Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Kongamano la Kiuchumi Mjini Şanliurfa Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa kongamano la kiuchumi katika ukumbi wa Hoteli ya Rouhi mjini Şanlıurfa lenye kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi!" sanjari na mnasaba wa kumbukumbu ya miaka wa 101 wa Hijria wa kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Muharram 1342 H.

Kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, watu wa mji wa Şanlıurfa walionyesha kupendezwa sana na mfululizo wa makongamano yaliyofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Migogoro ya Kiuchumi" ambapo walimiminika kwenye ukumbi wa mkutano hadi kujaa pomoni.

Kongamano lilianza chini ya usimamizi wa mwandishi mkuu wa jarida la Kokludegisim Mehmet Goçman, kwa kusoam kisomo kizuri cha aya za Quran Tukufu, kisha mwandishi wa jarida la Kokludegisim, Ustadh Mustafa Koçuk, alipanda jukwaa na kuwasalimu wageni kwa hotuba ya ufunguzi, ikifuatiwa na hotuba ya Dkt. Abdul Rahim Shin kwa anwani "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Migogoro ya Kiuchumi", ambapo alijadili kwa kutoa mifano kutoka karne 13 za historia ya Kiislamu akilini kwamba nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu ndio nidhamu sahihi na yenye mafanikio zaidi kuwahi kutokea, na akadhihirisha kwa kutaja mifano ya kitakwimu na mifano ya rai jumla, kwamba muhusika pekee anayehusika na mtikisiko wa kiuchumi unaoikumba dunia leo na unaoikumba Uturuki kwa sasa ni nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali, na khiyana ya watawala kwa hazina ya serikali. Shen alisema kwamba hata kama matajiri wangetoa zaka kwa tarakimu pekee, wangewaokoa watu kutokana na taabu, na huu ndio wajibu wa dola yenyewe. Alisimulia jinsi Dola ya Kiislamu ilivyotangaza vita dhidi ya wale waliokataa kutoa zaka katika zama za Khilafah ya Abu Bakr, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi.

Baada ya hotuba ya Dkt. Abdul Rahim Shin, Ustadh Abdullah Imamoglu, mwandishi wa kitabu “Sunnah ni Chimbuko la Maisha katika Uislamu na Elimu ya Kisiasa ya Muislamu,” aliwasilisha hotuba yenye kichwa “Utabikishaji Nidhamu ya Kiuchumi ya Kiislamu” ambapo alitaja riwaya fupi kutoka katika historia ya Uislamu uliotawala kwa muda wa karne 13, zikionyesha kwamba Uislamu una nidhamu yake ya kiuchumi na ilitabikishwa chini ya utawala wa Khilafah, na kwamba maadili na uaminifu ndivyo vilivyotawala katika jamii ya Kiislamu, hivyo wakajiepusha kutokana na kugusa hata uzi kutoka katika Bait ul Mal. Baada ya mifano hiyo, Imamoglu aliregea siku za sasa na kueleza jinsi watawala waliotabikisha mfumo wa kisekula wa kirasilimali walivyopora hazina ya dola bila ya kumuogopa Mwenyezi Mungu (swt), alidhihirisha wazi tofauti kati ya urasilimali wa kisekula na mfumo wa Uislamu.

Katika makongamano na programu zetu tulizoziandaa ndani ya wigo wa kampeni yetu kwa anwani "Masuluhisho ya Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi," ambayo imedumu takriban miezi miwili, tumejaribu kufafanua tofauti kati ya haki na batili kwenye kila jukwaa, na kwamba chanzo kikuu cha tatizo ni mfumo wa kisekula wa kirasilimali, na suluhisho msingi ni Uislamu na nidhamu yake ya kiuchumi.

Tungependa kuwashukuru washiriki walioshiriki katika programu ya kongamano na mjadala na wakaonyesha kuwa na hamu kubwa, na wageni wetu ambao walisikiliza programu kwa subira kwa saa nyingi wakiwa wamesimama kutokana na msongamano wa watu, na waandishi wetu waheshimiwa ambao walisafiri kutoka jiji hadi jiji kuwafahamisha Waislamu kuhusu masuluhisho ya kweli ya Kiislamu ya migogoro ya kiuchumi ambayo yalitayarishwa kwa juhudi kubwa.

Kongamano lilihitimishwa kwa kumuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kusimama kwa Dola ya Khilafah Rashida, itakabikisha upya mfumo huu.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumamosi, 25 Rajab Tukufu 1443 H – 26 Februari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu