Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kupambanua na Kudhihirisha Ukweli wa Wanaozushia Uongo Chama, Uongozi wake na Wabebaji Da’wah wake

Imewasilishwa na Ustadh Abdel Halim Zalloum (Abu Waleed)

Jumatano, 18 Jumada al-Akhar 1441 H sawia na Februari 12, 2020 M

 

[Bofya Picha utizame Video]

Alhamdulillah Rabb Al-Alamiin rehema na amani ziwe juu ya mtukukufu wa Wajumbe, familia yake na maswahaba zake…

Anasema Mwenyezi Mungu (swt) katika Kitabu Chake Kitukufu,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَنْ تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَى مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ)

“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.” [Al-Hujurat: 6]

Imenijia katika fahamu kwamba, jina hili Abdullah Abdullah, ambaye hakutaka kuliweka wazi jina lake la kweli, na ambaye amekuwa akikishambulia chama na uongozi wake, na ambaye anajitambulisha kwamba ndiye mimi, Abdel Halim Zalloum! Hakika huu ni uongo uliyo wazi na uzushi uliosambazwa sana na unafanywa tu na yule ambaye hana hofu na Mwenyezi Mungu (swt) wala kuogopa adhabu Zake…

Nashtakia kuhusiana na huyu mtu asiye julikana akitumia jina la Abdullah Abdullah, ambaye hakutaka kutumia jina lake halisi, na pia kwa yeyote ambaye husambaza taarifa zake kwa kueneza uongo. Nina washtaki wote hawa kwa Mwenyezi Mungu (swt) Ambaye ni Al-Muntaqim Al-Qahhar. Nawakumbusha kuhusu Hadith ya Mtume (saw) kwa kila mwenye kuzungumza mambo ya uongo:

Bukhar amevua katika Sahih yake kutoka kwa Mansour aliyepokea kutoka kwa Abi Wael aliyepokea kutoka kwa Abdullah (ra) kwamba Mtume (saw) alisema:

«إِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَصْدُقُ حَتَّى يَكُونَ صِدِّيقًا وَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ كَذَّابًا».

Ukweli hupelekea katika haki, na haki hupelekea katika Pepo.  Na binadamu ataendelea kuongea ukweli mpaka anakuwa mtu mkweli. Uongo hupelekea katika Al-Fajur (mfano uovu, kutenda uovu) na Al-Fajur (uovu) hupelekea katika Moto wa Jahannam, na binadamu ataendelea kuongea uongo mpaka ataandikwa kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa ni Mtu muongo”.

Mwisho, napenda nirekodi ujumbe huu katika sauti na video, ili kuweka wazi ukweli wa aliye tenda kosa hili la kudhalilisha utu wa mtu kwa kutumia jina langu. Kwa kufanya hivi huenda yeye pamoja na wote ambao wanamuunga mkono watatahayari mbele za Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake ((saw), na Waumini ambao wapo makini kuchunga mipaka na wala hawasemi uongo.

Jumatano, 18 Jumada al-Akhi 1441H sawa na Februari 12, 2020M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 01 Agosti 2020 12:54

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu