Alhamisi, 16 Rajab 1446 | 2025/01/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ripoti ya Habari ya Sudan

Muendelezo wa amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan katika wilaya na mikoa mbali mbali ya nchi ili kujenga rai jumla yenye ufahamu juu ya hukmu za Uislamu na suluhu zake zinazohusiana na mifumo mbali mbali ya maisha, ambazo zimeshughulikia mgogoro ya utawala na mipango inayopendekezwa kuutatua, na maafa ya mafuriko na mvua zilizonyesha katika mikoa mbalimbali nchini...

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliweka katika vyuo vikuu kona ya mazungumzo na majadiliano katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Mafunzo ya Kiuchumi, yenye kichwa: "Mpango wa Mzuri wa Mshawishi na Udandiaji Wimbi", mnamo Agosti 8, 2022, ambapo Ustadh Al-Fateh Abdullah, alianza mazungumzo yake kuhusu mpango huo, ambao ni wa saba baada ya mapinduzi ya Al-Burhan, alizungumzia Oktoba 25, mpango wa Chama cha Umma, mpango wa Volcker, Muungano wa Afrika, chombo cha kiserikali (IGAD), mpango wa maprofesa wa vyuo vikuu, na mengineyo kutoka dola ya Sudan Kusini, ambao yote inalingania suluhu ya kisiasa na mgao kati ya wagomvi na matokeo yake ni sifuri katika suluhisho. Alionyesha kwamba Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba ya Kiislamu yenye ibara 191 zilizotolewa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw). Alifafanua aina ya utawala na vyombo vya dola ya Khilafah katika utawala, idara, mfumo wa kiuchumi na mifumo mingine ya maisha.

Chini ya mada: "Mvutano  wa Mamlaka nchini Sudan", Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walitoa hotuba ya kisiasa katika eneo la Omdurman Magharibi huko Souk Libya mnamo Agosti 8, 2022 ambapo Ustadh Ishaq Muhammad alielezea hali ya Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu baada ya mapinduzi ya Kiarabu ambapo watu walidai mabadiliko, lakini walikatishwa tamaa na hawakuleta mabadiliko ya kweli, na nchi yetu ya Sudan ni shahidi bora wa hilo. Alisema mipango yote iliyoanzishwa haitatatua tatizo hilo kwa sababu hakuna tofauti kati ya nguvu na mamlaka, kwani sultan wa taifa ndiye anayechagua nani aliongoze kwa Sharia na dini, hivyo basi tunawahutubia Waislamu kuregelea Quran na kuhukumu kwa Sharia yake kupitia dola yake, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Mbele ya uwepo mkubwa na utendaji mwanana, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliweka kona ya mazungumzo na majadiliano katika vyuo vikuu yenye kichwa: "Meza ya Kongamano na Majaribio ya Wenye Uzoefu, Hivyo Suluhisho ni Nini? " katika Chuo Kikuu cha Al-Neelain, Kitivo cha Biashara, mnamo Agosti 18, 2022, ambapo Mhandisi Basil Mustafa alihutubia uhalisia wa mipango ambayo Meza ya Kongamano ilifanyika katika Ukumbi wa Urafiki mnamo Jumamosi na Jumapili, Agosti 13-14, na kuonyesha kuwa haikutoa suluhisho kwa shida za watu; bali ni kwa ajili ya kupumbaza na kugawanya madaraka na mali miongoni mwa wagomvi. Ama mzungumzaji wa pili, Ust. Al-Fateh Abdullah alianza mazungumzo yake kuhusu ukweli wa mazungumzo haya na mipango hii ambayo haikuegemezwa juu ya msingi wa Uislamu ni batili kwa mtazamo wa Sharia, na kwamba imeharamishwa na Sharia. Kisha akaeleza suluhisho la mgogoro wa kisiasa nchini; ni mgogoro wa kikatiba.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan waliweka kituo cha majadiliano ya umma katika vyuo vikuu Katikati mwa mji (Khartoum) jioni ya Agosti 21, 2022, ambapo Mashababu walielezea fikra za Kiislamu ambazo zinashughulikia matatizo ya maisha chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na kulikuwa na uungaji mkono wa fikra za Hizb kutoka kwa vijana waliohudhuria na walionyesha hamu yao ya kuwasiliana na mashababu wa Hizb. Ilikuwa ni hatua nzuri mno ya mazungumzo.

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu