Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Risala Kutoka kwa Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Siku Kuu ya Idd ul-Adha Yenye Baraka ya Mwaka 1440 H Ikiafikiana na Mwaka 2019 M

(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na juu ya jamaa na maswahaba zake, na wale wanaomfuata, ama baada yao.

Kwa Ummah mtukufu wa Kiislamu, kwa mahujaji wa Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, kwa wabebaji Da’wah watukufu, kwa waheshimiwa wanaozuru ukurasa wa Facebook,

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh, Mwenyezi Mungu aukubali utiifu wenu, na Mwenyezi Mungu aifanye Idd yenu ijae kheri na baraka. Mwenyezi Mungu aikubali Hajj ya waliohiji, na Mwenyezi Mungu aifanye iwe Hajj iliyo kubaliwa, na juhudi zilizo pokewa na dhambi zilizo samehewa. Pia namuomba Mwenyezi Mungu (swt) awape tawfiq wale ambao hawakuhiji mwaka huu wahiji mwakani kwa kheri juu ya kheri.

Kaka zangu na dada zangu waheshimiwa, tunamtukuza kwa Takbir na tunamsifu Mwenyezi Mungu kwa neema ya Uislamu, na tunamtukuza na kumsifu Yeye (swt) kwa neema ya ubebaji da’wah hii pamoja na swafu za Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah. Tunamtukuza na kumsifu Yeye Subhanahu wa Ta’ala kwamba chama hiki kimesimama imara licha ya njama za wakoloni na vibaraka wao, watawala wa biladi za Waislamu, na licha ya khiyana za wanafiki, ambao nyoyo zao zinaugua na wazushi. Hakika, tunamtukuza Mwenyezi Mungu kwa Takbir: Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd.

Khilafah, ambayo Hizb ut Tahrir inaisaka, inawakesheza usiku kucha wakoloni makafiri, na kuwaogofya vibaraka wao watawala katika biladi za Waislamu, na kuwatia dhiki wanafiki na wenye chuki ambao nyoyo zao zinaugua, wanao wakimbilia makafiri kwa ajili ya hifadhi kutokana na kile wanachodai kitawasibu.

[فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ مَرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَى أَنْ تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ فَعَسَى اللَّهُ أَنْ يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِنْ عِنْدِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَى مَا أَسَرُّوا فِي أَنْفُسِهِمْ نَادِمِينَ]

“Utawaona wale wenye maradhi nyoyoni mwao wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu yasitusibu mabadiliko. Huenda Mwenyezi Mungu akaleta ushindi au jambo jengine litokalo kwake wakawa wenye kujuta kwa waliyo yaficha katika nafsi zao.”

[Al-Ma’ida: 52]

Kaka zangu na dada zangu, mgogoro umepamba moto juu ya Hizb ut Tahrir tangu kuasisiwa kwake. Kutokana na vitendo vya watu wengi ambao Mwenyezi Mungu amewapofua uoni wao, kutokana na ukafiri wao, au kwa sababu ya unafiki wao Mwenyezi Mungu akaondoa hisia kutoka katika nyoyo zao, hivyo wakashiriki katika madhambi na uovu wakidhani kuwa wanaweza kuzuia kurudi kwa Khilafah. Walikuwa ni mataifa yaliyo shutushwa na neno la Haki, na makundi na watu binafsi wanaoogopa neno la haki, na makundi yote yawezungukwa na njama yao ovu, na Mwenyezi Mungu Ta’ala ni Mkweli:

[وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ]

“… Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Fatir: 43].

Ama kwa nchi za kikoloni za kikafiri zinazo chukia Uislamu na kurudi kwa dola yake, kwa chuki yao kwa Khilafah mithili ya makruseda, nchi hizi na vibaraka wao wamefanya kila aina ya juhudi iwezekanayo kuchora mbinu ovu na kutengeza mbinu chafu za kuwashtaki wafanyikazi wa dola ya Khilafah, kuwakamata na kuwatesa kufikia hadi ya kupata Shahada ndani ya magereza yao, huku wakati mwengine wakijihalalishia haya kwa madai ya uhalifu wa ugaidi, na nyakati nyingine kwa madai kuwa ni ukanda wa uzalishaji ugaidi. Hivi majuzi walikuja na madai ya ugaidi wa mtandaoni! Na kwamba chama hichi kinajaza kurasa za wanachama wake kwa maoni na fikra za ugaidi zenye kuchochea ghasia, hivyo basi wanawanyanyasa wanachama wa chama hichi katika kurasa zao na kuwaandama kwa kuwakamata na kuwatesa kwa kisingizio cha kutekeleza ugaidi wa mtandaoni! Na kila jicho linaweza kuona kuwa kurasa za wanachama wa chama hichi zinamulika neno la haki na kuonyesha uhalisia, huku kurasa zao watu hawa zikiwa zimejaa utapeli, udanganyifu, uongo na uzushi! Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali, wamepotoka kiasi gani hawa …    

Ama kwa wale wenye nyoyo zinazo ugua, wanafiki na wale wanao eneza uzushi: ukiukaji na uzushi wao haukuanza leo bali zamani, lakini kashfa yao na madai yao ya urongo mwanzoni yalikuwa yameangazia dhidi ya uongozi na maafisa wa chama huku wakihadaa kupitia kuonyesha imani katika fikra na njia ya chama … Hivi ndivyo walivyo jitokeza na kuficha lengo lao halisi, ambalo ni kutingisha mwili wa chama hiki na sio tu uongozi wake pekee. Lakini katika miaka ya hivi karibuni wameanza kushambulia umbo la chama hiki, fikra na njia yake. Wameangazia shambulizi lao juu ya tabanni, Nusra, uongozi wa Ummah, kuhisabu, kikao cha mwezi, nk., na hivyo kujifichua wenyewe kabla ya kufichuliwa na wengine! Lengo walilokuwa wamelificha, ambalo ni kuutingisha mwili wa chama hiki katika fikra na njia yake, limekuwa dhahiri sasa kwa kila anaye weza kuona …Lakini chama hiki kimebakia imara, cha kipekee na chema. 

 [كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا]

“… Ni kama mti mzuri, mizizi yake ni imara, na matawi yake yako mbinguni. Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi…” [Ibrahim: 24-25] Sifa njema zote ziwe kwa Mwenyezi Mungu Mola wa Walimwengu.

Kaka zangu na dada zangu waheshimiwa, nchi za kikoloni za kikafiri na vibaraka wao kamwe hawatapumzika, bali wataendelea kutengeza mbinu chafu, moja baada ya nyingine kwa sababu uzuiaji mafanikio ya chama hiki ya kusimamisha Khilafah ni kadhia nyeti kwao kama ambavyo kusimamisha Khilafah ni kadhia nyeti kwa chama hiki na waumini wote. Maadui wa Uislamu kwamwe hawatakoma njama zao dhidi ya chama hiki na Khilafah, na wataendelea. Ingawa wana uwezo zaidi kuliko sisi katika mbinu, licha ya hayo tuna mambo manne yanayo tupa hakikisho na kutia nguvu azma yetu na kamwe hatutatingishwa na mgogoro au kudhoofishwa na mzozo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu; bali watatuongezea nguvu juu ya nguvu, na upangaji njama ovu utawageukia dhidi yao wenyewe na utawapelekea kuangamia kwao.

[وَقَدْ مَكَرُوا مَكْرَهُمْ وَعِنْدَ اللَّهِ مَكْرُهُمْ وَإِنْ كَانَ مَكْرُهُمْ لِتَزُولَ مِنْهُ الْجِبَالُ]

“Na kwa hakika walifanya vitimbi vyao, na vitimbi vyao anavijua Mwenyezi Mungu. Wala vitimbi vyao si vya kuondosha milima.” [Ibrahim: 46].

Na Hizb inaendelea kutangaza haki na haiogopi lawama ya yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hadi isimamishe tena Khilafah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, licha ya matakwa ya watu hao.

Haya hapa ndio mambo hayo manne:

Jambo la kwanza: Pamoja na uzito huja wepesi, hili liko katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu katika zaidi ya aya moja:

[حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَنْ نَشَاءُ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ الْمُجْرِمِينَ]

“Hata Mitume walipokata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya wakosefu.” [Yusuf: 110].

Hili limethibitishwa kupitia Seerah ya Mtume (saw) kuwa ushindi uko karibu kila uzito unapo ongezeka… Katika Seerah ya Ibn Hisham:

“Ibn Ishaq asema: Khadijah bint Khuwaylid na Abu Talib walifariki mwaka mmoja, na majanga yakamfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa mpigo… hii ilikuwa miaka mitatu kabla ya hijra… Ibn Ishaq asema: Pindi Mwenyezi Mungu Azza wa Jal alipotaka kuifanya Dini yake itawale na kumuimarisha Mtume wake (saw) na kutimiza ahadi yake (swt) … Yeye (saw) alikipokea kikundi cha Al-Khazraj … Yeye (saw) aliwalingania kwa Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal … wakamuitikia na kumkubali …”

Msimu uliofuata, ahadi ya kwanza ya utiifu (Bay’ah) ya Aqaba ikafanyika, kisha ahadi ya pili ya utiifu, kisha Hijra na kusimamisha dola … hivyo basi pindi waumini wanaofanya kazi wanapokabiliwa na uzito ni ishara ya wepesi na ushindi kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Al-Qawi, Al Aziz, Al-Hakim.

Jambo la Pili: Mwenyezi Mungu ameahidi ukhalifah (utawala),

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur: 55].

Mtume (saw) ametoa bishara njema ya Khilafah baada ya utawala wa kiimla tunaoishi chini yake leo: Imepokewa na Ahmad na Abu Dawoud kutoka kwa Hudhayfa kuwa Mtume (saw) amesema:

…»ثُمَّ تَكُونُ جَبْرِيَّةً، فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ، ثُمَّ سَكَتَ«

“…kisha kutakuwepo na utawala wa kutenza nguvu (ملكًا جبرية) na utakuwepo kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha kutakuwepo na Khilafah kwa njia ya Utume.’ Kisha yeye ﷺ  akanyamaza.”

Jambo la Tatu: Ahadi ya Mwenyezi Mungu ya utawala na bishara njema ya Mtume (saw) ya kurudi kwa Khilafah imeandikwa katika Qadar ya Mwenyezi Mungu, katika Elimu yake (swt) katika Al-Lawh al-Mahfoudh. Wakati wake umeandikwa na Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim na hautacheleweshwa. Na kila siku ichapo hutusongeza karibu na wakati huo uliowekwa, na sio kutusongeza mbali nao, na hivyo nafsi zetu zina hamu na kuning’inia katika matarajio haya. 

Jambo la Nne: Mwenyezi Mungu (swt) hatawateremsha malaika kusimamisha Khilafah kwa ajili yetu, bali ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu kuwakirimu wale miongoni mwa watu ardhini wanaostahiki kuisimamisha kupitia mikono yao wenyewe, kwa bidii na kazi ya umakinifu na kuwa na ari na kufanya kazi hii kwa kujitolea. Hizb ut Tahrir inayofanya kazi kwa ajili ya Khilafah kwa idhini ya Mwenyezi Mungu inaistahili na kuistahiki. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kutukirimu kwa ushindi na ufunguzi (Fath) na kwamba tuwe wanajeshi wa Khilafah na kuishuhudia, na Takbir zetu za Idd ziungane na Takbir

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu” [Ar-Rum: 4-5].

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd

Wassalam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Ndugu Yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al Rashtah                                    Mkesha wa 10 Dhul Hijjah 1440 H

Amiri wa Hizb ut Tahrir                                                sawia na 11/8/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:46

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu