Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 24/07/2024

Maoni ya habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli… Kataeni demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, irudishe ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 18 Muharram Tukufu 1446 H sawia na 24 Julai 2024 M

Lengo la Kujitoa Muhanga kwa Imam Husein (ra) na Familia ya Mtume (ra) ilikuwa ni Kuilinda Khilafah Rashida


Mnamo tarehe 16 Julai 2024, Waziri Mkuu alizungumza juu ya kujitoa muhanga mkuu kwa Imam Husein (ra). Hata hivyo, watawala wa sasa hawakubali somo kuu la muhanga huu. Kujitolea muhanga kwa Familia ya Mtume (saw) kumethibitisha kwamba yule anayenyakua mamlaka katika Khilafah Rashida hawezi kukubaliwa. Basi vipi kutokuwepo kwa Khilafah Rashida yenyewe kutakubaliwa? Leo Waislamu wanateseka chini ya utawala wa mifumo ya makafiri na watawala madhalimu. Ni juu ya majeshi ya Waislamu kusimama pamoja na Umma wa Kiislamu dhidi ya wanyang'anyi wa leo. Majeshi lazima yatoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah Rashida, ili kukomesha utawala wa dhulma na uasi kwa Mwenyezi Mungu ﷻ.

12 Muharram Tukufu 1446 H - 18 Julai 2024 M

Demokrasia Imefeli Kabisa Kuwalinda Waislamu na Uislamu


Mnamo tarehe 17 Julai 2024, Wizara ya Mambo ya Nje alilaani dhidi ya Afghanistan, baada ya Waislamu kuwaua Waislamu katika Jimbo la Bannu mnamo Julai 15, 2024. Pakistan ni dola iliyofeli kwa sababu ya Demokrasia. Waislamu wanapigana na Waislamu, huku Mabaniani wakiwakandamiza Waislamu huko Kashmir, na Mayahudi wanawachinja Waislamu huko Palestina. Uchumi umesimama kwenye ati ati ya kuporomoka. Waislamu wanakandamizwa chini ya kodi kali. Bei za umeme na petroli zinapanda sana. Mahakama, vyama vya siasa, uongozi wa kijeshi na serikali ya kiraia wote wameingia katika mapambano makubwa ya kuwania madaraka. Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Sasa ni wakati wa kuondoa mfumo huu dhalimu na walinzi wake. Fuateni nyayo za Saad bin Muadh (ra), ambaye alitoa Nusrah yake kwa ajili ya Uislamu. Ipeni Nusrah Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida.

13 Muharram Tukufu 1446 H - 19 Julai 2024 M

Utoaji wa Haki Haraka Unataka Kuondolewa kwa Mahakama iliyojengwa juu ya Sheria ya Kiingereza, na Kuanzisha Mahakama za Sharia za Khilafah Rashida


Tume ya Mahakama ya Pakistan (JCP) ilikutana mnamo tarehe 19 Julai 2024, kujadiliana kuhusu uteuzi wa majaji waliostaafu kutokana na idadi kubwa ya kesi zinazoendelea. Kwa sasa kuna kesi milioni 2.26 zinazosubiri katika mahakama za Pakistan. Milioni 1.86 ziko katika mahakama za wilaya, huku kesi 390,000 zikiendelea katika Mahakama Kuu, Mahakama ya Upeo na Mahakama ya Sheria ya Shirikisho. Kesi zingine zimekuwa zikisikilizwa kwa miongo kadhaa, huku walalamishi na washtakiwa wamekufa wakisubiri haki. Je, kuna yeyote bado anayedai kwamba mahakama zilizoachwa nyuma na Raj mkoloni Muingereza zinaweza kutoa haki haraka? Kucheleweshwa haki ni kunyimwa haki. Mahakama za Shariah za Khilafah zinatoa haki haraka. Kwa zaidi ya miaka elfu moja, Khilafah ilisuluhisha kesi kwa haraka na kwa uadilifu, huku ikitokomeza uhalifu kikamilifu.

14 Muharram Tukufu 1446 H - 20 Julai 2024 M

Khilafah Rashidah Itakomesha Muungano na Maadui wa Waislamu


Katika Taarifa yake kwa Vyombo vya Habari Toleo Na. 20240719 - 01, CENTCOM ya Marekani ilitangaza mnamo tarehe 18 Julai 2024, “Jenerali Kurilla alisisitiza fursa za kimkakati zilizopo katika ushirikiano wa kijeshi wa Marekani na ‘Israel’.” Marekani inalipa umbile la Kiyahudi silaha, fedha na usaidizi wa vyombo vya habari huku ikifanya mauaji ya halaiki huko Gaza. Mwenyezi Mungu (swt) amesema, ِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ “Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah al-Mumtahina 60:9]. Khilafah Rashida itaondoa uwepo wa jeshi na ujasusi wa Marekani kutoka katika ardhi za Waislamu.

15 Muharram Tukufu 1446 H - 21 Julai 2024 M

Gaza Inahitaji Uhamasishaji wa Majeshi, Sio Matangazo


Mnamo tarehe 19 Julai 2024, serikali ya Pakistan ilimtangaza Netanyahu kuwa gaidi. Watawala wako chini ya shinikizo la matakwa ya Waislamu kuhamasisha majeshi. Jeshi la Mayahudi, lenye silaha nzito, lazima likabiliwe na jeshi la Waislamu, lenye silaha nzito. Jeshi la Mayahudi lazima lifukuzwe kutoka Palestina yote. Mwenyezi Mungu (swt) aliamrisha, وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ Na muwatoe popote walipo kutoeni[Surah Al Baqarah 2:191] Wajibu wetu ni kuwasiliana na jamaa na marafiki zetu katika jeshi. Ni lazima tuwatake watoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida. Khalifa Rashid ataukusanya Ummah na majeshi yake kukomboa ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu.

16 Muharram Tukufu 1446 H - 22 Julai 2024 M

Khilafah Rashidah Itamakinisha Utawala Wake Ulimwenguni Katika Teknolojia ya Habari


Hitilafu ya kompyuta duniani kote iliyoathiri viwanja vya ndege, benki na biashara nyingine mnamo tarehe 19 Julai 2024 ilihusishwa na sasisho la programu kwa huduma za Microsoft cloud lililotolewa na kampuni ya usalama wa mtandao ya Marekani ya CrowdStrike. Tukio hili linaangazia ukiritimba wa kampuni fulani za Marekani kwenye teknolojia ya habari ya kimataifa. Dola kote ulimwenguni zinategemea makampuni ya Marekani, ambayo pia hutumiwa kupeleleza serikali, wanajeshi, wafanyibiashara na watu binafsi. Khilafah Rashida itamaliza utawala wa Marekani wa miundombinu ya kimataifa ya teknolojia ya habari, kwa kuzingatia sekta ya kijeshi na teknolojia zinazohusiana, ikiwa ni pamoja na akili ya bandia (artificial intelligence) na kompyuta ya kiasi. Khilafah haitakubali aina yoyote ya kutawaliwa na makafiri. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ, وَلَن يَجْعَلَ ٱللَّهُ لِلْكَـٰفِرِينَ عَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ سَبِيلًا “Wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisa 4:141]

17 Muharram Tukufu 1446 H - 23 Julai 2024 M

Je, ni lini Umma na Majeshi Yake Watajibu Mauaji ya Gaza?


Mnamo tarehe 22 Julai 2024, Pakistan ilikaribisha Maoni ya Ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu “Matokeo ya Kisheria yatokanayo na Sera na Matendo ya “Israel” katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki.” Kwa hivyo, vibaraka wa Marekani nchini Pakistan wanakaribisha uamuzi usio na meno wa taasisi ya kikoloni. Kuhusu bwana wao, Marekani, imewezesha mauaji huko Gaza, kwa kutoa habari za kisiasa na vyombo vya habari, pamoja na silaha na ufadhili. Majeshi ya Waislamu lazima yawapindue vibaraka wa Marekani na kutoa Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Kwa haya watapata utukufu wa dunia na neema ya Akhera. Amesema Allah ﷻ ,  لِمِثْلِ هَذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَKwa mfano wa haya nawatende watendao.” [Surah Saffat 37:61]

18 Muharram Tukufu 1446 H - 24 Julai 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu