yake walikuwa

[كَسَرَابٍ بِقِيعَةٍ يَحْسَبُهُ الظَّمْآنُ مَاءً حَتَّى إِذَا جَاءَهُ لَمْ يَجِدْهُ شَيْئاً]

“Vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi) uwandani, Mwenye kiu huyadhania ni maji. Hata akiyaendea hapati chochote.” [An-Nur: 39]

Na kwa njama, kashfa na uovu wote dhidi ya chama na uongozi wake, wakidhania kwamba watakishawishi chama lakini walifeli kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na wakakata tamaa na hawakupata lolote zuri licha ya kiwango cha uongo wao, njama zao na uhadaifu wao kilipofikia,

 [وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ]

“…na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Fatir: 43]

[وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ ]

"Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46].

Kwa kutamatisha, misimamo yenu ndugu zangu iliyokita katika ukweli, nguvu na uwazi mbele ya kampeni za kufuatana dhidi ya ujumbe wa haki, unatukumbusha misimamo ya Maswahaba, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, kwa kufuata misimamo ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw), mtukufu na mwenye busara alipokabiliana na shari… Hivyo ndivyo misimamo yenu, iliyo madhubuti isiyodhoofika kwa shari na haitingishiki katika kipindi cha fitnah. Badala yake, ukakamavu wenu ni wenye nguvu na sauti zenu zinatamka haki. Munaitizama dunia mara moja na Akhera mara nyingi, kwa hiyo pongezi kwa chama kwa sababu kimewapata nyinyi na pongezi kwenu kwa kuwa na chama.

 [ رِجَالٌ لَا تُلْهِيهِمْ تِجَارَةٌ وَلَا بَيْعٌ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَإِقَامِ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ يَخَافُونَ يَوْماً تَتَقَلَّبُ فِيهِ الْقُلُوبُ وَالْأَبْصَارُ*لِيَجْزِيَهُمُ اللَّهُ أَحْسَنَ مَا عَمِلُوا وَيَزِيدَهُمْ مِنْ فَضْلِهِ وَاللَّهُ يَرْزُقُ مَنْ يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ]

“[Ni] wanaume ambao biashara wala kuuza hakuwashughulishi na kumdhukuru Mwenyezi Mungu, na kushika Sala, na kutoa Zaka. Wanaikhofu Siku ambayo nyoyo na macho yatageuka – Ili Mwenyezi Mungu awalipe bora ya waliyo yatenda, na awazidishie katika fadhila zake. Na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” [An-Nur: 37-38]

Mwisho wa kutamatisha, namuomba Mwenyezi Mungu (swt) atuwezeshe kutimia kwa bishara njema za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ili Khilafah ya Ummah huu iweze kurudi na baada ya hapo kuikomboa Al-Quds, na Roma itakombolewa kama ilivyotanguliwa na dadake… kutimia kwa hadith za Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw)… Na pia tunamuomba Yeye, Utukufu uwe Kwake, atupe msaada kutoka Kwake ili tuweze kuboresha na kukita katika kazi ili tuwe tunaostahiki kupata ushindi wa Mwenyezi Mungu, Al-Aziz Al-Rahim.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi* Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Wa Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Alhamisi, 7 Jumada Al-Awwal 1441 H                                                                             Ndugu Yenu,

2/1/2020 M                                                                                                       Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

                                                                                                                               Amiri wa Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 23 Januari 2020 14:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu