Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:

Ripoti ya Habari 16/04/2022    

Mnamo tarehe 15 Ramadhan 1443 H, katika Ukumbi wa Jiji la Dosa, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ilifanya iftar ya Ramadhan ya kila mwaka, iliyohudhuriwa na mkusanyiko mkubwa wa wanasiasa, wanahabari, wanazuoni, viongozi wa taasisi za kiraia, na wengineo wanaohusika na mambo ya umma, pamoja na mashababu wa Hizb ut Tahrir. Baada ya kufuturu na kuswali swala ya Maghrib, hafla ya kisiasa iliyopewa anwani

“Handaki la Mgogoro wa Kisiasa nchini Sudan, Lango Pekee la Kutokea ni Khilafah”

ikaanza. Hafla hii ilianza kwa kisomo cha Quran Tukufu na Sadiq Qasam Al-Sayyid – mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Kisha Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akachukua usukani; Mzungumzaji wa kwanza, Mhandisi Basil Mustafa, aliwasilisha waraka wenye kichwa: "Mamlaka Iliyonyakuliwa ya Ummah ni chombo cha ushawishi wa kisiasa kwa ukoloni" ambayo Mhandisi Basil aliwasilisha maelezo kamili ya jinsi mamlaka yalivyo nyakuliwa na kafiri  mkoloni, tangu kuvunjwa kwa dola ya Khilafah hadi leo, ambapo nchi za Magharibi zimekuwa zikinyakua mamlaka ya umma kwa kutumia zana.

Mhandisi Basil Mustafa

Mamlaka Iliyonyakuliwa ya Ummah ni chombo cha ushawishi wa kisiasa kwa ukoloni

Kisha waraka wa pili ulikuwa na kichwa: “Hadhara ya Magharibi Kafiri... mangati ambayo mwenye kiu kudhani kuwa ni maji,” ambapo wakili Ustadh Hatim Jaafar (Abu Awab) – mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alieleza kwamba Umma wa Kiislamu umeishi katika kivuli cha hadhara ya kikafiri ya Magharibi kwa zaidi ya miaka mia moja hadi vizazi vikaibuka.

Ustadh Hatim Jaafar (Abu Awab)

Hadhara ya Magharibi Kafiri... mangati ambayo mwenye kiu kudhani kuwa ni maji

Kisha waraka wa tatu na wa mwisho ulikuwa na kichwa: "Khilafah... Lango la Kutoka Salama kutoka kwenye Handaki la Giza", ambao uliwasilishwa na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akionyesha kwamba mfumo wa utawala katika Uislamu ni Khilafah, na ni uongozi mkuu kwa Waislamu wote duniani, ni faradhi, na ni dola ya kipekee katika umbo lake, vyombo na vifungu yake.

Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil)

Khilafah... Lango la Kutoka Salama kutoka kwenye Handaki la Giza

Ushiriki wa Hadhira

Kipindi cha Maswali na Majibu

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu